Blog - Page 19 of 20 - Fahamu Hili
Saturday, August 30Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Blog

Utafiti: Karatasi Zinazobandikwa Ukutani Zinaweza Kusababisha Ugonjwa

Utafiti: Karatasi Zinazobandikwa Ukutani Zinaweza Kusababisha Ugonjwa

Afya, Habari
Utafiti umebaini kuwa sumu zinazozalishwa na kuvu(fangus) zinazojizalisha kwenye karatasi za ukutani katika nyumba zetu zinaweza kuharibu hewa na kuiingia mwilini kwa urahisi, na kusababisha "maradhi ya jengo;". Maradhi ya jengo hutumiwa kuelezea hali ambayo wakazi wa jengo wanajihisi madhara makubwa ya afya ambayo yanaonekana kuwa yanahusishwa moja kwa moja na wakati waliotumia katika jengo fulani. "Tulionyesha kwamba sumu ya mycotoxins inaweza kuhamishwa kutoka vifaa vya vilivyo ukutani kwa hewa, katika ya hali ambayo inaweza kukutana na binadamu katika majengo," alisema Jean-Denis Bailly, Profesa katika Shule ya Veterinary School ya Toulouse nchini Ufaransa. "Kwa hiyo, mycotoxins inaweza kuvutwa na binadamu na inapaswa kuchunguzwa kama vigezo vya kupima ubora wa hewa ya nda...
Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Maendeleo Binafsi, Tija
Mafanikio yana maana mbalimbali kwa kila mtu; kama vile uzuri unavyotofautiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine. Ni jukumu lako kubainisha ni nini maana ya mafanikio na ni kwa namna gani utayafikia mafaniko hayo. Fuatana nami nikushirkishe vitu 10 vinavyozuia mafaniko yako kama unataka kuona na kufikia mafanikio yako. 1. Kutoa visingizio Acha kulaumu na kulalamikia watu wengine kwa kutokupata kile unachokihitaji. Acha kusingizia serekali na jamii kuwa ndiyo kikwazo cha wewe kufikia mafanikio yako. Watu waliofanikiwa hawalalamiki bali wanafanya kazi kwa bidii kufikia malengo yao. Kumbuka hakuna mtu aliyefanikiwa sana duniani kwa kusaidiwa na serikali au mtu fulani katika jamii; ukiwepo msaada basi utumie tu kama ngazi. 2. Kutazama tu mapungufu Umejijengea dhamiri ya kutofanya c...
Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Maendeleo Binafsi, Tija
Miaka kadhaa iliyopita mawasiliano yalikuwa magumu na ya gharama kubwa. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, mawasiliano yamerahisishwa na kuwa ya uhakika zaidi huku ghrama pia ikipungua. Kuwepo wa mtandao wa intaneti pamoja na mitandao ya kijamii kumewafanya watu kukaribiana zaidi. Baada ya kuanzishwa kwa mtandao wa Facebook ambao ulianzia huko Marekani na baadaye kuenea dunia nzima maisha ya watu yamebadilika sana. Facebook ina watumiaji hai zaidi ya bilioni 1.23 na bado Facebook inalenga kuwaongeza zaidi ili kuwafikia watu wote duniani. Pamoja na maendeleo haya makubwa kumeshuhudiwa madhara au changamoto kadha wa kanda zinazotokana na mitandao ya kijamii hasa Facebook. Hivyo basi hapa nitafafanua sababu kadhaa zinazodhihirisha ni kwa namna gani Facebook inakup...
Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka

Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka

Afya
Kwanini ni muhimu kunywa maji? Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo. Ninawezaje kutumia maji kama tiba? Unaweza kutumia maji kama tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo: Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka. Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni. Kama huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza tar...
Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Uteuzi wa jina la biashara ni hatua muhimu kama ilivyo kwa jiwe la pembeni katika nyumba. Watu wengi wamekuwa hawatilii maanani mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua jina la biashara au kampuni. Nimekuwa nikishuhudia makapuni mengi yakitumia majina ya ajabu ajabu yasiyoendana na biashara zao. Kwa sehemu kubwa kufanikiwa na kujulikana kwa biashara yako kunategemea jina la biashara yako. Fuatana nami katika makala hii ambayo nitakueleza mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua jina la biashara. 1. Uhusiano wa jina na bidhaa au huduma Je unafahamu kwamba jina la biashara linatakiwa liakisi huduma au biashara unayoifanya? Ni jambo jema kutumia jina linaloakisi kile unachokifanya. Kwa mfano jina kama vile “Samelctro” lifaa kwa kampuni ya vifaa vya kielektroniki, “Pamba L...
Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Maendeleo Binafsi, Tija
Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako. Ni kweli kuwa baadhi ya watu huanza maisha katika mazingira rafiki zaidi, lakini ninaamini kila mmoja ana nafasi na uwezo ya kufanikiwa. Haya ni baadhi mambo ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya na kujiambia na yamewatenga na mafanikio yao. 1. Ninahitaji shahada ya chuo kikuu ili kufanikiwa Unahitaji shahada kupata kazi katika ofisi fulani lakini si kuwa majasiriamali katika ofisi yako wewe mwenyewe. Ipo mifano kadha wa kadha duniani ya watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wakubwa bila kuwa na shahada ya chuo kikuu. Mfano wa watu hao ni Mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg. Hivyo basi fanya maamuzi leo ili ufikie kiwango bora cha...
Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda

Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda

Maendeleo Binafsi
Mambo yote katika maisha yetu yamefungwa kwenye muda, hivyo ni vyema kufahamu namna bora ya kutumia muda kwa njia yenye mafanikio. Kutumia muda vyema siyo tu kutakuwezesha kufanya kazi vyema, bali kutakuwezesha kuishi maisha vyema. Ni muhimu kupata muda wa kufanya mambo yote ya muhimu kwenye maisha yako, kwani kila moja lina nafasi na umuhimu wake. Hapa nitaeleza kanuni 9 yatakayokuwezesha kutawala muda vyema. 1. Anza na panga siku yako vyema Usikimbilie kuanza majuku yako ya siku bila kukaa chini na kutumia dakika chache za kutafakari mambo kadhaa. Tafakari ni jambo gani muhimu zaidi ili uweze kulipa kipaumbele katika siku yako. Jifunze kujiwekea malengo, haya yatakuwezesha kujua nini unachotakiwa kukitimiza ndani ya siku yako. Kwa njia hii utaweza kukamilisha vitu kulingana na muda...
Njia 3 za Kutengeneza Pesa kwa Kutumia YouTube bila Adsense

Njia 3 za Kutengeneza Pesa kwa Kutumia YouTube bila Adsense

Kipato, Tovuti na Blogu
Watengenezaji wengi wa video wanajua jisi ilivyo vigumu kutengeneza pato la uhakika kupitia Youtube kwa kutumia Adsense pekee. Watengenezaji wengi wa video wamekuwa wakifikiri kuwa kupakia video zenye ubora sana kwenye mtandao wa YouTube kutawafanya kupata fedha lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo. Ni vigumu kujua ni kiasi gani unaweza kupata kutokana na Adsense kwenye YouTube, lakini unaweza kukadiria kwa video kutazamwa mara elfu moja utapata takribani dola moja. Kiasi hiki ni kidogo ukilinganisha na kazi utakayokuwa umeifanya ili kukipata. Tazama njia tatu nitakazokueleza zitakazokuwezesha kupata fedha kwenye mtandao wa YouTube bila kutumia Adsense. 1. Mshirika au Wakala Unaweza kupata fedha kwenye YouTube kwa njia ya kuwa mshirika au wakala wa makapuni mbalimbali yanayozalis...
Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Inawezekana una wazo zuri sana la biashara na unatamani kulitekeleza haraka kadri iwezekananavyo. Pengine umeajiriwa katika taasisi au ofisi fulani na unashauku kubwa ya kuacha kazi ili uweze kuanzisha kampuni au biashara yako. Kabla hujafanya maamuzi yoyote ni vyema ukae chini na utafakari mambo kadhaa ambayo yatakuwa na manufaa makubwa kwako. Katika makala hii nitakueleza mambo 7 muhimu ambayo utahitajika kuyafanya kabla ya kuanza biashara yako. 1. Chagua wazo la biashara vyema Katika eneo ambalo watu wengi hukosea wakati wanapoanzisha kampuni au biashara ni uchaguzi wa wazo la kibiashara. Unapochagua wazo baya au usilolimudu, ni wazi kuwa hutoweza kulitekeleza na kupata faida. Hakikisha wazo unalolichagua unalimudu vyema pia linatekelezeka. Epuka kuchagua wazo pana sana au...
Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Afya
Watafiti wa afya nchini Marekani wamesema matumizi ya mafuta ya nazi si salama kwa afya kama ilivyo kwa nyama ya ng’ombe na siagi. Shirika la Moyo la Marekani (AHA), limeeleza kuwa mafuta yaliyoko kwenye nazi yanaweza kuongeza lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa AHA, wanadai kuwa kuna mafuta 82% katika nazi. Kuna zaidi ya 63% kwenye siagi, 50% kwenye nyama ya ng’ombe na 39% kwenye nyama ya nguruwe. Wataalamu hao wameongeza kuwa mafuta hayo yanaweza kusababisha lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu. Baadhi ya watu hudai kuwa ulaji wa mafuta ya nazi una manufaa kwa afya ya mlaji lakini AHA wamesema madai hayo hayajadhibitishwa. Wamependekeza kuwa, watu wajitahidi kupunguza kiasi cha mafuta yenye lehemu wanayoyatumia kila siku katik...