Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako - Fahamu Hili
Thursday, May 23Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Washirikishe Wengine Makala Hii:

fb

Miaka kadhaa iliyopita mawasiliano yalikuwa magumu na ya gharama kubwa. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, mawasiliano yamerahisishwa na kuwa ya uhakika zaidi huku ghrama pia ikipungua.

Kuwepo wa mtandao wa intaneti pamoja na mitandao ya kijamii kumewafanya watu kukaribiana zaidi.

Baada ya kuanzishwa kwa mtandao wa Facebook ambao ulianzia huko Marekani na baadaye kuenea dunia nzima maisha ya watu yamebadilika sana.

Facebook ina watumiaji hai zaidi ya bilioni 1.23 na bado Facebook inalenga kuwaongeza zaidi ili kuwafikia watu wote duniani.

Pamoja na maendeleo haya makubwa kumeshuhudiwa madhara au changamoto kadha wa kanda zinazotokana na mitandao ya kijamii hasa Facebook. Hivyo basi hapa nitafafanua sababu kadhaa zinazodhihirisha ni kwa namna gani Facebook inakupunguzia tija.

1. Facebook hupoteza muda

Fikiri wakati unaperuzi kwenye ukurasa wa Facebook, ukitazama vitu kadha wa kadha vilivyowekwa watu wengine; wakati mwingine unajisikia kama ni lazima kutoa maoni au kupenda kila kilichochapishwa.

Fikiri juu ya muda huu unaoutumia, muda ambao ungeweza kuutumia kwenye kazi nyingine yenye tija zaidi kama vile kujifunza kitu kipya au kutimiza majukumu yako ya kila siku.

Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

2. Facebook inaweza kupunguza dhamira yako

Umekuwa ukitembelea Facebook mara kwa mara na kukutana na marafiki au watu wako wa karibu wakionyesha picha au kuandika juu ya mafanikio yao kila mara; unapoendelea kutazama, hili linaweza kuondoa hamasa yako ya ndani.

Kwa kutazama machapisho kama haya kutakufanya uhisi kuachwa nyuma au kukwama katika kufikia mafanikio yako kama wenzako wanavyojionyesha.

Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

3. Kujishughulisha na watu wasiokuwa na maana

Hebu fikiri juu ya orodha ya marafiki ulio nao kwenye mtandao wa Facebook, je ni wote wanakupa kitu cha kufaa katika maisha yako? Je ni wote unawahitaji kwa sasa?

Unaweza kujikuta unatoa maoni, unapenda na kusambaza machapisho ya watu ambao kimsingi hawana tija yoyote kwako.

4. Facebook inakufanya kujishughulisha na vitu visivyo na tija

Kuna mamilioni vitu kwenye mtandao wa Facebook, lakini ni vichache sana vina tija na manufaa kwa ajili ya maisha yako.

Jiulize unapoteza muda wako kutazama kurasa za udaku au picha za ngono za watu fulani fulani, hizi zina tija yoyote kwako?. Kuna vitu vingi sana vyema na vyenye manufaa vya kujifunza na kufanya badala yake.

5. Facebook inaharibu uwezo wa kuwasiliana

Kuna uwezekano wa mtu kuzoea kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook kuwasiliana hadi kufikia kushindwa kuwasiliana vyema katika mazingira ya kawaida.

Wakati mwingine hata mtu anaweza kushindwa kusimama na kuzungumza mbele ya watu kwa kukosa uzoefu wa mawasiliano ya ana kwa ana.

Soma pia: Njia 10 za Kujenga Uwezo wa Kuzungumza Mbele ya Watu.

6. Facebook hukufanya mtumwa wa machapisho yako

Kwa kawaida watu hupenda kupata penda (likes) na maoni (comments) nyingi katika machapisho yao. Hivyo kwa njia hii watu hujikuta wakitumia muda na rasilimali kadhaa kama vile gharama za kuhariri picha ili ikubalike kwa watazamaji. Kwa kufanya hivi unajikuta unatumikishwa kwa njia moja au nyngine na Facebook.

7. Facebook hupoteza faragha ya mtu

Kuna wakati mtu anajenga mazoea ya kushirikisha vitu na matukio mbalimbali ya maisha yake kiasi cha kupoteza faragha. Mambo kama kuoga, kuvaa, kufanya tendo la ndoa, matibabu ndani ya chumba cha daktari, picha za maiti n.k.

Haya ni badhi tu ya mambo ambayo hayana mashiko sana kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii. Lakini hivi leo hali ni tofauti kwani watu huweka hata picha za ndani sana ambazo zisingestahili kuwekwa kwenye Facebook.

Soma pia: Vitu 11 Unavyotakiwa Kutoviweka Kwenye Mitandao ya Kijamii.

Hitimisho

Ni wazi kuwa kama hauchukui hatua stahiki wakati unapotumia mtandao wa Facebook, utajikuta katika hali ya Facebook kuwa sehemu ya maisha yako usiyoweza kutengwa nayo.

Mtandao wa Facebook una manufaa kadhaa licha ya kuwa na changamoto hizi lakini unahitajika kuwa makini na namna unavyoutumia mtando huu ili kulinda maisha yako ya sasa na baadaye.

Je una maoni gani kuhusu makala hii? Tafadhali tupe maoni yako kisha washirikishe wengine makala hii. Karibu pia ufuatilie ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

2.5 2 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x