Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa - Fahamu Hili
Monday, May 25Maarifa Bila Kikomo

Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Washirikishe Wengine Makala Hii:

dn

Mafanikio yana maana mbalimbali kwa kila mtu; kama vile uzuri unavyotofautiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine. Ni jukumu lako kubainisha ni nini maana ya mafanikio na ni kwa namna gani utayafikia mafaniko hayo.

Fuatana nami nikushirkishe vitu 10 vinavyozuia mafaniko yako kama unataka kuona na kufikia mafanikio yako.

1. Kutoa visingizio

Acha kulaumu na kulalamikia watu wengine kwa kutokupata kile unachokihitaji. Acha kusingizia serekali na jamii kuwa ndiyo kikwazo cha wewe kufikia mafanikio yako. Watu waliofanikiwa hawalalamiki bali wanafanya kazi kwa bidii kufikia malengo yao.

Kumbuka hakuna mtu aliyefanikiwa sana duniani kwa kusaidiwa na serikali au mtu fulani katika jamii; ukiwepo msaada basi utumie tu kama ngazi.

2. Kutazama tu mapungufu

Umejijengea dhamiri ya kutofanya chochote kwa kuwa wewe unaona tu matatizo. Kwa hakika katika ulimwengu huu kila kitu kina pande mbili; unachotakiwa kufanya ni kuyaona matatizo kwa jicho la mafanikio.

Badili mtazamao wako sasa epuka kuona tu matatizo na mapungufu ili uweze kufanya mambo yenye tija kwa ajili ya mafanikio yako.

3. Kuogopa kushindwa

Mara nyingi napenda kuwashauri watu kuwa ni bora kujaribu ukashindwa kuliko kushindwa hata kujaribu. Umekuwa haufanyi kitu chochote kwa kigezo kuwa unaogopa kushindwa; hakika hotofanikiwa kwani maisha yako yatamalizika wakati hujafanya chochote.

Je ulishwahi kufikiri kila mtu ulimwenguni angewaza kama wewe? Dunia hii isingekuwa na ugunduzi wala maendeleo yoyote.

Mwanasayansi Thomas Edison alijaribu mara 1,000 kutengeneza balbu ya umeme hadi alipofanikiwa. Je kwanini wewe hujajaribu hata mara moja? Anza kufanya leo na utaona matokeo yake.

Soma pia: Mambo 25 Unayoweza Kujifunza Kutokana na Makosa.

4. Kutafuta njia rahisi

Wahenga walisema rahisi ni gharama; pia wakesema rahisi inaumiza. Fahamu kuwa hakuna kitu kizuri kinachopatikana kwa urahisi. Jiulize ni kwa nini madini ya thamani hupatikana chini sana ardhini; baada ya swali hili utagundua kuwa kufikia mafanikio ni kupambana na changamoto.

Fanya kazi kwa bidii, tumia nguvu, juhudi na marifa yako yote ili uweze kufikia malengo yako ya maisha. Acha uvivu tesa mwili na akili yako kwa muda, kwani utaona matokeo mazuri.

5. Kujipiga mwenyewe

Kama hapendi kujipiga au kuumiza mwili wako wa damu na nyama kwanini unaruhusu kupiga au kuumiza akili na fikra zako?

Acha kuwaza mawazo yanayoumiza akili na fikra zako; yaliyopita yamepita, yasahau ujenge maisha mapya. Hakikisha huumizi fikra na akili zako kwani zinahitajika sana katika kufanikiwa kwako.

6. Kutokuwa na shukrani

Jifunze kusukuru na kuridhika kwa vitu na hali uliyonayo. Inawezekana kuna wengine wanatamani hata wawe na uwezo wa kuwa wazima kiafya lakini hawawezi. Ni wazi kuwa, ukiwa na shukurani pia utajifunza kuridhika.

Simaanishi uridhike na matatizo, la hasha, bali ujifunze kutambua unapopata mafanikio fulani; kwani hili litakuhamasisha kusonga mbele zaidi. Nimeshuhudia watu ambao wana mafaniko mengi tu lakini bado wanahangaika na kunung’unika kama vile hawana hitu. Hivyo badili mtazamo wako leo.

7. Ubinafsi na kushughulikia mahitaji yako tu

Inawezekana unawaza sana kuhusu maisha yako na mahitaji yako, tena unafikri kuvipata hivyo ndiko kufanikiwa. Hakia kufanikiwa halisi ni kuweza kuwasaidia na kuwafikia wengine. Pia kutumia mahitaji au matatizo ya wengine kama fursa ni njia bora zaidi ya kuhimiza mafanikio yako.

8. Kuvurugwa

Kuvurungwa? Ndiyo, kuvurugwa kunaweza kukutoa katika njia sahihi ya mafaniko yako. Unataka kuandika kitabu lakini… unataka kusoma lakini… unataka kuanzisha biashara lakini… unajikuta kuna mtu au kitu kinakuingilia.

Usiruhusu mtu au vitu kama vile mitandao ya kijamii kukutoa katika kufanya kile unachotaka kukifanya; jitenge navyo kisha fanyia kazi malengo yako.

Soma pia: Tabia 10 zitakazobadili maisha yako.

9. Kuishi bila malengo

Watu wengi hawana malengo wala hawafahamu maana na umuhimu wa malengo katika maisha yao. Malengo hukuwezesha kuona kituo au fikio fulani la baadaye katika maisha yako. Jiulize leo una malengo?

Je unafanya jitihada kuyafikia? Kama jibu ni hapana, hakika itakuwa ni vigumu sana kwa wewe kufanikiwa. Badili fikra zako sasa, jiwekee malengo na uyafuate

Soma pia: Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani.

10. Kukata tamaa

Ni kweli kuwa changamoto zipo kila siku kwenye maisha yetu, lakini hatutakiwi tuziruhusu zitukatishe tamaa. Inawezekana umekaribia kabisa kufika kwenye mafanikio lakini kutokana na upepo na mawimbi mengi katika njia yako unaamua kuacha na kurudi nyuma.

Nikutie moyo kuwa inuka fanya bidii bila kujali mawimbi na upepo nawe utayaona matunda ya jasho lako ndani ya muda mfupi.

Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

Mwisho

Nikutie moyo na kukuhamasisha kufanya bidii kadri uwezavyo ili kuyafikia mafanikio. Jitahidi kuziambia fikra zako kuwa unaweza, pia jifunze kwa wale waliofanikiwa. Kila jambo linawezekana chini ya jua, ni wewe tu kuchukua hatua sahihi na kwa wakati sahihi.

Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

Je una swali au maoni yoyote? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini, pia karibu uwashirikishe na wengine maarifa haya.

Washirikishe Wengine Makala Hii:

2
Tafadhali tuandikie maoni yako:

avatar
1 Comment threads
1 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
2 Comment authors
Kornel M.Omary materego Recent comment authors
newest oldest most voted
Omary materego
Guest
Omary materego

Natamani sana kupata kitabu chenu

Kornelio Maanga
Admin

Nashukuru sana kwa kutembelea blog yetu ya Fahamuhili; tunashukuru pia kwa maoni yako mazuri. Naahidi kufanyia kazi pendekezo lako.