
Mambo 10 ya Kuzingatia Unapochagua Anwani ya Mtandao (Domain)
Anwani mtandao ni muhimu sana kwa ajili ya utambulisho wa tovuti au blog ya kile unachokifanya. Inawezekana unamajina mengi ambayo unataka uyatumie kama anwani ya mtandao ya tovuti au blog yako; lakini ni muhimu kufahamu kuwa ukifanya makosa kwenye kuchagua anwani ya mtandao utaathirika kwa kiasi kikubwa. Madhara ya kukosea kuchagua anwani ya mtandao (domain) Kutokutambulisha vyema kile unachokifanya
Kukosa nafasi kwenye injini pekuzi
Kupoteza wasomaji au watembleaji
Kuingia kwenye migogoro ya kisheria ikiwa utatumia anzwani inayofanana na za wengine. Ikiwa unataka kufungua website au blog kwa ajili yako binafsi au bishara yako, basi fahamu mambo 10 ya kuzingatia unapochagua anwani ya mtandao (domain).
1. Upekee
Hakikisha unapochagua domain ni ya kipekee sana na i...