Ujasiriamali Archives - Fahamu Hili
Sunday, November 18Maarifa Bila Kikomo

Ujasiriamali

Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo

Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo

Ujasiriamali
Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujipatia kipato. Hivi leo kuna wajasiriamali wengi waliofanikiwa na wengine hawajafanikiwa. Kwa hakika wajasiriamali waliofanikiwa wanafahamu na wanaziishi sifa za wajasiriamali bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa mjasiriamali bora wakati una sifa za mwajiriwa. Ili kuwa mjasiriamali ni lazima kuzifahamu na kuziishi sifa za mjasiriamali. Karibu nikufahamishe sifa 10 za mjasiriamali. 1. Mwenye malengo Malengo ni mwongozo wa kukuwezesha kufanikisha jambo lolote. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Je umeamua kuwa mjasiriamali kwenye nini? Kwa ajili ya nini? Malengo yatakuongoza ufanye nini, wapi lini na kwa ajili ya nini. Bila malengo utafanya mambo bila mwongozo wowot...
Tofauti 10 Kati ya Mwajiriwa na Mjasiriamali

Tofauti 10 Kati ya Mwajiriwa na Mjasiriamali

Ujasiriamali
Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya mwajiriwa na mjasriamali; tofauti hii inahusisha tabia, fikra, maamuzi au hata matendo. Kuna baadhi ya watu ni wajasiriamali kwa mwonekano lakini kitabia ni waajiriwa; wapo pia wengine ni waajiriwa kimwonekano lakini ni wajasiriamali kitabia. Ikiwa basi unataka kuwa mjasiriamali, ni muhimu ufahamu tofauti 10 za msingi zilizopo kati ya mwajiriwa na mjasiriamali. 1. Mwajiriwa hupumzika kwenye likizo lakini mjasiriamali hutumia likizo kufanya kazi zaidi Kwa kawaida waajiriwa hufurahia muda wa likizo kwa sababu ndipo hupata muda wa kupumzika. Hali ni tofauti kwa mjasiriamali kwani hana likizo, na ikiwa ni mjasiriamali aliyeajiriwa, basi atatumia likizo yake kuendeleza mradi au biashara yake. 2. Mwajiriwa hulenga kupanda cheo lakini mjasiriamal...
Changamoto 12 za Ujasiriamali na Jinsi ya Kuzikabili

Changamoto 12 za Ujasiriamali na Jinsi ya Kuzikabili

Ujasiriamali
Kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake nyingi. Ni wazi kuwa wajasiriamali wakubwa na wadogo, wote hukutana na changamoto; tofauti yao ni chanzo cha changamoto hizo na njia wanazozitumia kuzikabili. Wajasiriamali wadogo ndiyo wamekuwa wakikabiliwa zaidi na changamoto hizo na hata kupelekea kupoteza biashara au miradi yao. Inawezekana wewe ni mmoja wapo wa wajasiriamali wanaokabiliana na changamoto. Karibu nikushirikishe changamoto 12 za ujasiriamali na jinsi ya kuzikabili. 1. Mtaji Kila biashara inahitaji mtaji ili iweze kujiendesha na kujipanua. Wajasiriamali wengi wanashindwa kuanzisha biashara au kupanua biashara zao kutokana na kukosa mtaji. Suluhisho: Kumbuka! Siyo lazima upate mtaji wote unaouhitaji, unaweza kuanza na mtaji kidogo sana n...
Kanuni 15 za Ujasiriamali Ambazo ni Lazima Uzifahamu

Kanuni 15 za Ujasiriamali Ambazo ni Lazima Uzifahamu

Ujasiriamali
Ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa ajira umekuwa wa shida sana, watu wengi hujikuta wakiwa na chaguo la kuwa wajasiriamali pekee kwenye maisha yao. Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo. Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali. 1. Kuwa mtatuzi wa matatizo Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajiki...
Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Ujasiriamali
Kuanza biashara kutoka kiwango cha sifuri siyo kazi rahisi. Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua. Unapokuwa kwenye biashara ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako; ili ujitahidi kuyaepuka ama kuyapunguza kadri iwezekanavyo. Ni dhahiri kuwa wajasiriamali wengi wamekwama kutokana na kupuuzia au kutofahamu makosa haya 15 ambayo hata wewe unatakiwa kuyafahamu na kuyaepuka. 1.Kujifanya unafahamu kila kitu Usijifanye unajua kila kitu, hasa kama ndiyo umeingia kwenye ulimwengu wa kibiashara. Kwanini? Kwa sababu kuendesha biashara ni kujifunza na kupata uzoefu. Jitahidi ku...
Mambo 5 Yanayosababisha Biashara za Wanawake Kufa

Mambo 5 Yanayosababisha Biashara za Wanawake Kufa

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Hivi leo wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahi na kufanyia kazi fursa mbalimbali. Fursa hizo ni pamoja na uwekezaji katika biashara ndogo na za kati. Ni dhahiri kuwa mama ndiye nayeumia zaidi pale familia inapokuwa na uchumi mbaya. Mama hapendi kuona watoto wanakosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu, matibabu n.k. Hivyo suala la kuboresha kipato cha familia limewafanya wanawake wengi kutafuta njia mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo njia ya kufanya biashara. Hata hivyo pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na wanawake, bado biashara zao ngingi hufa kutokana na sababu kadha wa kadha. Fuatana nami katika makala hii ufahamu mambo matano yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa. 1. Kukosa maarifa na elimu ya biashara Kitu chochote au kazi y...
Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Uteuzi wa jina la biashara ni hatua muhimu kama ilivyo kwa jiwe la pembeni katika nyumba. Watu wengi wamekuwa hawatilii maanani mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua jina la biashara au kampuni. Nimekuwa nikishuhudia makapuni mengi yakitumia majina ya ajabu ajabu yasiyoendana na biashara zao. Kwa sehemu kubwa kufanikiwa na kujulikana kwa biashara yako kunategemea jina la biashara yako. Fuatana nami katika makala hii ambayo nitakueleza mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua jina la biashara. 1. Uhusiano wa jina na bidhaa au huduma Je unafahamu kwamba jina la biashara linatakiwa liakisi huduma au biashara unayoifanya? Ni jambo jema kutumia jina linaloakisi kile unachokifanya. Kwa mfano jina kama vile “Samelctro” lifaa kwa kampuni ya vifaa vya kielektroniki, “Pamba L
Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Inawezekana una wazo zuri sana la biashara na unatamani kulitekeleza haraka kadri iwezekananavyo. Pengine umeajiriwa katika taasisi au ofisi fulani na unashauku kubwa ya kuacha kazi ili uweze kuanzisha kampuni au biashara yako. Kabla hujafanya maamuzi yoyote ni vyema ukae chini na utafakari mambo kadhaa ambayo yatakuwa na manufaa makubwa kwako. Katika makala hii nitakueleza mambo 7 muhimu ambayo utahitajika kuyafanya kabla ya kuanza biashara yako. 1. Chagua wazo la biashara vyema Katika eneo ambalo watu wengi hukosea wakati wanapoanzisha kampuni au biashara ni uchaguzi wa wazo la kibiashara. Unapochagua wazo baya au usilolimudu, ni wazi kuwa hutoweza kulitekeleza na kupata faida. Hakikisha wazo unalolichagua unalimudu vyema pia linatekelezeka. Epuka kuchagua wazo pana sana au...
Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo

Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Watu wengi wamekuwa wakitamani kuanza biashara lakini wanafikiri namna ya kuanza kwani mtaji wao ni mdogo sana. Usiogope; kuwa na mtaji mdogo au kutokuwa nao kabisa sio mwisho wako wa kutimiza malengo yako. Zipo mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukuwezesha kufanya biashara hata kama utakuwa na mtaji mdogo. Tafadhali fuatilia hoja jadiliwa hapo chini kwa ufafanuzi zaidi. 1. Kuwa mbunifu Moja kati ya mambo ambayo yatakusaidia sana kwenye kuanza biashara kwa mtaji mdogo ni ubunifu. Kwa njia ya ubunifu utaweza kushinda biashara na bidhaa zilizoko sokoni kwa urahisi zaidi. Unaweza kufanya haya yafuatayo: Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema. Hili litakusaidia kukabili changamoto vyema. Angalia tatizo au uhitaji uliopo sasa na uutatue kwa bidhaa au hudum...