Ujasiriamali Archives - Page 2 of 2 - Fahamu Hili
Thursday, April 25Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Ujasiriamali

Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Ujasiriamali
Kuanza biashara kutoka kiwango cha sifuri siyo kazi rahisi. Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua. Unapokuwa kwenye biashara ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako; ili ujitahidi kuyaepuka ama kuyapunguza kadri iwezekanavyo. Ni dhahiri kuwa wajasiriamali wengi wamekwama kutokana na kupuuzia au kutofahamu makosa haya 15 ambayo hata wewe unatakiwa kuyafahamu na kuyaepuka. 1.Kujifanya unafahamu kila kitu Usijifanye unajua kila kitu, hasa kama ndiyo umeingia kwenye ulimwengu wa kibiashara. Kwanini? Kwa sababu kuendesha biashara ni kujifunza na kupata uzoefu. Jitahidi ku...
Mambo 5 Yanayosababisha Biashara za Wanawake Kufa

Mambo 5 Yanayosababisha Biashara za Wanawake Kufa

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Hivi leo wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahi na kufanyia kazi fursa mbalimbali. Fursa hizo ni pamoja na uwekezaji katika biashara ndogo na za kati. Ni dhahiri kuwa mama ndiye nayeumia zaidi pale familia inapokuwa na uchumi mbaya. Mama hapendi kuona watoto wanakosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu, matibabu n.k. Hivyo suala la kuboresha kipato cha familia limewafanya wanawake wengi kutafuta njia mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo njia ya kufanya biashara. Hata hivyo pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na wanawake, bado biashara zao ngingi hufa kutokana na sababu kadha wa kadha. Fuatana nami katika makala hii ufahamu mambo matano yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa. 1. Kukosa maarifa na elimu ya biashara Kitu chochote au kazi y...
Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Jina la Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Uteuzi wa jina la biashara ni hatua muhimu kama ilivyo kwa jiwe la pembeni katika nyumba. Watu wengi wamekuwa hawatilii maanani mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua jina la biashara au kampuni. Nimekuwa nikishuhudia makapuni mengi yakitumia majina ya ajabu ajabu yasiyoendana na biashara zao. Kwa sehemu kubwa kufanikiwa na kujulikana kwa biashara yako kunategemea jina la biashara yako. Fuatana nami katika makala hii ambayo nitakueleza mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua jina la biashara. 1. Uhusiano wa jina na bidhaa au huduma Je unafahamu kwamba jina la biashara linatakiwa liakisi huduma au biashara unayoifanya? Ni jambo jema kutumia jina linaloakisi kile unachokifanya. Kwa mfano jina kama vile “Samelctro” lifaa kwa kampuni ya vifaa vya kielektroniki, “Pamba L...
Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Inawezekana una wazo zuri sana la biashara na unatamani kulitekeleza haraka kadri iwezekananavyo. Pengine umeajiriwa katika taasisi au ofisi fulani na unashauku kubwa ya kuacha kazi ili uweze kuanzisha kampuni au biashara yako. Kabla hujafanya maamuzi yoyote ni vyema ukae chini na utafakari mambo kadhaa ambayo yatakuwa na manufaa makubwa kwako. Katika makala hii nitakueleza mambo 7 muhimu ambayo utahitajika kuyafanya kabla ya kuanza biashara yako. 1. Chagua wazo la biashara vyema Katika eneo ambalo watu wengi hukosea wakati wanapoanzisha kampuni au biashara ni uchaguzi wa wazo la kibiashara. Unapochagua wazo baya au usilolimudu, ni wazi kuwa hutoweza kulitekeleza na kupata faida. Hakikisha wazo unalolichagua unalimudu vyema pia linatekelezeka. Epuka kuchagua wazo pana sana au...
Mbinu 10 za Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo

Mbinu 10 za Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Watu wengi wamekuwa wakitamani kuanza biashara lakini wanafikiri namna ya kuanza kwani mtaji wao ni mdogo sana. Ni ukweli usiopingika kuwa idadi kubwa ya watu walioshindwa kuanzisha biashara wakishindwa katika eno hili la kuanza biashara na mtaji mdogo. Usiogope; kuwa na mtaji mdogo au kutokuwa nao kabisa sio mwisho wako wa kutimiza malengo yako. Zipo mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukuwezesha kufanya biashara hata kama utakuwa na mtaji mdogo. Tafadhali fuatilia hoja jadiliwa hapo chini kwa ufafanuzi zaidi. 1. Kuwa mbunifu Moja kati ya mambo ambayo yatakusaidia sana kwenye kuanza biashara kwa mtaji mdogo ni ubunifu. Kwa njia ya ubunifu utaweza kushinda biashara na bidhaa zilizoko sokoni kwa urahisi zaidi. Unaweza kufanya haya yafuatayo: Chagua wazo la biashara unalolipenda na ku...