
Athari 8 Kiafya za Dawa za Kuulia Wadudu — Viwatilifu
Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu. Takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO zinabainisha kuwa kuna zaidi ya vifo 220,000 vitokanavyo na athari za sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu—viwatilifu. Ikiwa unataka kuweka afya yako salama, basi karibu nikushirikishe athari 8 kiafya za dawa za kuulia wadudu — viwatilifu.
1. Husababisha saratani
Watafiti mbalimbali wa maradhi ya saratani wanaeleza kuwa dawa za kuulia wadudu zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha seli za saratani mara zinapoingia kwenye mwili wa binadamu. Hatari hii hutokea zaidi pale amb...