
Hatimaye Ghana Yarusha Satelaiti Yake ya Kwanza Kwenda Anga za Juu
Satelaiti ijulikanayo kama GhanaSat-1, ambayo iliundwa na wanafunzi kutoka katika Chuo Kikuu cha All Nations cha Koforidua, ilirushwa kwenda kwenye mzingo wa dunia kutoka kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu. Shange na vifijo vya watu takriban 400 wakiwemo wanafunzi na waandisi walikokuwa wakishuhudia tukio hili zilisikika katika mji wa kusini mwa Ghana. Mji huo ndipo lilipofanyika zoezi hilo la urushaji wa satelaiti hiyo. Mawasiliano na chombo hicho yalianza kupokelewa muda mfupi baada ya chombo hicho kurushwa. Maradi huo uligharimu dola za kimarekani 50,000 ulifadhiliwa na shirika la Japan Aerospace Exploration Agency (JAXA). Satelaiti hiyo itatumika katika mambo mabalimbali kama vile kufwatilia ukanda wa pwani wa Ghana, kuchora ramani na kuijengea nchi hiyo uwezo kati...