
Fahamu Tabia 10 za Watu Wenye Wivu Ili Uwaepuke
Mara mtu apatapo mafanikio mambo mengi hutokea au hubadilika. Moja kati ya mambo ambayo hutokea ni mabadiliko kwa watu wanao mzunguka mtu huyo. Wengine humpenda, wengine humheshimu, wengine humchukia au hata kumwonea wivu. Wivu umekuwa ukitesa na kurudisha maendeleo ya watu nyuma hasa wale ambao ndio huwa na wivu huo mioyoni mwao. Kwa kuwa wivu hauwaathiri wale walio nao pekee, ni vyema nawe ukafahamu tabia za watu wenye wivu ili uwaepuke wasije wakakuathiri kwa kukurudisha nyuma katika hatua zako za maendeleo.
1. Hawastaajabishwi na mafanikio ya wengine
Moja kati ya tabia kubwa ya watu wenye wivu ni kutostaajabishwa na mafanikio ya wengine. Wao hata wasikie jambo zuri au kubwa kiasi gani la mtu mwingine wao hujifanya kuliona kama la kawaida tu. Unaweza kusikia hata wakisem...