Andika Makala Kwenye Fahamuhili.com - Fahamu Hili
Friday, September 29Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Andika Makala Kwenye Fahamuhili.com

Andika

Je unahitaji makala yako ionekane kwenye tovuti hii? Fahamuhili.com tunawakaribisha watu ambao wanapenda kushirikisha ulimwengu mawazo na maarifa yao.

Ikiwa unapenda kuandika makala kwenye tovuti yetu, unakaribishwa sana kufanya hivyo bila kizuizi.

Faida za Kuandika Makala Kwenye Tovuti Yetu:

  • Kuboresha maisha ya watu wengine kutokana na mawazo au maarifa yako.
  • Utaweza kufikisha mawazo au maarifa yako kwenye ulimwengu.
  • Utaongeza kiwango chako cha ushawishi na kufahamika.
  • Utaongeza watembeleaji kwenye tovuti yako. (tutaweka maelezo yako mafupi (bio), picha pamoja na tovuti yako kama unayo mwisho wa kila makala yako)
  • Utaongeza uwezo wako wa uandishi.

Mada Unazoweza Kuandikia:

  • Ujasiriamali.
  • Biashara na Uchumi.
  • Maendeleo Binafsi.
  • Tija (Productivity).
  • Kipato au Uongezaji wa Kipato.
  • Familia na Mahusiano.
  • Teknolojia.
  • Hamasa (Motivation).
  • Afya.
  • Mtindo wa Maisha.
  • Maarifa (New Things and Facts).
  • Tovuti na Blog.
  • Fursa.
  • Nyumba na Makazi.

Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi Wako:

  • Makala isiwe imechapishwa mahali pengine popote hata kama ni kwenye blog yako.
  • Chagua kichwa kizuri cha makala ambacho kinavutia na kueleweka vyema. Tunapendelea zaidi makala zenye kufundisha, kujibu swali au kutatua tatizo la mtu fulani.
  • Uandishi rafiki unaosomeka kwa urahisi bila kuchosha. (Tumia sentensi fupifupi, aya fupifupi pamoja na utumizi wa namba na mishale-bullets ikibidi kufanya hivyo).
  • Matumizi sahihi ya lugha pamoja na uhariri mzuri wa makala yako.
  • Makala iwe angalau na urefu wa maneno kuanzia 600.
  • Ikiwa makala inahitaji picha au video maalumu; basi weka viunganishi vya kufikia picha hizo. Ikiwa makala haihitaji picha maalumu au unazozipendelea, Fahamuhili tutaweka picha moja kuu sisi wenyewe.
  • Hatupokei makala zenye lengo la kujitangaza au makala zilizowekwa viunganishi venye lengo la kupeleka watembeleaji kwenye tovuti fulani.
  • Hatupokei makala za chuki, ubaguzi, siasa, udaku, biashara haramu au makala zinazokiuka sheria na maadili.
  • Tutafurahi ikiwa utaweka viunganishi vinavyolenga makala nyingine kwenye tovuti hii.
  • Tunapendelea zaidi pia makala ambazo zinalenga wazungumzaji wote wa lugha ya Kiswahili badala ya watu kutoka eneo au nchi fulani pekee.

Makala za mfano:

Jinsi ya Kutuma Makala:

Tafadhali tuma makala yako kwetu kupitia barua pepe ya fahamuhili@gmail.com. Hakikisha unaambatanisha kila kitu kuhusu makala moja kwenye barua pepe moja.

Tafadhali pia tuma picha na maelezo mafupi kukuhusu wewe (bio). Unaweza kutazama mfano kwenye makala za mfano hapo juu. Ikiwa una tovuti au blog, pamoja na akaunti za mitandao ya kijamii, tafadhali ambatanisha viunganishi vyake pia.

Kukubaliwa na Kuchapishwa:

Fahamuhili itaipitia na kuitathimini makala yako ili kuona kama imekidhi vigezo vyetu. Ikiwa imekidhi vigezo tutakufahamisha kuwa imekubaliwa pamoja na tarehe itakapochapishwa.

Tutatangaza na kuisambaza makala yako katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii pamoja na kuwajulisha wasomaji wetu kupitia barua pepe.

Nawe pia unaweza kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii mara itakapochapishwa ili makala yako kupitia Fahamuhili ifahamike zaidi. Kwa maswali na ushauri tafadhali wasiliana nasi

Fahamuhili tunakupenda na tunathamini mchango wako. Karibu Fahamuhili; Maarifa bila kikomo!