Sera ya Faraga - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Sera ya Faraga

Tamko hili kuhusu faragha linatumika kwa tovuti ya Fahamuhili na vyombo vingine vyovyote vya kisheria vinavyodhiibiti, kuhakiki au kutumia taarifa zitakazochukuliwa kupitia tovuti hii bila ya kutoa taarifa yoyote ya binafsi. Hata hivyo mtumiaji, anakubali kutumia taarifa hiyo  kwa mujibu wa tamko hili la sera.

Tafadhali zingatia kuwa Tovuti hii ina viungo (links) vya tovuti nyingine, visivyotawaliwa na tamko hili la faragha.

Iwapo una swali au kero yoyote kuhusu tamko hili la faragha, tumia kiungo cha “Wasiliana Nasi” au tuma barua pepe kwenda fahamuhili[at]gmail.com. Tovuti hii haitachukua taarifa zako binafsi unapotembelea tovuti yetu, isipokuwa utakapoamua kutupatia taarifa hizo.

Taarifa Inayochukuliwa

Unapotembelea tovuti ya Fahamuhili, tunaweza kuhifadhi baadhi ya taarifa zikiwemo anwani ya intaneti unakopitia, tarehe, muda, anwani ya Intaneti ya tovuti ulikounganishwa kwenye tovuti ya Fahamuhili, jina na kurasa ulizovinjari. Taarifa inayochukuliwa inatumika kubainisha idadi ya watu waliotumia sehemu mbalimbali za tovuti yetu ili kuboresha hudama zetu. Aidha, tunatumia taarifa hizi kufanya tathimini ya wasomaji na kuifanya tovuti kuwa na manufaa zaidi.

Taarifa Binafsi

Unaweza kutoa taarifa zako binafsi kama vile barua pepe, simu, au jina ili kuweza kupata mrejesho (updates) na taarifa mbalimbali. Taarifa inayojazwa kwenye fomu ya maoni itatumika tu kujibu ujumbe wako au kusaidia kupata taarifa uliyoomba.

Tunatumia mbinu na teknolojia mbalimbali ili kuhakikisha kuwa taarifa na mawasiliano yako katika tovuti yetu viko salama.

Taarifa unayotupatia haitapatiwa kampuni, mtu au taasisi nyingine kwa namna yoyote ile isipokuwa imehitajika kwa mujibu wa sheria.