
Mbinu 7 za Kukurahisishia Kusoma Vitabu Unapokuwa na Shughuli Nyingi
Kama nilivyoeleza kwenye makala mbalimbali kuwa kusoma vitabu kuna manufaa mengi sana ambayo kila mtu mwenye maono anapaswa kuyapata. Vitabu hubeba maarifa kemkem ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kukusaidia kubadili maisha yako. Soma pia: Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu Hata hivyo bado watu wengi wanashindwa kusoma vitabu jinsi ipasavyo. Ikiwa unapenda kusoma vitabu lakini una shughuli nyingi, basi karibu nikushirikishe mbinu kadhaa zitakazo kuwezesha kusoma vitabu kwa urahisi.
1. Tumia simu yako
Karibu kila mtu leo ana simu ya kisasa ya mkononi (smartphone), hata hivyo bado watu wengi hawafahamu nguvu au matumizi adhimu yanayopatikana kwenye simu hizo. Ni ukweli usiopingika kuwa ulimwengu wa kutumia simu kama kifaa cha kupiga na kupokea simu pamoj...