Tija Archives - Page 2 of 3 - Fahamu Hili
Saturday, July 11Maarifa Bila Kikomo

Tija

Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta

Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta

Tija
Kuandika kwa kasi na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta kuna manufaa mengi kama vile kuweza kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi, kuweza kuandika mambo mbalimbali kwa kutumia kompyuta na hata sifa ya kukuwezesha kupata kazi mbalimbali. Hivyo, najua unatamani kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta; lakini tatizo bado hujaweza kuacha kasi ya kudonoa na kuweza kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi. Karibu ufahamu njia 5 ambazo unaweza kuzitumia ili kuboresha uwezo wako wa kuandika kwa kutumia kompyuta. 1. Elewa na tumia baobonye (keyboard) vyema Ili uweze kuongeza kasi yako ya kuandika pamoja na usahihi ni lazima uelewe baobonye vyema na kuitumia vyema. Zingatia haya yafuatayo: Elewa mpangilio wa vitufe kwenye baobonye. Panga vidole kulingana na vitufe sta...
Mambo 10 Usiyojua Kama Unaweza Kuyafanya kwa Kutumia Google

Mambo 10 Usiyojua Kama Unaweza Kuyafanya kwa Kutumia Google

Tija
Google ni rafiki wa karibu katika maisha yetu. Kupitia injini pekuzi ya Google tunaweza kupata majibu ya maswali mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kuwa katika matumizi yetu ya teknolojia hatuwezi kuepuka kutumia Google. Kupitia Google unaweza kupata majibu ya maswali mbalimbali, kazi, marafiki, bidhaa, huduma, elimu n.k. Pamoja na nafasi hii kubwa ya Google kwenye maisha na kazi zetu, bado watu wengi hawafahamu vyema matumizi mbalimbali ya Google. Karibu nikufahamishe mambo 10 usiyojua kama unaweza kuyafanya kwa kutumia Google. 1. Kikokotozi (calculator) Ikiwa unataka kufanya mahesabu kadhaa, huhitaji kikokotozi au simu yenye kikokotozi kama uko karibu na Google.  Kwa kuandika neno calculator kwenye ukurasa wa Google mara moja utapata kikokotozi kwa ajili ya kufanyia hesabu.
Faida 5 za Kusema “Hapana”

Faida 5 za Kusema “Hapana”

Tija
Ni muhimu kukumbuka kuwa “Hapana” ni jibu rahisi pia dogo sana lakini lina nguvu kubwa. Ni vyema kufahamu nguvu iliyoko kwenye jibu la “Hapana” ili tuweze kuboresha maisha yetu. Kila siku kwenye maisha yetu tunatakiwa kufanya maamuzi fulani ya kukataa au kukubaliana na mipango au jambo fulani. Ni wazi kuwa maamuzi tunayoyafanya kuhusu mambo na mipango hii, ndiyo huamua na kuatawala hali za maisha yetu ya sasa na baadaye. Karibu nikushirikishe faida 5 za kusema hapana katika mipango na mambo mbalimbali kwenye maisha yako. 1. Hukutenga na mipango mibaya Siyo kila mpango unafaa kwenye maisha yako. Mipango mingine inaweza kuangamiza ndoto na malengo yako. Kwa mfano mtu akakushawishi uingie kwenye biashara ya dawa za kulevya, je unafikiri utaweza kweli kupata manufaa ya uh
Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi

Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi

Tija
Kuamka mapema asubuhi kuna manufaa mengi sana. Unapoamka mapema asubuhi unaongeza ufanisi na tija katika utendaji wako wa kazi. Kumbuka pia muda wa asubuhi ndipo mtu anapokuwa na afya njema kiakili na kimwili; hivyo kuamka mapema kutakuwezesha kuutumia muda huu vyema. Pamoja na umuhimu huu wa kuamka mapema, siyo watu wengi wanaoweza kutimiza lengo lao la kuamka mapema. Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha tatizo hili kama vile matatizo ya kiafya, kisaikolojia na hata kimazingira. Ikiwa basi wewe ni mmoja wapo wa watu wanaotamani kuamka mapema, basi fahamu njia 10 za kukuwezesha kuamka mapema asububi. 1. Lala muda sahihi Muda wa kulala ni muhimu sana katika kukuwezesha kuamka mapema asubuhi. Hakikisha unalala mapema na unapata muda wa kutosha wa kulala. Kwa kawaida bina...
Mbinu 7 za Uandishi Bora wa Vitabu

Mbinu 7 za Uandishi Bora wa Vitabu

Tija
Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu 7 zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chag...
Mbinu 10 za Uhakika  za Kufahamu Kiingereza/English kwa Muda Mfupi

Mbinu 10 za Uhakika za Kufahamu Kiingereza/English kwa Muda Mfupi

Tija
Kujifunza lugha mpya kunaweza kuwa ni kugumu, lakini inawezekana. Je unatamani kufahamu na kumudu lugha ya Kiingereza kwa muda mfupi? Kumudu Kiingereza inawezekana lakini kuna mambo kadhaa unatakiwa kuyafahamu na kuyafanya kwa uhakika. Ikiwa unapenda kuwa wa kimataifa, basi fuatilia mbinu 10 za uhakika zitakazo kuwezesha kufahamu Kiingereza/English kwa muda mfupi. 1. Penda na furahia Kiingereza Ili uweze kufanya au kujifunza kitu chochote ni lazima kwanza ukipende. Ikiwa unataka kufahamu Kiingereza kwa muda mfupi ni lazima ukipende kwani ndipo utaweza kujifunza kila mara bila kuchoka wala kukata tamaa. Kila mara jihamasishe kwa kutafakari manufaa utakayoyapata baada ya kufahamu Kiingereza vizuri. 2. Jifunze Kiingereza kila siku Huwezi kufahamu Kiingereza kama hutojifunza kila si...
Fahamu Njia 6 za Kulinda Akaunti Zako za Mitandao ya Kijamii

Fahamu Njia 6 za Kulinda Akaunti Zako za Mitandao ya Kijamii

Teknolojia, Tija
Mitandao ya kijamii ni kitu muhimu sana kwenye maisha binafsi na shughuli za kiuchumi kama vile biashara. Kutokana na umuhimu huu, kuna haja ya kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa salama. Je ulishawahi kufikiri nini kitatokea ikiwa mtu mbaya atapata nafasi ya kuingia kwenye akaunti zako? Ni wazi kuwa mambo kama haya hapa chini yanaweza kutokea: Kuiba wafuasi wako utakaokuwa umewakusanya muda mrefu. Kutapeli watu mbalimbali wanaokufahamu katika mitandao ya kijamii kwa kutumia akaunti yako. Kuchafua taswira yako; kumbuka mtu mbaya anaweza kuweka maudhui mabaya yatakayoshusha hadhi yako. Kuiba ama kutumia vibaya taarifa zako binafsi zilizoko kwenye akaunti yako. Ni wazi kuwa ipo sababu ya kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa sal...
Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema

Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema

Tija
Unaweza ukawa unajiuliza tovuti hizo ni zipi? Intaneti imejaa tovuti nyingi sana, za maana na zisizo za maana. Hata hivyo bado tovuti za maana na zenye manufaa zimeweza kujibainisha wazi kati ya zile zisizofaa. Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe tovuti 20 ambazo kwa namna moja au nyingine zitakufaa katika maisha yako ya kila siku. 1. Have I Been Pwned? Tovuti: https://haveibeenpwned.com/ Hii ni tovuti nzuri sana kwa ajili ya kukagua kama barua pepe yako imeshavuja kwenye taarifa za siri zilizoibiwa. Hivi leo kuna makampuni na tovuti nyingi zinazodukuliwa na kuibiwa taarifa za watumiaji wake. Hivyo unaweza kuwa ni moja kati ya watu ambao barua pepe zao ziliibiwa. Ikiwa utaambiwa kua barua pepe yako imeonekana kwenye taarifa zilizodukuliwa basi badili neno la siri hara...
Njia 8 za Kutambua Bidhaa Feki au Bandia

Njia 8 za Kutambua Bidhaa Feki au Bandia

Tija
Mara nyingi tunanunua vitu na bidhaa mbalimbali bila kuzifahamu au kuzichunguza vyema. Hili limepelekea watu wengi kununua bidhaa zisizofaa kwao au zenye madhara kwenye afya zao. Kutokana na ukosefu wa elimu pamoja na kuishi kwa mazoea, watu wengi hawajui wala hawachunguzi vyema bidhaa wanazozinunua ili kuhakikisha ubora wake. Madhara ya kutumia bidhaa feki au bandia: Matatizo ya kiafya kama vile saratani na ulemavu. Upotevu wa fedha. Ajali (Milipuko, shoti ya umeme, n.k). Huathiri uchumi. Ni wazi kuwa yapo madhara mengi yatokanayo na matumizi ya bidhaa feki. Hivyo ni vyema ukafahamu njia za kubaini bidhaa hizi. 1. Ofa na matangazo yasiyo ya kawaida Wahenga walisema “Chema chajiuza kibaya chajitembeza”; ni vyema ukawa makini na bidhaa zenye punguzo kubwa la bei ku
Vitu 15 Vinavyofanywa na Watu Werevu (Smart)

Vitu 15 Vinavyofanywa na Watu Werevu (Smart)

Tija
Unaweza kujiuliza ni mambo gani yanayomfanya mtu kuwa mwerevu (smart). Je ni wingi wa maarifa anayoyafahamu? Au je ni kiwango cha wastani au cha juu cha kufikiri kwake? Ukweli ni kuwa ni werevu ni uwezo wa kufanya maamuzi yatakayofaa wakati wote; au ni kuweza kuibua kitu kizuri katika kitu kibaya au wakati mbaya. Watu werevu huweza kufanya maamuzi ambayo yanazingatia matokeo ya mbeleni ya maamuzi hayo. Ni dhahiri kuwa watu werevu (smart) ni tofauti na watu wengine kutokana na yale wanayoyafanya au kutofanya. Fahamu mambo 10 ambayo watu werevu hawayafanyi. 1. Hawapuuzi uwekaji akiba Katika maisha ya kiuchumi kuna vipindi viwili; kipindi cha mavuno(shibe) na kipindi cha ukame(njaa). Ni watu wachache sana ndio wanaoweza kuishi katika vipindi hivi viwili bila shida. Watu werevu hawapu...