Faida 5 za Kusema "Hapana" - Fahamu Hili
Tuesday, October 3Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 5 za Kusema “Hapana”

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Hapana

Ni muhimu kukumbuka kuwa “Hapana” ni jibu rahisi pia dogo sana lakini lina nguvu kubwa. Ni vyema kufahamu nguvu iliyoko kwenye jibu la “Hapana” ili tuweze kuboresha maisha yetu.

“’Hapana’ ni sentensi kamili. Haihitaji maelezo ya ziada. Kwa hakika unaweza kujibu ombi la mtu kwa jibu rahisi la ‘Hapana’.”

Sharon E. Rainey

Kila siku kwenye maisha yetu tunatakiwa kufanya maamuzi fulani ya kukataa au kukubaliana na mipango au jambo fulani.

Ni wazi kuwa maamuzi tunayoyafanya kuhusu mambo na mipango hii, ndiyo huamua na kuatawala hali za maisha yetu ya sasa na baadaye.

Karibu nikushirikishe faida 5 za kusema hapana katika mipango na mambo mbalimbali kwenye maisha yako.

1. Hukutenga na mipango mibaya

Siyo kila mpango unafaa kwenye maisha yako. Mipango mingine inaweza kuangamiza ndoto na malengo yako.

Kwa mfano mtu akakushawishi uingie kwenye biashara ya dawa za kulevya, je unafikiri utaweza kweli kupata manufaa ya uhakika? Unaweza kukamatwa na maisha yako yakaishia gerezani.

Huu ni mfano wa mipango mibaya ambayo watu wanapaswa kutokusita kusema hapa; kumbuka hakuna mkato kwenye mafanikio.

“Jifunze kusema ‘hapana’ kwa mazuri ili uweze kusema ‘ndiyo’ kwa bora.”

John C. Maxwell

Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

2. Hukufanya kuonekana mtu mwenye msimamo

Tutatambua vipi msimamo wako ikiwa wewe unakubali kila kitu? Ni muhimu kusema hapana ili watu watambue kuwa una masimamo fulani ambao hauwezi kuuacha.

Ikiwa kuna jambo au kitu ambacho hukipendi, basi tumia buasara kusema hapa ili watu waheshimu msimamo wako.

Kwa mfano ikiwa wewe hutumii pombe au sigara, basi sema wazi hapa kwa vitu hivi hata kama hutamfurahisha unayempa jibu hilo.

3. Hufanya mawazo yako yaheshimike

Watu wataheshimu mawazo yako kama unayabainisha na kuyatetea wazi. Kusema hapana ni njia ya kuonyesha aina ya mawazo uliyonayo.

Tumia hekima na busara kupinga mawazo yale ambayo wewe huyataki; moja kwa moja wale unaowaeleza wataweza kutambua wazi mawazo yako na kuyaheshimu.

4. Hukuokolea fedha na muda

“Kama kweli unataka kuwa mtumiaji mzuri wa muda, unatakiwa kujifunza kusema hapana kwa watu wengine na kufanya hivyo mara kwa mara.”

Sunday Adelaja

Unaposema hapana utaepuka mambo na tabia mbalimbali ambazo zinaweza kukupotezea muda na pesa nyingi.

Ni muhimu kusema hapana kwa maswala kama vile pombe, uzinzi, matumizi mabaya mitandao ya kijamii, uzururaji, n.k.

Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

5. Hukuwezesha kufikia ndoto na maono yako

Ili tuweze kufikia ndoto zetu tunahitaji kuepuka mambo mbalimbali yasiyoendana na ndoto au maono yetu.

Ka njia ya kusema hapana unaweza kuondoa mambo yote ambayo kwa namna moja au nyingine hayakuwezeshi kutimiza ndoto au maono yako.

Inaweza kuwa ni mtu, kazi, tabia n.k. ambavyo haviendani na ndoto zako; hivo ni muhimu kusema hapana.

Soma pia: Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani.

Neno la Mwisho:

Naamini umeona jinsi jibu dogo la “Hapana” lilivyo na nguvu kubwa katika maisha yako.

Ni muhimu kufahamu kuwa mtu mwenye malengo ni lazima aweze kusema hapana kwa vitu, watu, tabia au kazi ambazo hazimuwezeshi kutimiza malengo yake. Je wewe huwa unasema hapana?

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini. Usisahau pia kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

2.3 3 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

6 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ramadhan Kasherente
Ramadhan Kasherente
3 years ago

Nimeipenda hii blog kwakweli muandishi mungu amjaalie

Amani
Amani
3 years ago

Nahitaji kujiunga

Andrew william
Andrew william
5 months ago

Kabisa ni vyema tukazifahamu njia zinazoweza kutusaidia kutunza pesa vizuri

6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x