Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Kufanikiwa

Ikiwa wewe ni mjasiriamali unayeanza au umeajiriwa sehemu fulani, kuna tabia ambazo unatakiwa kuzifahamu na kuzifanya ili uwe na mafanikio.

“Mafanikio sio zaidi ya tabia chache  rahisi zinazotekelezwa kila siku.”

Jim Rohn

Watu wengi hufikiri kuwa mafanikio ni jambo linalotokea kwa bahati tu; lakini mafanikio ni matokeo ya tabia au mikakati inayofanywa mara kwa mara.

Hivi leo kuna watu tunaowachukulia kuwa wamefanikiwa; watu hawa wana tabia fulani za msingi zinazofanana. Karibu nikufahamishe tabia 10 za watu waliofanikiwa ambazo unaweza kujifunza ili uweze kufanikiwa.

1. Wana mipango

“Tumia muda wako kutafakari ni fursa ipi uifanyie kazi na anza kuifanyia kazi kama mbwa mwitu waliopatwa na kichaa”

Neal Goldman

Watu waliofanikiwa hawafanyi kazi bila mipango madhubuti. Watu hawa hupanga mipango mbalimbali wanayotakiwa kuitekeleza; mwishoni hukagua kama mipango yao wameitekeleza jinsi ipasavyo.

Ni muhimu kujifunza tabia hii ya kujiwekea mipango na kufanya mambo kulingana na mipango husika bila kusahau kufanya tathimini mwishoni.

2. Hawaahirishi bali wanafanya

Watu waliofanikiwa hawana tabia ya kuahirisha mambo, bali huyafanya kadri wapatapo muda. Mara nyingi watu wa kawaida hujidanganya kuwa kuna muda, kesho ipo, nitafanya baadaye n.k.

Ikiwa tunataka kufanikiwa, ni lazima tufanye mambo bila visingizio wala kuahirisha.

“Tunaweza kutazama likitokea, au tukawa sehemu yake”

Elon Musk

3. Wanafanya kazi kwa bidii

Ni rahisi kufikiri kuwa watu waliofanikiwa wanalala au kukaa tu na pesa zinawajia. Watu waliofanikiwa wanajua nini maana ya kufanya kazi kwa bidii kweli.

Hakuna kitu kizuri kinachokuja kwa urahisi. Ni lazima kufanya bidii na kuwa na nidhamu ya kazi ndipo tunaweza kuona matokeo mazuri.

“Kila siku naamini ukiweka juhudi kwenye kazi matokeo yatatokea.”

Michael Jordan

4. Wanafanya wanachokipenda

“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.”

Marsha Sinetar

Je unapenda unachokifanya? Siri moja wapo ya kufanikiwa katika jambo lolote ni kufanya kile unachokipenda.

Watu wengi waliofanikiwa wanafanya kile wanachokipenda ndiyo maana wanakifanya kwa bidii na kwa ufanisi mkubwa.

Ni muhimu kujifunza tabia hii ya kufanya kile unachokipenda kutoka kwa watu waliofanikiwa ili tuweze kufikia ndoto zetu.

5. Wanaweka malengo

Hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa bila malengo chini ya jua. Malengo ni mwongozo wa wewe kufikia mafanikio yako.

Watu waliofanikiwa wamejenga tabia ya kujiwekea malengo stahiki pamoja na mikakati ya kuyatimiza. Kila mara wanahakikisha wanafanya jambo kufikia au kuendeleza lengo lao.

Ni muhimu kufahamu kuwa lengo ni matokeo ambayo mtu anataka kuyafikia katika kipindi fulani cha muda; hivyo ni muhimu kubainisha matokeo hayo pamoja na njia utakazotumia ili kuyafikia.

Soma pia: Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani.

6. Wanasoma sana

“Kusoma ni zana ya msingi katika kuishi maisha mazuri.”

Joseph Addison

Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma. Watu husoma ikiwa kuna mitihani au kitu kingine cha lazima sana.

Watu waliofanikiwa wanasoma vitabu na makala nyingi kila mara kadri wanavyoweza. Mfano mzuri ni bilionea Bill Gates na Mark Zuckeberg, hawa wamekuwa mabalozi wakubwa wa vitabu pamoja na kuwahamasisha watu kusoma vitabu.

Kuna maarifa na hekima kubwa sana iliyofichwa kwenye vitabu; hivyo ni muhimu kujiwekea utaratibu wa kusoma vitabu na makala mbalimbali kama hii unayoisoma kutoka Fahamuhili.com.

Epuka au punguza kusoma vitu visivyo na tija kama vile udaku na maswala ya burudani.

7. Wanathubutu

Watu wengi wana mawazo mazuri lakini wana hofu na wasiwasi wa kuyafanyia kazi mawazo yao. Hali hii ni kinyume kwa watu waliofanikiwa kwani wao hufanya juu chini ili kufanyia kazi mawazo yao.

Hawaogopi kushindwa wala kupata hasara. Hivyo ikiwa tunataka kufanikiwa, ni lazima tuwe na udhubutu na ujasiri wa kufanya mambo.

“Ndoto zetu zote zinaweza kutokea ikiwa tuna ujasiri wa kuzifuata.”

Wale Disney

Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

8. Wanalinda afya zao

Afya njema ndiyo msingi wa mafanikio yetu. Kamwe hatuwezi kuzalisha au kufanya kazi yoyote yenye tija ikiwa hatutakuwa na afya njema.

Watu waliofanikiwa wamejijengea utamaduni wa kukagua afya zao pamoja na kufanya mambo mbalimbali ili kuzilinda.

Ni muhimu kuhakikisha tunafanya mazoezi, tunakula chakula bora pamoja na kufanya uchunguzi wa kitabibu kila tupatapo nafasi.

9. Wanajali muda

Kutokujali muda ni tatizo linalowakabili watu wengi. Kutokana na kukosa utaratibu mzuri wa kutekeleza majukumu, watu wengi hupoteza muda kwenye mambo ambayo hayana maana.

Watu waliofanikiwa wana ratiba iliyopangiliwa vizuri na wanayoifuata kila siku. Hawatawaliwi na mambo kama vile sherehe, mitandao ya kijamii, starehe, marafiki, michezo n.k.

Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda.

10. Wanajenga mahusiano

Siri nyingine ya mafanikio inayofahamika vyema kwa watu waliofanikiwa, ni kujega mtandao (network) wa mahusiano na watu sahihi. Ili kukamilisha lengo au maono yako ni lazima utahitaji watu fulani kwa namna moja au nyingine.

Hivyo ni muhimu kujenga mtandao wa mahusiano na watu sahihi ambao watakuwezesha kwa njia moja au nyingine kufikia lengo lako.

Hapa namkubuka blogger na marketer maaraufu Neil Patel, anaeleza kuwa kwa njia ya kujenga mahusiano na watu wakubwa ameweza kupata kazi kubwa zenye pesa nyingi.

Soma pia: Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako.

Hitimisho

Naamini sasa hutoota tena mafaniko bali utaanza kuyatengeneza na kuyaishi. Ni wazi kuwa ili tuweze kufanikiwa ni lazima tuwe na tabia kama za watu waliofanikiwa. Je una tabia tajwa hapo juu?

Tafadhali tushirikishe maoni yako hapo chini bila kusahau kuwashirikisha wengine makala hii. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3.8 12 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

29 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jovin
Jovin
4 years ago

Ni nzuri na nimependa katika upande Wa kujenga network asante

Misinzo shija
Misinzo shija
4 years ago

Nimeshukur sana maana changamoto nyingi zinanikumba kwenye safar yangu yamafanikio

Deus
Deus
Reply to  Misinzo shija
3 years ago

imekaa vizuri

Sabyna
Sabyna
4 years ago

Nashukuru Mungu kwa mwandishi nimejifunza kitu

merina
merina
3 years ago

Asante kwa kunifungua

John mlewa
John mlewa
3 years ago

Nimeipenda hii

Frank
Frank
2 years ago

Mungu akubaliki makala hii imenipa Mwanga na kujitafakali mmi mwenyewe. Makala hii ni meipenda mnooo

Wallace
Wallace
1 year ago

Kwakweli nimepana elimu bora sana, katika hatua yangu ya mafanikio

Wallace
Wallace
1 year ago

Nimepata somo

Pius mibaroy
Pius mibaroy
1 year ago

Me kwa upended wangu nimesha gundua vitu flan ambavyo hua ni lazimq uvitekeleza ili uweze kufikia malengo

Siraj ramadhan
Siraj ramadhan
1 year ago

Am so interested in your different articles, i would like to join more. 0762344492

Benson Humphrey
Benson Humphrey
1 year ago

nimefurahiii sanaaa nimejifunzaa vizurii sana na kuelewa jinsi ya kufanya mambo kwa uhakikaa zaidii thanks bro

Zengo Emmanuel
Zengo Emmanuel
1 year ago

Very nice

Allan Odhiambo Ogutu
Allan Odhiambo Ogutu
1 year ago

Napendezwa

Filbert mashaka
Filbert mashaka
1 year ago

Napenda nakara hii

trackback
MAMBO 3 WANAYOFANYA WATU WALIOFANIKIWA. - Kingi Kigongo
1 year ago

[…] watu waliofanikiwa duniani.1. Ni wasomaji wazuri sana wa vitabu.Jambo la kwanza kabisa ambalo watu waliofanikiwa hufanya ni wasomaji wazuri sana wa vitabu. Ukifuatilia matajiri wote wakubwa wa dunia kama vile […]

KESARI FABIANO NKANJIRA
KESARI FABIANO NKANJIRA
7 months ago

Asante sana nimeyaelewa mawazo yako, nathan nitafanya mabadiliko makubwa kwa hiki nilichojifunza.

29
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x