Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani - Fahamu Hili
Friday, September 29Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Malengo

Kabla hujakamilisha chochote maishani, ni lazima ufahamu unahitaji nini. Ni lazima ukae chini utafakari kama kile unachokifanya kina thamani kwako; ikiwa hakina thamani, basi tenga muda ujiwekee malengo yenye maana kwako.

“Maisha bila malengo ni sawa na kuanza safari bila kufahamu unakotaka kwenda au kufika.”

Kujiwekea malengo maishani kuna umuhimu mkubwa kwani hutufanya tujikite sawasawa kwenye kila tunachokifanya.

“Kujiwekea malengo ni hatua ya kwanza ya kufanya visivyoonekana vionekane”

Tony Robbins

Je uko tayari kuweka malengo? Karibu nikufahamishe faida 10 utakazozipata ikiwa utajiwekea malengo maishani mwako.

1. Hukupa mwongozo

Awali ya yote, malengo hukupa mwongozo na mwelekeo maishani mwako. Malengo hukuwezesha kubaini kitu unachokilenga, na hukufanya uelekeze nguvu zako kwenye kitu husika.

Badala ya kushika hiki na kile au kuwa huyu na yule, malengo yatakuwezesha kufahamu unatakiwa kufanya nini au kuwa nani.

2. Hukuwezesha kufanya maamuzi

Baada ya kujiwekea malengo utaweza kubaini ni maamuzi gani yanafaa na ni yapi hayafai kulingana na malengo uliyojiwekea.

Pia utaweza kufahamu mambo ya msingi maishani mwako, hivyo utaweza kufanya maamuzi kulingana na mambo hayo.

Mtu mwenye malengo huwa makini kwenye maamuzi yake kwani analinda asije akafanya maamuzi yatakayoathiri lengo lake.

3. Hukuwezesha kutawala baadaye yako

Unapokuwa na malengo na mipango stahiki ya kuyatimiza, ni wazi kuwa moja kwa moja umeshatawala baadaye yako.

Kuweka malengo ni jambo zuri ambalo litakuwezesha kufahamu aina na mfumo wa maisha yako ya baadaye. Jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa unaweka mipango sahihi na inayotekelezeka ya kutimiza malengo yako.

Ni muhimu kuhakikisha kila siku kuna kitu kinachofanyika ili kukamilisha sehemu fulani ya malengo uliyojiwekea maishani.

“Malengo ni ramani ya barabara inayokuongoza na kukuonyesha ni nini kinawezekana kwenye maisha yako”

Les Brown

4. Hukuwezesha kujikita kwenye mambo muhimu

Kuna mambo mengi kwenye maisha yetu ya kilasiku, lakini siyo yote ni ya muhimu kwenye kutimiza ndoto zetu.

Ukiwa na malengo ni rahisi kubaini mipango au mambo yasiyokuwa na umuhimu kwa kutazama yale yote yanayokinzana na malengo yako.

Haijalishi unalipenda jambo fulani kwa kiasi gani, kama linakinzana na malengo yako, basi huna budi kuliacha.

5. Malengo hukuhamasisha

Unapotazama uzuri na ubora wa malengo yako unapata matumaini na hamasa kubwa.

Hamasa huzidi pale ambapo unaanza kuona ukikamilisha malengo yako ya muda mfupi; hili hukuhamasisha kufanya bidii zaidi ili kuyafikia yale ya muda mrefu.

Ni wazi kuwa chanzo kizuri cha hamasa, ni kujiwekea malengo na kuanza kuyatimiza.

“Jenga ndoto zako wewe mwenyewe, la sivyo mtu mwingine atakuajiri kujenga zake.”

Farrah Gray

Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

6. Hutusaidia tusipoteze muda

Mtu mwenye malengo kamwe hawezi kupoteza muda. Ukiwa una malengo ni wazi kuwa muda wako wote utakuwa umegawanywa kwenye kuyafanyia kazi na kuyatimiza malengo yako.

Kwa njia ya kujiwekea malengo hutopoteza muda kwa kufanya mambo ambayo hayakuwezeshi kufikia ndoto na malengo yako.

Haitarajiwi mtu mwenye malengo kuwa mlevi, mvivu, anayechelewa kuamka, anayeshinda kwenye mitandao ya kijamii au vijiwe n.k.

Soma pia: Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi.

7. Hukuwezesha kufanya uwekezaji sahihi

Ukiwa na malengo ni wazi kuwa utafahamu nini, wapi na lini uwekeze; kwani malengo yako yatakuwezesha kubaini ni uwekezaji gani unaoendana na lengo lako.

Lakini usipokuwa na malengo utawekeza kwenye kila kitu kinachokuja mbele yako na matokeo yake hutoweza kufanikiwa.

8. Malengo hukuwezesha kujitathimini

Unapimaje kufanikiwa kwako kama huna kipimo cha kupimia kufanikiwa huko? Malengo ni kipimo muhimu kitakachokuwezesha kutathimini kama umefanikiwa au la.

Ukiwa na malengo ni rahisi kutazama kama yale uliyoyafanya au unayoyafanya yamekuwezesha kutimiza au kufikia lengo lako.

Ikiwa yamekuwezesha, basi unafanya vizuri; lakini ikiwa hayajakuwezesha kufikia lengo, basi kuna mambo ya kuyatazama upya.

9. Hukufanya upende kile unachokifanya

Kama nilivyotangulia kusema pale awali, kuwa malengo hukuongoza kufahamu unatakiwa kufanya nini, malengo pia yatakuwezesha upende kile unachokifanya.

Ni ukweli usiopingika kuwa ukifanya kitu ambacho unajua kinakamilisha malengo yako utakipenda. Hivyo ni muhimu kuwa na malengo ili yatufanye tupende kile tunachokifanya.

Kwa mfano ukiwa na lengo la kupata kipato cha Sh. 7,000,000 kwa mwezi, ni wazi kuwa utapenda kile unachokifanya kwani kinakuwezesha kutimiza lengo lako.

10. Ujasiri binafsi

Watu wenye malengo wana ujasiri binafsi mkubwa, wanaamini wao siyo kama watu wengine kwa sababu kuna vitu wanavyoviona tofauti na watu wengine.

Mtu mwenye malengo anajiamini kuhusu maisha yake ya sasa na ya baadaye kwa sababu ana mipango na mikakati stahiki katika maisha yake.

Neno la mwisho:

Kumbuka “mpango mzuri leo ni bora kuliko mpango mkamilifu kesho.” Naamini umefahamu wazi umuhimu wa kujiwekea malengo maishani mwako. Je wewe una malengo? Je unafanya kazi kuyatimiza?

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini pia usisahau kuwashirikisha wengie makala hii. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3.8 5 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

22 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Joe Lee
Joe Lee
4 years ago

Ni mwanga, ni bora zaidi nimeipenda hii

Djuma Nassor
Djuma Nassor
3 years ago

Nimefaikidaka saana kwa nakala zako mbalimbali, endelea na juhidi ya kufunza jamii. Mungu atakulipa

Barakat
Barakat
3 years ago

Shukran sana sasa kuanzia leo naamka nakuwa mpya kabisa thanks broo

Daud Leonard sahani
Daud Leonard sahani
3 years ago

Hongera Sana nimejifunza mengi na ninaendelea kupata mengi zaidi hakika hakili inapata chakula kizuri

Amos mbise
Amos mbise
Reply to  Daud Leonard sahani
3 years ago

Nashkuru sana kwa masomo yenu mazuri yanatufundisha na kutujenga katika msingi ulio Bora zaidi so

Reginald
Reginald
3 years ago

Ahsante sana

Privanus katinhila
Privanus katinhila
2 years ago

Ni faraja kubwa kwangu kuona Taifa lina wadau wanao weza kusaidia wengine kwa kutoa mchango chanya. Hongera sana

KingEga
KingEga
2 years ago

Yes

Baba Benny
Baba Benny
1 year ago

Thank you so much for this education be blessed

Leonard Levi
Leonard Levi
1 year ago

May the Almighty God bless you for these wonderful teachings

Leonard Levi
Leonard Levi
1 year ago

Good massege

22
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x