Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora - Fahamu Hili
Monday, May 25Maarifa Bila Kikomo

Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Je kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wengi au miaka mingi katika uongozi? La hasha, kiongozi bora hujengwa kwa sifa anuwai.

Ni rahisi kufikiri kuwa kiongozi bora hutokea kwa bahati tu au hakuna haja ya kujifunza jinsi ya kuwa kiongozi bora. Wewe kama mtu anayehitaji kusimamia na kuratibu shughuli mbalimbali ni lazima ufahamu sifa zinazomfanya mtu kuwa kiongozi bora ili uwe na mafaniko.

“Kama matendo yako yanawahamasisha wengine kupata ndoto zaidi, kujifunza zaidi, kufanya na kuwa zaidi, wewe ni kiongozi.”

John Quincy Adams

Katika makala hii utaweza kufahamu sifa 10 zitakazokufanya kuwa kiongozi bora.

1. Uwazi

Uwazi ni sifa muhimu inayomfanya mtu kuwa kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima awe wazi katika utendaji kazi wake.

Uwapo kiongozi kuna siri za kazi lakini namna ya utendaji kazi hautakiwi uwe siri au usioeleweka kwa wale unaowaongoza. Kiongozi bora anatakiwa kuwa na mpangilio mzuri na unaoeleweka wa utendaji kazi wake.

2. Maono

“Kiongozi ni yule anayejua njia, anakwenda njia hiyo na anaonyesha njia.”

John C. Maxwell

Maono ni picha inayojengeka katika fikira ya matokeo ya jambo ambalo linapangwa kutekelezwa.

Kama wewe ni kiongozi asiyeweza kuona picha ya baadaye ya kampuni au taasisi hutawea kuiongoza kampuni kufikia mafaniko na malengo yake. Jitahidi kujifunza kuwa na maono katika jambo lolote unalolifanya ili lifanikiwe.

3. Uadilifu

Ili uwe kiongozi bora huna budi kuwa mwadilifu. Heshimu kazi, tunza muda, tunza fedha pia tumia nafasi yako kwa njia amabyo si ya kibadhirifu.

Ni rahisi mtu kushawishika kutumia ofisi au nafasi ya kiuongozi kwa maslahi binafsi jambo ambalo linamfanya kupoteza sifa yake ya kiongozo bora.

4. Ujasiri

Huwezi kuwa kiongozi bora kama hutakuwa na ujasiri katika maswala mbalimbali. Unahitaji ujasiri kufanya maamuzi mbalimbali katika eneo au taasisi unayoiongoza kama vile kufanya uwekezaji mpya, kubadili mfumo wa utendaji kampuni au taasisi n.k.

Lazima kiongozi aoneshe ujasiri kwa watawaliwa au wafanyakazi wengine katika maamuzi yake anayoyafanya kila siku.

5. Subira

Kuna mambo yanayohitaji subira katika maisha. Kiongozi asiye bora hutaka kila kitu kitimie kwa siku moja. Kuwa kiongozi mkomavu ni kuwa subira na uvumilivu.

Wakati mweingine kampuni au taasisi yako inaweza kuwa inapita kwenye kipindi kigumu; usipokuwa kiongozi mwenye subira unaweza kufanya maamuzi ambayo yataathiri kampuni daima.

6. Mbunifu

“Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”

Steve Jobs

Kufankiwa kwa kampuni au taasisi kunahitaji ubunifu wa hali ya juu kila mara. Hivyo basi ili uweze kuwa kiongozi bora jitahidi kuwa mbunifu.

Buni mbinu, mawazo na miradi mbalimbali ambayo itawezesha kampuni au taasisi kukua na kufikia malengo yake.

Epuka kutegemea mawazo ya zamani hata kama bado yanailetea kampuni faida kwani mambo yanaweza kubadilika wakati wowote.

7. Uwajibikaji

“Uongozi ni kuwa mtumishi kwanza.”

Allen West

Ukitaka kuwa kiongozi bora huwezi kujitenga na uwajibikaji. Lazima uwajibike kutimiza majukumu yako yote.

Utawezaje kuwaongoza na kuwahimiza wengine kutimiza majukumu yao kama wewe mwenyewe huwezi kutimiza majukumu yako? Nasisitiza tena kwa kusema wajibika katika nafasi yako na wale unaowaongoza watawajibika katika nafasi zao.

8. Kujituma

Kujituma ni jambo muhimu sana kwa kiongozi bora. Kiongozi bora hahitaji sheria na usimamizi mkali ili atimize majukumu yake.

Hivyo basi, ukitaka kuwa kiongozi bora ni lazima ujifunze kujituma bila kusukumwa na mtu. Fanya bidii uwapo kazini au katika nafasi yako yaa kiuongozi; hili litakujenga na kukufanya kuwa kiongozi bora.

9. Mawasiliano

Mawasiliano ni swala muhimu sana linalojenga utawala bora. Katika taasisi au kampuni isiyokuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano lazima kutatokea migongano na misuguano isiyokuwa na sababu.

Ukiwa kiongozi hakikisha unakuwa na mfumo mzuri wa mawasiliano na watu wengine katika taasisi au kampuni unayoiongoza. Hakikisha pia unajenga mfano mzuri wa kutoa taarifa katika kampuni au taasisi iliyopo.

10. Nidhamu

Kuna mambo ambayo huwezi kufanya unapokuwa kiongozi hata kama wengine wanayafanya au unavutiwa nayo. Siku zote epuka tabia zisizo endana na kiongozi bora kama vile ulevi, umbeya, uvivu, anasa, starehe, kuongea hovyo n.k.

Onesha watu unaowaongoza kuwa wewe ni kiongozi mwenye uelewa uliokujengea nidhamu na kujitawala.

Hitimisho

Hapa nimekueleza sifa kumi zitakazo kuwezesha kuwa kiongozi bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa kiongozi atakayeleta mabadiliko katika taasisi au kampuni unayoiongoza kama hutojifuza kuwa kiongozi bora.

Je una maoni gani juu ya hoja zilizojadiliwa hapa pamoja na suala zima la kiongozi bora? Tafadhali tupe maoni yako hapa chini tafadhali. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

Washirikishe Wengine Makala Hii:

15
Tafadhali tuandikie maoni yako:

avatar
7 Comment threads
8 Thread replies
3 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
8 Comment authors
Abeid Juma Abeid HekeScarfaceKornelio MaangaElias Davidgeorge Recent comment authors
newest oldest most voted
Abubakary Ahmed
Guest
Abubakary Ahmed

Hongera kiongozi

spajo
Guest
spajo

nmeipendaaa

samwel
Guest
samwel

well done

george
Guest
george

Napenda sifa hizi na ni nzuri na nilizitumia chache zikaniletea faida; ila asante kwa kusijua nyingine .

Elias David
Guest
Elias David

Nimefurahishwa na uchambuzi wenu

Scarface
Guest
Scarface

Yamegusa nyoyo za watu wengi na kila kiongozi angependa kufuata hizi kanuni.

Abeid Juma Abeid Heke
Guest
Abeid Juma Abeid Heke

Nime elewa Sana juu y’all sifa za Kuwa kiongozi bora. Hongera Sana kwa kuelimisha jamii