
Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako
Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako. Ni kweli kuwa baadhi ya watu huanza maisha katika mazingira rafiki zaidi, lakini ninaamini kila mmoja ana nafasi na uwezo ya kufanikiwa. Haya ni baadhi mambo ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya na kujiambia na yamewatenga na mafanikio yao.
1. Ninahitaji shahada ya chuo kikuu ili kufanikiwa
Unahitaji shahada kupata kazi katika ofisi fulani lakini si kuwa majasiriamali katika ofisi yako wewe mwenyewe. Ipo mifano kadha wa kadha duniani ya watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wakubwa bila kuwa na shahada ya chuo kikuu. Mfano wa watu hao ni Mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg. Hivyo basi fanya maamuzi leo ili ufikie kiwango bora cha...