
Sababu 7 za Kwa nini Hutakiwi Kucheza Michezo ya Kubahatisha
Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi au changamoto za maisha watu wengi hutekwa na mambo mbalimbali hasa yale yanayohusu kupata pesa za haraka. Nilipofanya utafiti mdogo nilibaini kuwa “njia za kupata pesa kwa haraka” pamoja na “njia za kupata utajiri kwa haraka” ni moja kati ya vitu vinavyotafutwa sana na watu kwenye mtandao. Hii inadhihirisha uhitaji mkubwa wa watu kutaka kupata pesa, tena kwa muda mfupi. Hivyo basi, hili limepelekea watu wengi kutekwa na michezo ya bahati nasibu wakifikiri kuwa inaweza kuwatoa katika matatizo au mahitaji yao ya kifedha. Haijalishi unacheza au huchezi michezo ya kubahatisha, karibu nikufahamishe sababu 7 za kwanini hutakiwi kucheza michezo ya kubahatisha.
1. Ni biashara
Hakuna mtu atakayetoka China, India au Marekani ili aje Afrika kukugawia...