
Madaraja 15 Makubwa au Marefu Zaidi Duniani
Kwa siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa maendeleo makubwa katika shughuli mbalimbali za binadamu. Sekta ya ujenzi na usafiri ni moja kati ya sekta ambazo binadamu amepiga hatua kubwa. Kila siku kumekuwa kukibuniwa na kufanyika maboresho mbalimbali katika miundombinu ya usafirishaji. Kumeshuhudiwa ujenzi wa barabara za kisasa, reli, viwanja vya ndege au hata kubuniwa kwa baadhi ya aina mpya za usafiri. Kutokana na hili, yapo madaraja mbalimbali yaliyojengwa sehemu mbalimbali duniani ili kuboresha usafiri wa barabara na reli. Karibu uongeze maarifa yako kwa kufahamu madaraja 15 makubwa au marefu zaidi duniani kwa sasa.
1. Daraja la Danyang–Kunshan
Daraja la Danyang–Kunshan ndilo daraja refu kuliko yote duniani, lina urefu wa kilometa 164.8. Daraja hili linapatikana huko China kat...