Kila siku binadamu anafanya shughuli mbalimbali katika kuandaa au kutengeneza mazingira bora kwa ajili yake kuishi. Kazi hii zinahusisha ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, makazi, viwanda, ofisi n.k.
Hata hivyo, shughuli hizi za binadamu hupelekea uharibifu mkubwa wa mazingira ya asili ikiwemo misitu, mito, milima, wanyama, maziwa, hewa n.k
Wapo watu waliolitambua hili na kuamua kufanya kazi zao kwa kuzingatia kulinda na kuheshimu mazingira ya asili. Karibu utazame picha kadha wa kadha zinazonyesha kazi hizo.
1. Nyumba ya duara iliyojengewa kwenye mti huko Tokyo, Japan
2. Mgahawa wa kahawa huko Shanghai, China
3. Mti katikati ya nyumba huko Almaty, Kazakhstan
4. Mti kwenye hoteli huko Izmir Uturuki
5. Nyumba ya makazi huko West Virginia
6. Nyumba iliyojengwa katikati ya miti huko Poland
7. Mti katikati ya nyumba huko Rio de Janeiro, Brazil
8. Makazi binafsi huko Austin, Texas
9. 25 Green, huko Turin, Italia
10. Barabara iliyoheshimu mti
Naamini umeona na kujifunza kuwa inawezekana kufanya shughuli mbalimbali kama vile ujenzi huku tukilinda mazingira ya asili. Kuna umuhimu mkubwa wa kutunza mazingira ya asili ili nayo yatunze uhai wa vizazi vya sasa na baadaye.
Soma pia: China Kujenga “Mji Msitu” Ambao Utakuwa na Mamilioni ya Mimea na Miti 40,000.
Je una swali au maoni yoyote? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.