Inawezekana unabeba pesa kwenye pochi au mfuko wako au pengine umezitunza benki, lakini ni kwa kiasi gani unafahamu kuhusu pesa? Ni dhahiri kuwa unaweza kuzitumia pesa hadi mwisho wa maisha yako bila hata kujua mambo fulani yanayozihusu. Fuatilia makala hii nikufahamishe mambo 6 usiyoyafahamu kuhusu pesa.
1. Pesa ya noti siyo karatasi
Watu wengi wanafikiri kuwa pesa ya noti imetengenezwa kwa karatasi lakini si kweli. Malighafi zilizotengenezea pesa ya noti, mojawapo ni pamba. Imetengenezwa hivi ili iwe imara zaidi na yenye kukabiliana na mambo kama vile vimiminika na uchafu.
2. Wazo la ATM liliibuka bafuni
Mgunduzi John Shepherd-Barron alipata wazo la kuweka ATM bafuni manamo miaka ya 1960 akiwa bafuni.
3. Pesa zina virusi vya mafua na cocaine
Utafiti umebaini kuwa kutokana na pesa kupita kwenye mikono na sehemu mbalimbali, nyingi zina virusi vya mafua na chembechembe za madawa ya kulevya (cocaine).
4. Wote walio hai sasa walizikuta pesa
Hii ina maana gani? Inaaminika kuwa pesa zilianza kutumika mnamo miaka 5,000 K.B. Ni dhahiri kuwa watu wote walio hai duniani leo walizikuta pesa na kuna uwezekano wakaondoka kabla ya kuja kwa mbadala wa pesa.
5. Asili ya pesa za noti ni China
Inaaminika kuwa pesa za noti zilibuniwa huko China. Mnamo mwaka wa 910 pesa hizi zilimshangaza Marco Polo alipotembelea China katika safari zake.
6. Kutengeneza pesa ni taaluma ngumu
Watu wengi wanafahamu kuwa madaktari na wanasheria wanahitaji miaka mingi (5 – 6) kufuzu taaluma zao. Lakini taaluma ya kutengeneza pesa “engraiving” inahitaji miaka takriban 15 ili kufuzu. Hii pia ndiyo sababu ni vigumu kutengeneza pesa bandia ambazo hazitobainika.
Naamini umepata maarifa fulani ambayo awali haukuwa nayo. Tungependa kupokea maoni, au maswali kutoka kwako, Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.