Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu - Fahamu Hili
Thursday, March 28Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Hofu

Hofu ni hisia ambazo zinatulinda na vitisho vinavyotuzunguka. Kila mtu ana hofu, lakini viwango na aina ya hofu hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Wapo watu ambao huhofu juu ya vitu na mambo mbalimbali hadi kushindwa kuendelea na majukumu au maisha yao ya kawaida.

Ikiwa unapenda kufahamu aina za hofu (phobia) ili pia uchunguze kama una aina hizo basi fuatilia makala hii nikufahamishe aina 70 za hofu.

  1. Pogonophobia – Pogonophobia ni hofu ya kuogopa ndevu au kukaa karibu na mtu mwenye ndevu. Hofu hii huwapata zaidi wanawake.
  2. Astraphobia – Hofu hii pia inajulikana kama astrapophobia, brontophobia, keraunophobia, au tonitrophobia; hii ni hofu ya kuogopa radi.
  3. Photophobia – Hii ni hofu ya kuogopa mwanga; mara nyingi husababishwa na matatizo ya kiafya ya macho.

Soma pia: Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona.

  1. Zoophobia – Hii ni hofu ya kuogopa wanyama.
  2. Achievemephobia – Hii ni hofu ya kuogopa mafanikio. Je unaogopa kufanikiwa? Je unafikiri ukifanikiwa utaibiwa? Ikiwa jibu ni ndiyo basi una Achievemephobia.
  3. Thalassophobia – Hii ni hofu ya bahari; mawimbi, maji na wanyama wake.
  4. Musophobia – Hii ni hofu ya kuogopa panya.
  5. Enochlophobia – Hofu ya kuogopa mkusanyiko wa watu. Ikiwa unaogopa kukaa au kusimama mbele ya mkusanyiko wa watu, basi huenda una aina hii ya hofu.
  6. Xenophobia – Kuogopa watu au vitu visivyofahamika au vigeni.
  7. Iatrophobia – Hii ni hofu ya kuogopa daktari.
  8. Hippopotomonstrosesquippedaliophobia – Hii ni hofu ya kuogopa maneno marefu. Je unaogopa kusoma au kuandika maneno marefu? Ikiwa ndiyo, basi huenda una hofu hii.
  9. Agliophobia – Hii ni hofu ya kuogopa maumivu. Pia kuogopa juu ya kitu chenye maumivu kinachoweza kutokea.
  10. Myrmecophobia – Hofu ya kuogopa wadudu.
  11. Arachnophobia – Hii ni hofu ya kuogopa buibui; hofu hii inaathiri wanawake kwa asilimia 48 na wanaume asilimia 12.
  12. Alektorophobia – Hofu ya kuogopa kuku. Je kuku anakufanya uchanganyikiwe au ukose amani?
  13. Anthropophobia – Hii ni hofu ya kuogopa watu.
  14. Gephyrophobia – Je huwa unaogopa unapofika kwenye daraja? Basi inawezekana una Gephyrophobia. Hii ni hofu ya kuogopa madaraja.
  15. Gerascophobia – Hofu ya kuogopa kuzeeka. Kusogea kwa umri ni kitu cha kawaida, lakini watu wengi huhofia hili.
  16. Telephonophobia – Hofu ya kuogopa kuongea kwa simu.
  17. Ligyrophobia – Hofu ya sauti kubwa au kelele.
  18. Ombrophobia – Hofu ya mvua. Je unaogopa mvua? Ikiwa unaogopa mvua basi utakuwa una Ombrophobia.
  19. Equinophobia – Hii ni hofu ya kuogopa farasi.
  20. Bathophobia – Hofu ya kuogopa kina (Inaweza kuwa ni kwenye ziwa, bonde, shimo n.k.)
  21. Aerophobia – Hofu ya kuogopa kusafiri au kuruka kwa ndege.
  22. Phobophobia – Hii ni hofu ya kuogopa hofu.
  23. Theophobia – Hofu ya kumwogopa Mungu au dini.
  24. Numerophobia – Hofu ya kuogopa namba na hesabu.
  25. Athazagoraphobia – Hofu ya kuogopa kusahauliwa au kusahau vitu.
  26. Phasmophobia – Hofu ya kuogopa mizimu.
  27. Metathesiophobia – Hofu ya kuogopa mabadiliko. Ikiwa hutaki kubadilika na unataka kubaki jinsi ulivyo, basi inawezekana una hofu hii.
  28. Panophobia – Hofu ya kuogopa kila kitu au kuhofia kuwa vitu vibaya vitatokea.
  29. Hemophobia – Hofu ya kuogopa damu.
  30. Vehophobia – Hofu ya kuendesha gari.
  31. Cibophobia – Hofu ya kuogopa chakula.
  32. Somniphobia – Hofu ya kulala. Kuhofia nini kinaweza kutokea mara baada ya wewe kulala.
  33. Taphophobia – Hofu ya kuogopa kuzikwa ukiwa hai kwa makosa na kuamka ndani ya jeneza ardhini.
  34. Pediophobia – Hofu ya kuogopa midoli.
  35. Scelerophobia – Hofu ya kuhofia wahalifu au uhalifu.
  36. Catoptrophobia – Hofu ya kuogopa kioo au mwonekano wako kwenye kioo.
  37. Galeophobia – Hofu ya kuogopa samaki aina ya papa.
  38. Philophobia – Kuogopa kupenda au hisia za kupenda.
  39. Ranidaphobia – Hofu ya kuogopa vyura.
  40. Apiphobia – Hofu ya kuogopa nyuki.
  41. Atychiphobia – Hofu ya kuogopa kushindwa. Hii ni kizuizi kikubwa sana cha mafanikio ya watu wengi.
  42. Basiphobia – Hofu ya kuogopa kuanguka. Wengine hata wakiwa wanatembea hupata hofu hii.
  43. Ichthyophobia – Hofu ya kuogopa samaki.
  44. Nyctophobia – Hofu ya giza. Mara nyingi hofu hii hutokea kwa watoto.
  45. Ailurophobia au Gatophobia – Hofu ya kuogopa paka. Inaelezwa kuwa Benito Mussolini na Adolf Hitler walikuwa na hofu hii.
  46. Glossophobia – Hofu ya kuogopa kuongea mbele za watu.

Soma pia: Njia 10 za Kujenga Uwezo wa Kuzungumza Mbele ya Watu.

  1. Gynophobia – Hofu ya kuogopa wanawake.
  2. Trypanophobia – Hofu ya kuogopa sindano.
  3. Bananaphobia – Hofu ya kuogopa ndizi.
  4. Technophobia – Hofu ya kuogopa teknolojia.
  5. Katsaridaphobia – Hofu ya kuogopa mende. Hii huwafanya baadhi ya watu kufanya usafi wa kupindukia ili kuondoa mende.
  6. Chronophobia – Hofu ya kuogopa juu ya baadaye; watu wengi huhofia nini kitatokea kwenye baadaye zao hivyo wanakuwa na hofu.

Soma pia: Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako.

  1. Didaskaleinophobia – Hofu ya kuogopa kwenda shule.
  2. Cacomorphobia – Hofu ya kuogopa watu wanene.
  3. Aphenphosmphobia – Hofu ya kuogopa ukaribu au uhusiano wa kimapenzi.
  4. Lepidopterophobia – Hofu ya vipepeo na wadudu wengine warukao.
  5. Autophobia – Hofu ya kuogopa kuachwa au kutelekezwa na mtu fulani.
  6. Carcinophobia – Hofu ya kuogopa saratani (Cancer).
  7. Globophobia – Hofu ya kuogopa mapulizo au maputo. Mapulizo ni mapambo mazuri lakini kwa wengine huwatisha.
  8. Ornithophobia – Hofu ya kuogopa ndege.
  9. Aquaphobia – Hofu ya kuogopa maji.
  10. Cynophobia – Hofu ya kuogopa mbwa. Je una hofu hii? Kama unayo basi tuko pamoja, mimi pia naogopa mbwa.
  11. Pyrophobia – Hofu ya kuogopa moto.
  12. Thanatophobia – Hofu ya kifo.
  13. Ophidiophobia – Hofu ya kuogopa nyoka.
  14. Androphobia – Hofu ya kuogopa wanaume.
  15. Tokophobia – Hofu ya kuogopa kupata ujauzito na kujifungua.

Zipo aina nyingi sana za hofu (Phobia), lakini naamini kwa hizi chache umebaini aina yako au umejifunza jambo fulani. Je wewe una aina gani ya hofu? Unaishindaje?

Soma pia: Njia 7 Bora za Kushinda au Kukabiliana na Hofu.

Tafadhali tuandikie maoni na maswali yako hapo chini bila kusahau kuwashirikisha wengine makala hii. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

2 1 vote
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x