
Athari au Madhara 10 ya Intaneti Unayopaswa Kuyafahamu
Katika dunia hii ya leo ni vigumu kuishi bila kutumia intaneti kwa namna moja au nyingine. Watu hutumia intaneti kuwasiliana, kupata taarifa na habari au hata kujipatia kipato. Kuwepo kwa intaneti kumerahisisha maisha ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa na kufanya utendaji kazi wake uwe bora zaidi. Pamoja na intaneti kuwa na manufaa kadha wa kadha, intaneti ina athari mbalimbali. Hivyo basi fahamu madhara 10 ya intaneti.
1. Taarifa za uongo
Kila mtu anaweza kuweka taarifa kwenye mtandao wa intaneti, hivyo ni rahisi kukumbana na taarifa zisizo za kweli. Swala hili limepelekea baadhi ya nchi na mashirika mbalimbali kujaribu kukabili taarifa mbalimbali zinazopatikana kwenye mtandao ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na taarifa hizo. Ni vyema kuhakikisha tovuti au blog ...