
Kwa kuwa vitabu ni kisima kikubwa cha maarifa, kila mara teknolojia inakuja na mbinu mbalimbali zitakazotuwezesha kuvuna maarifa haya.
Ikiwa unapenda kusoma vitabu au una nia ya kusoma vitabu, basi fahamu programu ya Balabolka itakayokuwezesha kusoma maandishi au vitabu kwa sauti au kuvibadili kuwa sauti ili uvisikilize badala ya kuvisoma.
Hivyo kwa kutumia programu hii unaweza kusoma vitabu pepe kwa urahisi kabisa na mahali popote bila kizuizi. Badala ya kusikiliza mziki siku nzima sasa unaweza kusikiliza vitabu.
Sifa za programu ya Balabolka
- Ni programu ya BURE
- Inaweza kusoma vitabu vya lugha mbalimbali kama vile Kiingereza, Kiarabu, Kijerumani, Kifaransa, Kichina, n.k.
- Inaweza kubadili kitabu kuwa faili la sauti kama vile WAV, MP3, MP4, OGG au WMA
- Inaweza kusoma vitabu pepe vilivyoko kwenye muundo wa AZW, AZW3, CHM, DjVu, DOC, DOCX, EML, EPUB, FB2, HTML, LIT, MOBI, ODS, ODT, PDB, PRC, PDF, RTF, TCR, WPD, XLS, XLSX.
Jinsi ya kupakua na kusakinisha (install) programu ya Balabolka
- Tembelea Tovuti ya Balabolka na upakue programu hii.
- Ukishaipakua isakinishe (install) proramu ya Balabolka kwenye kompyuta yako.
- Baada ya kusakinisha programu ya Balabolka unaweza kupakua na kusakinisha sauti ya msomaji ya Kiingereza kutoka Microsoft inayojulikana kama SAPI 5 hapa British English (19.4 MB)
- Unaweza kupakua na kusakinisha pia Speech Platform Runtime ili uweze kuongeza sauti zaidi kutoka Runtime Languages. Chagua sauti za lugha unayoitaka zinazoanza na “MSSpeech_TTS_” kisha uzipakue na kuzisakinisha.
Baada ya kufanya michakato hii kwa usahihi unaweza kufungua programu yako ya Balabolka na kuchagua sauti ya msomaji unayoitaka kama ni American English au British English kisha bonyeza Read aloud.
Balabolka ni programu nzuri sana ambayo unaweza kufanya nayo kazi kwa namna tofautitofauti; unaweza kusoma maelezo zaidi kwenye tovuti ya programu hii.
Je bado unapata shida kusoma vitabu au kutumia programu hii? Naamini sasa umepata zana muhimu ambayo itakuwezesha kusoma vitabu kwa urahisi kabisa.
Soma pia: Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu
Ikiwa una maoni au swali tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.