Satelaiti ijulikanayo kama GhanaSat-1, ambayo iliundwa na wanafunzi kutoka katika Chuo Kikuu cha All Nations cha Koforidua, ilirushwa kwenda kwenye mzingo wa dunia kutoka kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
Shange na vifijo vya watu takriban 400 wakiwemo wanafunzi na waandisi walikokuwa wakishuhudia tukio hili zilisikika katika mji wa kusini mwa Ghana. Mji huo ndipo lilipofanyika zoezi hilo la urushaji wa satelaiti hiyo. Mawasiliano na chombo hicho yalianza kupokelewa muda mfupi baada ya chombo hicho kurushwa.
Maradi huo uligharimu dola za kimarekani 50,000 ulifadhiliwa na shirika la Japan Aerospace Exploration Agency (JAXA).
Satelaiti hiyo itatumika katika mambo mabalimbali kama vile kufwatilia ukanda wa pwani wa Ghana, kuchora ramani na kuijengea nchi hiyo uwezo katika anga za juu.
Dkt. Richard Damoah amabaye ni mratibu wa mradi huo akizungumza na BBC alisema kufanikiwa kwa mradi huo ni mwanzo mpya wa taifa hilo katika maswala ya anga za juu. Pia aliongeza kuwa mradi huo utakuwa na manufaa kwa vizazi vya sasa na vya baadaye.
Alifafanua kuwa mradi huo utawezesha miradi kama vile ya utoaji wa mafunzo pamoja na ufwatiliaji wa uchimbaji haramu wa madini.
Kutokana na mafanikio haya yaliyofanywa na wasomi hawa kutoka katika chuo cha All Nations raisi wa Ghana Nana Akufo-Addo amewapongeza wanajamii wote wa chuo hiki kwa kuiweka Ghana katika ulimwengu wa anga za juu.
Je Afrika tutafika? Naamni una maoni kadhaa kuhusu maendeleo haya ya Ghana; tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe na wengine.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.