Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu - Fahamu Hili
Tuesday, March 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Faida za maziwa

Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa?

Ni wakati wako sasa wa kujiuliza kwa kina juu ya faida zitokanazo na unywaji wa maziwa. Fuatana nami katika makala hii nikueleze faida 10 zitokanazo na unywaji wa maziwa.

1. Hujenga na kulainisha ngozi

Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara.

Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku.

2. Huimarisha meno

Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D; hivyo jitahidi kunywa maziwa kwani maziwa huwa na vitamini D.

3. Huimarisha mifupa

Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kunywa maziwa ili kuimarisha ukuaji wao. Ni kweli pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa ili kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya magonjwa kama vile udhaifu wa mifupa (osteoporosis). Maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa na ambayo hufyonzwa kutokana na uwepo wa vitamini D.

4. Kujenga misuli

Maziwa yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli. Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena. Maziwa huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli wakati wa kazi mbalimbali.

5. Kupunguza uzito

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda. Pia maziwa yanaweza kutumiwa kama kileta hamu ya kula yaani appetizer.

6. Huondoa msongo wa mawazo

Hebu fikiri juu ya vitamini na virutubisho vilivyoko kwenye maziwa; hivi huweza kuondoa msongo. Baada ya kazi nyingi za siku, inashauriwa kunywa angalau bilauri (glass) moja ya maziwa ya uvuguvugu. Hili litakusaidia kukuondolea msongo katika misuli na neva zako za fahamu.

7. Huzuia maumivu wakati wa hedhi

Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.

8. Huongeza nguvu za mwili

Je unaishiwa nguvu mapema au kuchoka sana? Kama jibu ni ndiyo, unahitaji virutubisho vilivyoko kwenye maziwa. Hivi vitaupa mwili wako nguvu mpya na kukufanya kuwa mwenye nguvu na furaha siku nzima.

9. Huondoa kiungulia

Kiungulia huwasumbua sana watu wengi. Kiungulia husababishwa na asidi zipatikanazo tumboni. Hivyo maziwa (ambayo si mgando) hutengeneza utando maalumu tumboni ambao hupambana na asidi hizi.

Kwa hiyo nywaji wa maziwa (ambayo si mgando) utakusaidia kupambana na tatizo la kiungulia ndani ya muda mfupi.

10. Hupambana na maradhi mengine

Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha. Magonjwa hayo ni kama vile shinikizo la damu na kiharusi. Inaaminika pia maziwa hupunguza lehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona. Baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.

Hitimisho

Yaliyozungumziwa hapa ni faida 10 za kunywa maziwa. Naamini umebaini kuwa maziwa yana manufaa mengi sana kwa ajili ya afya yako zaidi ya haya yaliyotajwa. Ni jambo jema kujizoesha kula vitu vya asili, kwani ndivyo huhitajiwa zaidi na mwili wa mwanadamu. Jizoeze kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku kwa ajili ya afya ya mwili wako.

Je una maoni gani kuhusu makala hii? Je wewe huwa unakunywa maziwa? Tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe na wengine. Karibu pia ufuatilie ukurasa wetu  wa Facebook ili  ufahamu mengi zaidi.

4.3 12 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

22 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Joseph Sima
Joseph Sima
6 years ago

Asanteni sana kwa makala nzuri nimeelimika sana.

jane
jane
5 years ago

Join the discussion…want to gain wait what should i do?

Kornelio Maanga
Reply to  jane
5 years ago

Nashukuru sana kwa kutembelea blog yetu ya Fahamuhili; karibu tena.

Lilla
Lilla
4 years ago

Je kuna madhara endapo utakunywa maziwa ambayo hayajachemshwa naomba msaada kwa hilo

Kornelio Maanga
Reply to  Lilla
4 years ago

Ndiyo; unaweza kupata maambukizi ya magonjwa yanayosababishwa na bakteria wabaya wanaopatikana kwenye maziwa ambayo hayajachemshwa. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Eva sospeter
Eva sospeter
4 years ago

Asant sana nme elewa faida zote ulizoelezea hapo kuusu unywaji wa maziwa…sasa swali langu lipo hapa napenda kunywa maziwa sana ila kuna point moja hap inasema hupunguza uzito..na wakat mm nataka niongez uzito so naweza endelea kunywa na isiwe na shida yoyote??

Anderson makame
Anderson makame
3 years ago

Nataka kufahamu faida ya matundamwirini

Kornelio Maanga
Reply to  Anderson makame
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; tutaandaa makala kuhusu faida za matunda; karibu sana Fahamuhili.com

Felix Emmanuely
Felix Emmanuely
3 years ago

Je maziwa ya unga nayo yana faida kama hizi?

Kornelio Maanga
Reply to  Felix Emmanuely
2 years ago

Ndiyo ingawa virutubisho vyake vimepungua na kemikali za utunzaji zimeongezwa. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Six saimon
Six saimon
3 years ago

Ahsante sana doctor

Peter
Peter
1 year ago

Nimegundua kitu hapa

Ken dinyo
Ken dinyo
1 year ago

Maziwa yanatajwa kua nikinywaji kinacho punguza mafuta mwilini nikweli au

Shiwa sagaika
Shiwa sagaika
1 year ago

Naomba kujua faida za maziwa freshi na maziwa mtindi it

Epimarkproner
Epimarkproner
1 year ago

Natoa shukrani kwa wale walio amua kuandika nyakara hii ya kujua maarifa ya faida ya maziwa

Kornelio Maanga
Reply to  Epimarkproner
7 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Antony claudy
Antony claudy
1 year ago

Merits of milk

Mpagama
Mpagama
1 year ago

Sawa Apo nimeelewa vzl Sana faida za maziwa

mfaume yusufu
mfaume yusufu
9 months ago

ahsante kwa faida zilizo tolewa nauliza swali

1_je yapo madhara hupatikana katika kutumia maziwa kwa sisi wa kiume?
2_yafaa mtu kuamua kua chakula chake kwa mchana kuwa ni maziwa?
*AHSANTE*

Claire
Claire
7 months ago

Asanteni kwa faida za unywaji wa maziwa . Je hasara ziko wapi??

Kornelio Maanga
Reply to  Claire
7 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; tutaandaa makala kuhusu hasara. Karibu sana Fahamuhili.com

22
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x