Kornelio Maanga, Author at Fahamu Hili
Tuesday, March 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Author: Kornelio Maanga

Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Mambo 10 ya Kuzingatia ili Kutoa Huduma Nzuri kwa Wateja

Mambo 10 ya Kuzingatia ili Kutoa Huduma Nzuri kwa Wateja

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Changamoto ya huduma duni kwa wateja imekuwa kubwa sana kwenye biashara nyingi za kiafrika. Watoa huduma wengi hawajui na hawataki  kufahamu umuhimu wa kutoa huduma nzuri kwa wateja. Kwenye biashara na huduma nyingi mteja huchukuliwa kama kitu kisicho na nafasi wala umuhimu wowote. Lakini ukweli ni kuwa mteja ni msingi muhimu sana katika kufanikiwa kwa huduma au biashara yoyote ile. Kumbuka biashara yoyote isiyozingatia kutoa huduma nzuri kwa wateja wake itapoteza wateja na hatimaye itakufa. Kwa kutambua umuhimu wa kutoa huduma nzuri kwa wateja karibu nikushirikishe mambo 10 ambayo unapaswa kuyazingatia ili kutoa huduma nzuri. 1. Elewa hitaji la mteja Kamwe huwezi kumhudumia mteja vizuri bila kufahamu hitaji lake. Mara mteja anapofika katika biashara yako hakikisha unafa...
Mbinu 7 za Kulinda Biashara Yako Dhidi ya Athari za Corona (COVID 19)

Mbinu 7 za Kulinda Biashara Yako Dhidi ya Athari za Corona (COVID 19)

Biashara na Uchumi
Ni wazi kuwa dunia nzima inapitia msimu mpya baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa homa ya mapafu wa Corona ulioibuka mnamo mwaka 2019 (COVID 19). Pasipo shaka sekta na taasisi mbalimbali zimeshuhudia mabadiliko makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa hayakutegemewa wala hazikujiandaa kwa mabadiliko hayo. Moja ya sekta iliyoathiriwa na inaendelea kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko yaliyoletwa na Corona ni biashara; biashara nyingi zimeporomoka, nyingine zimekufa na wakati nyingine zikijikuta katika wakati mgumu wa kujiendesha kwa utamaduni wake uliozoeleka. Karibu nikushirikishe mbinu 7 ambazo ikiwa utazitekeleza kikamilifu basi kwa kiasi kikubwa utaweza kukabili athari zitokanazo na ugonjwa wa Corona  (COVID 19) kwenye biashara. 1. Punguza matumizi yasiyo ya lazima Kutoka...
Athari 5 za Kukopesha Pesa na Bidhaa kwa Wateja

Athari 5 za Kukopesha Pesa na Bidhaa kwa Wateja

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Katika jaamii zetu za kiafrika suala la mikopo ya bidhaa au fedha kutoka kwenye biashara kwenda kwa wateja limezoeleka sana. Ingawa jambo hili linaweza kuwa na manufaa kwa upande fulani, hata hivyo kutokana na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu wengi jambo hili limekuwa na athari nyingi kuliko faida. Inawezekana umekuwa ukiwakopesha wateja wako wa maana sana, au umekuwa ukitumia mikopo kama njia ya kuuza huduma au bidhaa zako, lakini karibu nikushirikishe athari tano za mikopo hiyo. 1. Kumpoteza mteja Kuna usemi usemao kumkopesha mteja ni kumfukuza. Nimesikia mara kadhaa wafanyabiashara wakisema tangu ni mkopeshe haji tena dukani kwangu, au tangu nimkopeshe anapita mbali tu. Mara nyingi mteja akishakopeshwa pesa au bidhaa haji tena kwenye biashara husika ili kukwepa ku...
Mambo 8 ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Eneo la Kufanyia Biashara

Mambo 8 ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Eneo la Kufanyia Biashara

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Je ni maeneo gani sahihi ya kufungua biashara ili uweze kupata wateja, kukuza biashara na kutengeneza faida. Je, kila eneo linafaa kwa biashara? Hivyo basi, ili tuweze kujibu maswali haya vyema, hatuna budi kuangalia mambo 8 muhimu ya kuzingatia wakati wakuchagua eneo la kufanyia biashara ili ipate soko na kukua kila wakati. 1. Ushindani Ushindani ni jambo muhimu sana linaloweza kufanya eneo la biashara kuwa zuri au baya. Hebu fikiri mtu mchanga kabisa anaanzisha biashara mahali ambapo tayari kuna wafanyabiashara wengine wakubwa wenye uzoefu, mtaji, vitendeakazi au hata mtandao mzuri wa washirika. Bila shaka, itakuwa vigumu sana kwa mtu huyo kukua kibiashara. Ni lazima mtu apime na achague eneo amabalo lina ushindani ambao anaweza kuumudu na kukua. 2. Uhusiano kati ya biashar...
Zifahamu Aina 9 za Wateja ili Ukuze Biashara Yako

Zifahamu Aina 9 za Wateja ili Ukuze Biashara Yako

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Mteja ni nani? Mteja ni mtu yeyote anayenunua bidhaa au huduma inayotolewa na biashara fulani. Mteja ni mtu muhimu sana katika biashara yoyote. Lengo la kuanzisha biashara ni kupata wateja watakaonunua bidhaa au  huduma yako. Biashara yoyote isipopata wateja bora na wa uhakika, ni wazi kuwa haiwezi kufanikiwa; itakufa tu. Soma pia: Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa Kutokana na kukosa uelewa, wafanyabiashara wengi hawawafahamu wateja vyema, hivyo kutokuwamudu vyema; jambo ambalo huwakwamisha kufikia malengo yao. Ikiwa wewe ni mfanya biashara tayari au unataka kuanza kufanya biashara, karibu nikushirikishe aina 9 za wateja unazoweza kuzitumia kukuza biashara yako. 1. Wateja wapya Hawa ni wateja ambao huja kwenye biashara yako kwa mara ya kwanza, mnaweza kuwa m...
Fahamu Njia 8 Unazoweza Kuzitumia ili Kupata Mtaji

Fahamu Njia 8 Unazoweza Kuzitumia ili Kupata Mtaji

Ujasiriamali
Nifanyeje nipate mtaji? Nina wazo zuri lakini sina mtaji? Haya ni maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa sana na wasomaji wa Fahamuhili.com, pamoja na watu wengi ninaokutana nao kwenye maisha ya kila siku. Kutokana na sababu hii, nimeona ni vyema niandae makala ambayo itajibu maswali ya wasomaji wangu pamoja na wale wote wenye maswali kama haya. Ingawa mtaji siyo kigezo pekee cha kufanikiwa kwenye biashara au mradi unaoufanya, mtaji unabaki kuwa kiungo muhimu sana katika kutekeleza wazo fulani au mradi kwa ufanisi. Kwa kuwa watu wengi huanzisha miradi au biashara kwa lengo la kupata pesa, huwa vigumu sana kuwa na pesa za kutosha kuanza utekelezaji wa wazo hilo. Karibu ufuatilie makala hii kwa karibu nikushirikishe njia 8 unazoweza kuzitumia ili kupata mtaji wa kutekeleza wazo la...
Mambo 10 ya Kujifunza Kama Mjasiriamali Kutokana na Anguko la Nokia

Mambo 10 ya Kujifunza Kama Mjasiriamali Kutokana na Anguko la Nokia

Biashara na Uchumi, Ujasiriamali
Kama wewe uliwahi kidogo kwenye ulimwengu wa simu za mkononi, utakuwa umetumia au hata kusikia juu ya uimara, umaarufu na ubora wa simu za Nokia. Mnamo mwaka 1998 Nokia ilikuwa ndiyo kampuni bora ya kutengeneza na kuuza simu za mkononi duniani kote. Faida ya kampuni ya Nokia ilikwea kutoka dola za kimarekani bilioni 1 mwaka 1995 hadi dola bilioni 4 mwaka 1999; huku simu yake ya Nokia 1100 ikiwa ndiyo simu iliyowahi kuuzwa zaidi duniani. Nokia 1100 (Chanzo cha Picha: marketplace.citify.ca) Pamoja na mafanikio haya Nokia iliyoyapata, kwa kipindi kisichozidi miaka sita kuanzia mwaka 2007, hisa za Nokia ziliporomoka kwa asilimia 90.Kwa kutambua nafasi Nokia iliyokuwa nayo ikilinganishwa na anguko kubwa lililoipata, ni wazi kuwa kuna mengi ya kujifunza kama mjasiriamali au kiongoz...
Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia ili Kupunguza Gharama za Ujenzi

Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia ili Kupunguza Gharama za Ujenzi

Nyumba na Makazi
Ikiwa unajenga nyumba mpya au unafanya ukarabati wa nyumba ya zamani, suala la kupunguza gharama za ujenzi ni muhimu sana. Watu wengi wamejikuta katika hali ngumu ya kifedha au hata kukwama katika ujenzi kutokana na kushindwa kuweka mikakati mizuri ya kupunguza gharama za ujenzi. Kwa kutambua umuhimu wa ujezi, na kwa kutambua kuwa ujenzi ni jambo linalogharimu fedha nyingi; nimeona ni vyema nikushirikishe mambo 10 muhimu unayoweza kuyazingatia ili uweze kupunguza gharama za ujenzi. 1. Chagua kiwanja bora Uchaguzi sahihi wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi ni jambo muhimu sana. Watu wengi hujikuta wakitumbukia kwenye gharama kubwa za ujenzi kutokana na uchaguzi duni wa kiwanja. Hebufikiri ukinunua kiwanja sehemu ambayo ni mkondo wa maji au udongo wake unatitia; hili litakulaz...
Fahamu Tabia 10 za Watu Wenye Wivu Ili Uwaepuke

Fahamu Tabia 10 za Watu Wenye Wivu Ili Uwaepuke

Maendeleo Binafsi
Mara mtu apatapo mafanikio mambo mengi hutokea au hubadilika. Moja kati ya mambo ambayo hutokea ni mabadiliko kwa watu wanao mzunguka mtu huyo. Wengine humpenda, wengine humheshimu, wengine humchukia au hata kumwonea wivu. Wivu umekuwa ukitesa na kurudisha maendeleo ya watu nyuma hasa wale ambao ndio huwa na wivu huo mioyoni mwao. Kwa kuwa wivu hauwaathiri wale walio nao pekee, ni vyema nawe ukafahamu tabia za watu wenye wivu ili uwaepuke wasije wakakuathiri kwa kukurudisha nyuma katika hatua zako za maendeleo. 1. Hawastaajabishwi na mafanikio ya wengine Moja kati ya tabia kubwa ya watu wenye wivu ni kutostaajabishwa na mafanikio ya wengine. Wao hata wasikie jambo zuri au kubwa kiasi gani la mtu mwingine wao hujifanya kuliona kama la kawaida tu. Unaweza kusikia hata wakisem...
Mbinu 7 za Kukurahisishia Kusoma Vitabu Unapokuwa na Shughuli Nyingi

Mbinu 7 za Kukurahisishia Kusoma Vitabu Unapokuwa na Shughuli Nyingi

Tija
Kama nilivyoeleza kwenye makala mbalimbali kuwa kusoma vitabu kuna manufaa mengi sana ambayo kila mtu mwenye maono anapaswa kuyapata. Vitabu hubeba maarifa kemkem ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kukusaidia kubadili maisha yako. Soma pia: Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu Hata hivyo bado watu wengi wanashindwa kusoma vitabu jinsi ipasavyo. Ikiwa unapenda kusoma vitabu lakini una shughuli nyingi, basi karibu nikushirikishe mbinu kadhaa zitakazo kuwezesha kusoma vitabu kwa urahisi. 1. Tumia simu yako Karibu kila mtu leo ana simu ya kisasa ya mkononi (smartphone), hata hivyo bado watu wengi hawafahamu nguvu au matumizi adhimu yanayopatikana kwenye simu hizo. Ni ukweli usiopingika kuwa ulimwengu wa kutumia simu kama kifaa cha kupiga na kupokea simu pamoj...