
Faida 7 za Kuwa na Uvumilivu Unazotakiwa Kuzifahamu
Maisha yana milima na mabonde, kipindi cha raha na shida. Katika kipindi cha shida au wakati mtu anapokutana na changamoto swala la uvumilivu linahitajika sana, tena sana. Kukosa uvumilivu kumewafanya wengi kushindwa kufanya maamuzi sahihi na kujikuta wakitumbukia kwenye shida zaidi. Haijalishi unapitia magumu mengi kiasi gani, kuvumilia ni lazima. Ikiwa unataka kujifunza faida au umuhimu wa uvumilivu, basi fahamu faida 7 za uvumilivu katika maisha yako.
1. Hukuwezesha kufanya maamuzi sahihi
Ndani ya uvumilivu kuna subira, ikumbukwe kuwa wahenga walisema subira yavuta heri. Hii ina maana kuwa kufanya maamuzi mara ukutanapo na changamoto kunaweza kukusababishia kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Kwa mfano hebu fikiri mtu ameachwa na mchumba wake ghafla naye mara moja anataka kupa...