Mpiga Ngoma Maarufu wa Mtaani Anayetengeneza Midundo kwa Kutumia Ndoo - Fahamu Hili
Friday, November 16Maarifa Bila Kikomo

Mpiga Ngoma Maarufu wa Mtaani Anayetengeneza Midundo kwa Kutumia Ndoo

Washirikishe Wengine Makala Hii:
Gordo
Mpiga Ngoma Gordo.

Nani anahitaji ngoma wakati anaweza kutumia ndoo kutengeneza sauti na midundo ya pekee? Mpiga ngoma wa mtaani kule Australia aitwaye Gordo, ambaye awali alisoma nchini Japan, anafahamu kuwa inawezekana kutengeneza muziki kutoka kwenye kila kitu bila tatizo lolote.

Akiwa mwenye nguvu, nia na shauku, Gordo anaonekana akitumia ndoo, vijiti vya kupigia ngoma na miguu yake kutengeneza midundo mizuri ya ngoma.

Ikiwa hana shughuli na wasanii wengine, mwaliko kwenye tukio au sherehe basi utamkuta Gordo akiwa kwenye mitaa ya Sydney akidhihirisha kipaji chake katika jamii.

Watu wengi huvutiwa na kipaji chake na hata kumzawadia pesa na vitu vingine; naamini hata wewe utakapotazama video zake hapa chini, hakika atakuvutia na kukuhamasisha sana. Karibu!

Gordo akipiga ngoma mtaani.

Mwendelezo wa kazi zake za mtaani.

Gordo akitoa maelekezo jinsi ya kupiga ngoma kwa ndoo.

Unaweza kutazama video zake zaidi kupitia chaneli yake ya YouTube: Gordo Drummer

Neno la Mwisho:

Ni wazi kuwa kuthubutu na nia ya ndani huwezesha kila kitu kufanikiwa. Gordo ameonyesha uthubutu mkubwa katika kudhihirisha kipaji chake bila kukubali kukwamishwa na mazingira au mtu yeyote. Ni ukweli usiopingika kwamba wengi wangeona aibu kupiga ngoma za ndoo au hata kupiga ngoma mtaani kama Gordo.

Inuka leo, tekeleza maono na ndoto zako, dhihirisha kipaji chako bila woga wala kisingizio chochote, nawe utafanikiwa.

Je umefurahia video hizi? Je una maoni gani? Je umehamasika kunoa kipaji chako? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini. Usisahau pia kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook.

ZINAZOHUSIANA

Kornel ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Tafadhali tuandikie maoni yako:

avatar