
Athari 5 za Kukopesha Pesa na Bidhaa kwa Wateja
Katika jaamii zetu za kiafrika suala la mikopo ya bidhaa au fedha kutoka kwenye biashara kwenda kwa wateja limezoeleka sana. Ingawa jambo hili linaweza kuwa na manufaa kwa upande fulani, hata hivyo kutokana na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu wengi jambo hili limekuwa na athari nyingi kuliko faida. Inawezekana umekuwa ukiwakopesha wateja wako wa maana sana, au umekuwa ukitumia mikopo kama njia ya kuuza huduma au bidhaa zako, lakini karibu nikushirikishe athari tano za mikopo hiyo. 1. Kumpoteza mteja Kuna usemi usemao kumkopesha mteja ni kumfukuza. Nimesikia mara kadhaa wafanyabiashara wakisema tangu ni mkopeshe haji tena dukani kwangu, au tangu nimkopeshe anapita mbali tu. Mara nyingi mteja akishakopeshwa pesa au bidhaa haji tena kwenye biashara husika ili kukwepa ku...