Usalama wa Msingi wa Kompyuta: Jinsi ya Kujilinda na Virusi, Wadukuzi na Wezi
Watu wengi hufikiri kuwa usalama wa kompyuta ni swala gumu lenye changamoto kubwa. Inaweza kuwa hivyo kama hukuchukua hatua sahihi mapema. Katika makala hii utafahamu hatua tano muhimu ambazo zitakuwezesha kujilinda na virusi, wadukuzi na wezi katika kifaa chako cha kielektroniki.
1. Wezesha automatiki sasishi (automatic updates)
Programu mbalimbali za kompyuta hutoa masasisho (updates) mara kwa mara ili kuziba mianya mbalimbali hasa ya kiusalama iliyobainika katika matoleo ya awali. Program kama Microsoft Window, Mozilla na Chrome ni baadhi ya programu muhimu zinazohitajika kusasishwa kwa wakati. Hivi leo programu mbalimbali huja na usasishaji wa automatiki lakini watu wengi hupenda kuuzima usasishaji huu bila kuzingatia umuhimu wake wa kiusalama. Hivyo basi, ili kuwa salama zing...