
Kampuni 7 za China Zilizofanikiwa Sana Barani Afrika (2017)
China ni moja kati ya nchi zenye makampuni mengi yaliyowekeza barani Afrika. Takwimu zinaeleza kuwa zaidi ya kampuni 10,000 za kichina zipo barani Afrika kwa sasa. Inaelezwa kuwa kampuni hizo zimefanikiwa sana na kujipatia faida kubwa kwa muda mfupi. Takwimu hizo zinaeleza kuwa robo ya kampuni hizo zilirudisha mtaji wake ndani ya miezi 12, wakati asilimia 50 zilitumia takriban miaka mitatu au pungufu kurudisha mtaji wake. Fahamuhili tunapenda kukupa maarifa, hivyo fahamu kampuni 7 za China zilizofanikiwa sana barani Afrika kwa mwaka 2017.
1. TECNO
Hii ni kampuni ya kuuza vifaa vya kielektroniki, hasa simu kutoka China. Inaelezwa kuwa kampuni hii imefanikiwa kushika asilimia 40 ya soko katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. Pamoja na ushindani mkubwa kutoka kwa wazalishaj...