
Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia ili Kupunguza Gharama za Ujenzi
Ikiwa unajenga nyumba mpya au unafanya ukarabati wa nyumba ya zamani, suala la kupunguza gharama za ujenzi ni muhimu sana. Watu wengi wamejikuta katika hali ngumu ya kifedha au hata kukwama katika ujenzi kutokana na kushindwa kuweka mikakati mizuri ya kupunguza gharama za ujenzi. Kwa kutambua umuhimu wa ujezi, na kwa kutambua kuwa ujenzi ni jambo linalogharimu fedha nyingi; nimeona ni vyema nikushirikishe mambo 10 muhimu unayoweza kuyazingatia ili uweze kupunguza gharama za ujenzi. 1. Chagua kiwanja bora Uchaguzi sahihi wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi ni jambo muhimu sana. Watu wengi hujikuta wakitumbukia kwenye gharama kubwa za ujenzi kutokana na uchaguzi duni wa kiwanja. Hebufikiri ukinunua kiwanja sehemu ambayo ni mkondo wa maji au udongo wake unatitia; hili litakulaz...