Makosa 8 ya Kuepuka Kabla na Wakati wa Kujenga Nyumba - Fahamu Hili
Friday, June 2Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Makosa 8 ya Kuepuka Kabla na Wakati wa Kujenga Nyumba

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Nyumba Nzuri

Nyumba ni hitaji muhimu kwa watu wote. Kila mmoja anatamani na ana ndoto za kununua au kujenga nyumba nzuri na ya kisasa. Ni kweli kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji rasilimali nyingi hasa fedha.

Pamoja na gharama hizi za ujenzi wa nyumba bado watu wengi wamekuwa wakishindwa kupata nyumba nzuri huku wakiwa tayari wamepoteza kiasi kikubwa cha pesa. Ni wazi kuwa yapo makosa mbalimbali yanayosababisha hali hii yakiwemo yale ya ukosefu wa elimu pamoja na uzembe wa aina mbalimbali.

Karibu ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu makosa 8 unayoweza kuyaepuka wakati wa kujenga nyumba ili hatimaye uwe na nyumba bora.

1. Kutozingatia kanuni za kununua kiwanja

Watu wengi hawafahamu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wanaponunua kiwanja. Hivyo hujikuta wakiingia katika matatizo mbalimbali kama vile kuvunjiwa nyumba zao, kujenga kwenye maeneo mabaya kama matindiga na mikondo ya maji. Ni muhimu kuhakikisha mambo yafuatayo kabla na wakati wa kutafuta kiwanja cha kujenga nyumba:

  • Kiwanja hakina umiliki zaidi ya mtu mmoja
  • Kiwanja hakina mgogoro wa kisheria
  • Kiwanja hakiko kwenye hifadhi ya barabara au mazingira
  • Kiwanja kinafaa kwa ujenzi (Siyo tindiga, eneo la magadi, eneo la maporomoko ya ardhi au mkondo wa maji)

Soma pia: Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Kiwanja au Ardhi.

Ukizingatia haya utaweza kupata kiwanja kizuri kwa ajili ya kujenga nyumba bora kwa ajili ya matumizi yako.

2. Uchaguzi duni wa ramani

Mara nyingi mtu humwita fundi na kumwambia kuwa “nataka unijengee nyumba ya vyumba vitatu”. Fundi anapouliza ramani yako iko wapi wao husema we angalia tu nzuri alimradi iwe ya vyumba vitatu. Hili ni kosa kubwa sana kwani husababisha watu wengi kujengewa nyumba ambazo hawazipendi.

Ramani nzuri kwa fundi inaweza isiwe nzuri kwako na familia yako. Zingatia uchaguzi wa ramani kwa makini kulingana na wewe unavyopenda, hili litakufanya pia upende nyumba itakayojengwa.

Ramani
Ramani mbaya.

3. Kutokufanya makadirio sahihi

Ni wazi kuwa umeona nyumba nyingi zikianzwa lakini hazimaliziki. Hili kwa kiasi kikubwa linatokana na kufanya makadirio na maandalizi duni kabla ya kuanza kujenga. Ujenzi wa nyumba unahitaji maandalizi mazuri hasa kifedha. Ni muhimu kujiandaa vyema kabla ya kuanza ujenzi ili usikwamie njiani.

Mambo unayoweza kufanya:

  • Weka makadirio ya gharama za ujenzi ili angalau uandae kiasi fulani cha pesa.
  • Nunua baadhi ya vifaa kabla. Unaweza kununua mchanga, mawe, kokoto, nondo, mabati n.k. Ili kupunguza matumizi ya pesa wakati wa ujenzi.
  • Weka mipango ya kutunza mahitaji yako mengine ya pesa kabla ya kuanza ujenzi. Kwa mfano ada za shule, kodi mbalimbali, chakula n.k.
  • Punguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kabla na wakati wa ujenzi. Ikumbukwe kuwa pesa nyingi zitahitajika kwenye ujenzi.

Soma pia: Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema.

4. Kutokubainisha mahitaji

Mahitaji ya nyumba hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Hivyo ni vyema ukabainisha mahitaji yako kwa nyumba husika. Nimeshuhudia watu wakijenga nyumba na kuzivunja ua kuzifanyia marekebisho kila mwaka kutokana na kutobainisha mahitaji yao mapema.

Kurekebisha au kuvunja na kujenga upya nyumba yako kutakupotezea kiasi kikubwa sana cha pesa. Kwa mfano wengi hurekebisha nyumba zao ili kuongeza vitu kama vile jiko, choo na bafu, milango, madirisha n.k. ambavyo wangepanga mapema wangekuwa wameviweka mwanzoni.

5. Kutokuwaza mbeleni

Ni vyema kuwaza mbeleni kwani nyumba ni kitu utakachokitumia muda mrefu. Ni vyema ukafahamu vitu na mahitaji utakayoyataka kwenye nyumba yako kwa siku za mbeleni. Hili litakuwezesha kujenga nyumba utakayoitumia na kuifurahia kwa muda mrefu zaidi.

Ni vyema pia ukawaza kuweka miundombinu ya kisasa kama vile umeme, simu (intercom), nyaya za televisheni, Kiyoyozi, na hata Data. Hata kama huna pesa za kuweka mambo haya unaweza kubuni nyumba ambayo baadaye itaruhusu miundombinu hii.

Nyumba
Nyumba ya Kisasa

Soma pia: Njia 8 Rahisi za Kupunguza Matumizi ya Umeme.

6. Kutumia mafundi duni

Wengi hupenda kuokoa gharama kwa kutumia mafundi wenye uwezo mdogo ili wawalipe kwa bei nafuu. Ni wazi kuwa rahisi inaumiza. Jiande vyema kabla ya ujenzi ili uweze kuitendea haki nyumba yako kwa kutumia mafundi bora wanaoimudu kazi yao vyema. Kutumia mafundi bora kutakufanya kupata pia kazi yenye ubora.

Nhazi
Ngazi zilizokosewa.

7. Kupuuza kanuni muhimu za ujenzi

Ujenzi una kanuni zake mbalimbali ambazo ni vyema zikazingatiwa. Kutokana na uelewa mdogo, watu wengi hawazingatii kanuni muhimu za ujenzi kama vile kumwagilia maji yakutosha pamoja na kujenga nyumba kulingana na muda.

Nimeshuhudia nyumba nyingi zikivunjika kutokana na kujengwa haraka haraka bila kutoa muda wa kutosha kwa nyumba kukomaa na kustahimili uzito. Pia nimeona watu wakipuuzia umuhimu wa kunyesha sehemu iliyojegwa kwa maji mengi; ni muhimu kunyesha vyema eneo lililojengwa kwani “uimara wa saruji ni maji”; unaweza kunyesha angalau kwa siku saba asubuhi na jioni.

Nyumba iliyoporomoka
Nyumba iliyoporomoka kutokana na kupuuza kanuni za ujenzi.

8. Matumizi ya vifaa duni

Kama nilivyoeleza katika maelezo yaliyotangulia, uhaba wa fedha huwafanya watu wengi kufanya kazi duni. Hivi leo kuna vifaa mbalimbali vya ujenzi, lakini si vyote ni bora. Kwa mfano, hakuna haja ya kununua kitasa kinachovunjika baada ya mwezi au vigae vinavyofubaa. Kwa kufanya hivi utapoteza pesa nyingi kwa kununua vifaa hivyo mara kwa mara. Jibane, jipange ufanye kitu cha uhakika.

Soma pia: Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia ili Kupunguza Gharama za Ujenzi

Hitimisho

Ni wazi kuwa ujenzi wa nyumba ni shunguli pevu inayohitaji kutulia, moyo na maandalizi stahiki. Hakuna kitu kinachoshinda nia na mipango mizuri. Naamini kwa kuyaepuka makosa tajwa hapo juu utaweza kujenga nyumba bora, salama na ya kisasa kabisa.

Je umeshajenga nyumba yako? Ulipata changamoto gani na ulizitatuaje? Tafadhali tushirikishe kwa kutoa maoni yako hapo chini. Pia usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook pamoja na kuwashirikisha wengine makala hii.

3.9 13 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
guest

24 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Hafidh hassan
Hafidh hassan
5 years ago

Maelezo yamenisaidia
Asante sana

jeff
jeff
4 years ago

Kiufup nimefurah kwa maelekezo haya ingawa bado sina hata kiwanja nahc haitakuwa tabu kkukipata nikijiweka sawa

Edmund Mayer
Edmund Mayer
4 years ago

Asante ndg Kornel. Ninafurahia msaada wako! Nitatumia maarifa hayo kuboresha maisha yangu na ya wengine.

John
John
4 years ago

Iko vizuri, nimeipenda

Erick kabwe
Erick kabwe
4 years ago

Nimeshukuru sana Mahana Na Mimi mwaka Huuuu Ndo Bado Nimehanza kujenga nyumbani kigoma kweli Nimepata ubunifu zaidi nakujifunza zaidi Asante sana Na Mungu Akubariki sana

Fred
Fred
3 years ago

Thank you kaka maelezo yamekuwa msaada sana kwangu.

aloyce
aloyce
3 years ago

thankd sana kwa kueza kunifunguwa macho hasa katika sector ya umwailiaji maji huu kweli weng hupuuzia

Mwatima
Mwatima
3 years ago

Mada nzuri sana mkuu. Nimejifuna vitu

Naomy Lema
Naomy Lema
3 years ago

Asante kwa maelekezo mazuri kwani nataraji kuanza ujenzi mwakani naamini yatanisaidia

Mpepo Fd
Mpepo Fd
3 years ago

Nimefurahi nimejifunza mengi mungu akubariki sana,

Mecksony kangusi
Mecksony kangusi
2 years ago

Asante Sana kwa ushauri wenu

Mika Mambo
Mika Mambo
11 months ago

Asante kwa maelezo mazuri ila yamesaiidia sana kuelewa nn cha kufanya, nina shida binafsi kama inawezekana tuwasiliane kwa email yangu iyo.

24
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x