Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema - Fahamu Hili
Friday, April 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema

Washirikishe Wengine Makala Hii:

pesa

Je, huwa unajisikia vibaya unapohitaji pesa kwa ajili ya matumizi yako lakini unajikuta mifuko yako ni mitupu? Haijalishi unapata pesa kiasi gani, swala la matumizi mazuri ya pesa ni jambo muhimu; hili litakuwezesha kuwa na kitu wakati wa uhitaji.

Watu wengi wanapata pesa lakini si wote wanaoweza kuzitumia vyema. Wengi hujikuta wakizitumia kwenye mambo na mipango ambayo mwishoni haiwaletei tija katika maisha yao.

Naamini ungependa kuwa na matumizi mazuri ya pesa; sasa fahamu njia 10 zitakazokuwezesha kutumia pesa vyema.

1. Weka bajeti

Ni rahisi kusikia watu wakilalamikia bajeti za serekali na kuzikosoa lakini wao wenyewe hawana bajeti zao binafsi. Unawezaje kukosoa bajeti ya serekali wakati ya kwako mwenyewe imekushinda? Fikiri tofauti; tambua umuhimu na jinsi ya kujiwekea bajeti. Bajeti yako binafsi itakuwezesha kufahamu mapato yako, mambo gani muhimu unayotakiwa kuyafanya na yatakugharimu kiasi gani cha pesa. Kwa kufanya hivi utaweza kutafuta na kutumia pesa kulingana na bajeti uliyojiwekea na kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu.

2. Panga manunuzi kabla

Ni muhimu kupanga manunuzi yako kabla ya kwenda sokoni au dukani. Hili litakuwezesha kubainisha nini unachotakiwa kununua na kwa gharama gani. Unapokwenda sokoni au dukani bila kupanga manunuzi yako ni rahisi ukanunua vitu ambavyo hukuvipanga. Unaweza kuorodhesha vitu katika kipande kidogo cha karatasi pamoja na bei zake ili uwe ni mwongozo wako katika manunuzi.

3. Weka vipaumbele

Kuna mahitaji mengi kwenye maisha ya mtu; lakini kuna yaliyo muhimu zaidi kuliko mengine. Jifunze kubainisha mambo ya muhimu zaidi ili uanze kuyatengea pesa kwanza. Kwa mfano maswala kama vile eilimu, uwekezaji, kodi ya nyumba, chakula, ni baadhi tu ya mambo muhimu kuliko gari, pombe, simu pamoja na mambo mengine ya anasa. Ukijifunza kuwa na mtazamo wa kutambua vipaumbele utaweza kutenga na kutumia pesa kwenye mambo ya muhimu kwanza.

4. Tumia kidogo kuliko unachopata

Ni rahisi kutumia kuliko kutafuta; hivyo si jambo la kustaajabisha ukajikuta unapata elfu tano kwa siku lakini unatumia elfu saba. Maana yake hapa unatengeneza deni mahali la shilingi elfu mbili kila siku. Inawezekana unakula akiba au faida katika kile unachokifanya. Jifunze kutumia kidogo kuliko kile unachokipata ili uweze kutunza pesa kwa ajili ya wakati wa uhitaji.

5. Tumia vitu (huduma) vyema

Kuna huduma kadha wa kadha tunazozihitaji kila siku katika maisha yetu kama vile maji, umeme, gesi, simu n.k. Mara nyingi watu hushindwa kutumia huduma au vitu hivi vyema na kujikuta wakijiongezea gharama za maisha zisizokuwa na sababu ya msingi. Mambo unayoweza kuzingatia katika swala hili:

  • Epuka tabia kama vile kuacha taa zikiwa zimewashwa hata wakati wa mchana bila sababu. Punguza matumizi ya pasi, redio na hata televisheni. Pia unaweza kununua taa zinazookoa umeme yaani energy servers.

Soma pia: Njia 8 Rahisi za Kupunguza Matumizi ya Umeme.

  • Unaweza ukaokoa maji kwa kutumia maji ya mvua au toka chanzo kingine badala ya kutumia maji ya bomba kwa kila kitu.
  • Punguza matumizi ya gesi kwa kuzima jiko pale lisipokuwa na uhitaji. Hakuna haja ya kupasha maji moto kila wakati huku unaweza kuogea maji ya baridi au uvuguvugu.
  • Epuka kupiga simu zisizokuwa na ulazima kwani kwa kufanya hivi unapoteza pesa bila sababu. Jiunge kwenye vifurushi (bundles) vya muda mrefu kuliko vya siku moja ili uweze kupata muda wa kutosha kutumia vyema muda wako wa maongezi.

6. Tafuta punguzo

Mara nyingi vitu huuzwa kwa punguzo, hivyo ni vyema ukanunua vitu kwa punguzo kuliko kununua kitu katika bei halisi ili kupuguza gharama. Naamini unafahamu kuwa yapo maduka yanayouza aina fulani ya shati kwa shilingi laki tatu, lakini shati hilo hilo linauzwa kwa shilingi elfu kumi na tano duka jingine. Sasa kwanini usinunue kwenye hili duka la pili linalouza shati kwa shilingi elfu kumi na tano? Epuka sifa na ufahari usiokuwa na sababu, tafuta na nunua vitu kwa punguzo ili kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu.

7. Linda afya yako

Kutokana na watu kutojali wala kufahamu umuhimu wa kuwa na afya njema, wengi wamekuwa wakitumia gharama zisizokuwa na sababu kwenye matibabu. Kuna hatua kadhaa unazoweza kuzitumia kujilinda na maradhi yasiyokuwa na sababu kama vile kula chakula bora pamoja na kuzingatia kanuni za afya kama vile usafi. Chukua hatua mapema ili usipoteze pesa zako hosipitalini kila siku kutibu maradhi ya tumbo au malaria ambayo ungeweza kuyazuia.

8. Acha tabia badhirifu

Kuna tabia kadha wa kadha ambazo watu wengi hawazijui kama ni moja kati ya tabia badhirifu. Tabia kama vile Kuvuta sigara, pombe, unywaji wa soda, ulaji wa pipi, kulipia michezo ya kompyuta, kukodisha filamu, kamari n.k ni baadhi tu ya tabia badhirifu. Unaweza kuepuka tabia hizi na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinapotea bila sababu.

9. Rekodi matumizi yako

Kwenye suala la kutunza kumbukumbu binafsi hasa za kipesa ni suala gumu kwa watu wengi. Lakini ni vyema ukajifuna kutunza kumbukumbu za matumizi yako ili hatimaye uweze kufahamu jinsi ulivyotumia kipato chako. Kwa kufanya hivi utaweza kubaini ni wapi ambapo hukutumia pesa zako vyema na utaweza kujirekebisha wakati mwingine.

10. Weka akiba

Mara ngingi watu hujitetea kuwa hawawezi kuweka akiba kwa kuwa hawana kipato kikubwa. Ukweli ni kuwa kuweka akiba siyo kuwa na kipato kikubwa bali ni maamuzi pekee. Fahamu kuwa kuna wakati chanzo chako cha kipato cha sasa kinaweza kukauka; hivyo kuwa na akiba kutakuwezesha kukidhi mahitaji yako kwa wakati ambao huna kipato cha uhakika au cha kutosha. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:

  • Andaa bahasha nne (1. Kuwekeza, 2. Matumizi ya lazima, 3. Akiba 4. (Jambo lingine muhimu linalohitaji pesa)
  • Gawa kila unachokipata na kukiweka kwenye bahasha hizo nne. Kumbuka bahasha zote zinatakiwa kupata mgao; bahasha ya nne inaweza kuwa chochote kulingana na matumizi yako, Mf. Ada za Shule, Malipo ya Bima, n.k.
  • Tumia pesa kulingana na bahasha. Bahasha ya akiba ni kwa ajili ya baadaye. Pia bahasha ya kuwekeza ni kwa ajili ya miradi na uwekezaji utakaofanya baadaye.

Naamini kwa kufanya hivi utaweza kupangilia pesa zako vyema na hatimaye kujiwekea akiba.

Neno la mwisho: Pesa siyo kila kitu katika hii dunia, lakini ina nafasi kubwa sana. Hivyo ukitaka kuwa na utawala mzuri katika maisha yako ni vyema ukaimarisha misingi ya matumizi yako ya pesa. Epuka tabia za kitoto au za watu wasiokuwa na busara, ambao hula au kutumia kila wanachokipata. Naamini njia hizi 10 zilizoelezwa hapa zitakupa mwanzo mzuri wa matumizi ya pesa.

Je una swali au maoni yoyote kuhusu makala hii? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine. Pia usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3.9 30 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

59 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
masele bundala
masele bundala
4 years ago

naomba ushauri nin mashamba mawili nataka nilikodishe shamba moja miaka 4 nipate mtaji nitakuwa nimefanya vyema

Lulu vero
Lulu vero
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Nimeipenda Hii

george
george
4 years ago

Napenda kujifunza zaid

maulid
maulid
4 years ago

Maelezo mazuri sana brother

Kokugonza Alfred
Kokugonza Alfred
4 years ago

Asante sana kwa elimu yako, nimejifunza vitu vingi sana

Razaki
Razaki
4 years ago

Nimependa hii

E. JACOB
E. JACOB
3 years ago

Ahsante sana kwa elimu hii ya mafanikio juu ya pesa

Joshua
Joshua
3 years ago

Pesa inawezaje kuleta manufaa juu ya matumizi yake

Joshua
Joshua
3 years ago

Jinsi yakuishii kwenye maisha ya utajiri nfo kuna furaha

Leutnat Misana
Leutnat Misana
3 years ago

Asante kwa maelezo mazuri, muhimu na yenye tija ktk kuongeza maarifa

John mlewa
John mlewa
3 years ago

Daah aseh imekaa powa sana hii

Robert
Robert
3 years ago

Njia ni nzuri je kuna namna hata ya kuandaa chati ambayo itakuwa nasehemu ya matumizi akiba na nyingi kama ipo tafadhari naomba kujua

Philbert
Philbert
3 years ago

Yes

Signativer 4rever
Signativer 4rever
3 years ago

Nimependa saaa jinsi ulivyopanga mpangilio mzuri wa fedha,, nimejifunza kitu kutokana na hiii makala

Sephord Saul
Sephord Saul
3 years ago

Asante sana kwa somo hili.
Naomba nitoe ombi kama waweza andaa somo la ”Namna sahihi ya kugawanya pesa unapoipata kuepuka madeni na pia kutimiza malengo fulani”
Barikiweni

Last edited 3 years ago by Sephord Saul
FILI JUMA YELLA
FILI JUMA YELLA
2 years ago

Ahsante kwa elimu nzuri ya fedha hakika nimejifunza na kutambua makosa naamini elimu italeta mabadiriko.

ANNAROSE PETER
ANNAROSE PETER
2 years ago

Asantee kwa ushauri nimejifunza

beryl
beryl
2 years ago

Nashuru sana

Alex Mwanjabala
Alex Mwanjabala
2 years ago

Asante

George Mwemezi
George Mwemezi
2 years ago

Nimeeelewa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kutunza akiba na kutubza helq kwa ajili ya miradi sante sana

Abeid
Abeid
1 year ago

Shukraaani nmejifunza mengi

Peter Issack Kimaro
Peter Issack Kimaro
1 year ago

Njia hiyo ya Bahasha ninaianza kesho Asubuhi najuta kwa kuchelewa kujua njia hii nimekuwa nikipata kipato kikubwa lakini sioni chamaana wapi pesa zinaenda ila njia hii sitaiacha.asante sana kwa elimu yako and God blessing you

julius
julius
1 year ago

Thank

kiliani mbembati
kiliani mbembati
1 year ago

mawazo mazuri broo

ushindiboniphace@gmail.com
ushindiboniphace@gmail.com
1 year ago

kaka iv nikwanini watu wenye pesa Hana uhusiano nzur na maskin Kwa mfano mm nimefanya Kaz Kwa mtu nikinunu kitu Cha saman ananiachixha kaz

Husseni Kasimu
Husseni Kasimu
1 year ago

Hii nimeipenda na pia mmenipa ufahamu ambayo nilikuwa sina

paul karanja
paul karanja
1 year ago

marafiki huwa wanataka kila mmoja kusaidia yule mwingine ni lazima

Evaristo amos
Evaristo amos
1 year ago

Nimependa sana

Mr.Luca
Mr.Luca
1 year ago

Author, I attracted by your writing style, am ego to learn from you

Kempa
Kempa
10 months ago

Hii ni Kali Kaka umeiweka vizuri Sana aiseee

59
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x