Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo yanatokana na sumu zilizopo katika miili yao. Inawezekana umewahi kusikia mambo mengi kuhusu sumu kwenye mwili, lakini hufahamu chazo halisi cha sumu hizi.
Mabadiliko ya mazingira na mtindo wa maisha hupelekea kutengenezeka na kuingia kwa sumu nyingi ndani ya mwili wa binadamu. Sumu hizi hutokana na vyakula, vinywaji na hata mazingira tunayoishi.
Sumu hizi huweza kuleta madhara makubwa mwilini kama vile kushindwa kufanya kazi kwa viungo vya mwili na hata aina mbalimbali za saratani.
Ni vyema ukafahamu njia bora za kuondoa sumu mwilini mwako ambazo unaweza kuzifanya wewe mwenyewe bila gharama za ziada.
1. Kula vyakula vya asili
Hivi leo watu hufikiri kula vyakula vya asili ni kupitwa na wakati. Wengi husifu vyakula vya viwandani na vile vya kukaangwa kuwa ndivyo vyakula bora.
Vyakula kama vile Chipsi, nyama, Baga, na tambi ni baadhi tu ya vyakula ambavyo vinaonekana kuwa vya kisasa na bora zaidi, lakini katika uhalisia manufaa yake mwilini ni kidogo.
Ili uweze kuondoa sumu mwilini mwako ni vyema ukaepuka vyakula hivi kwani huwa vina viini vinavyojenga sumu mwili. Jizoeze kula vyakula vya kuchemsha zaidi tena vya asili. Matunda na mbogamboga zisizo na madawa zitakufaa zaidi.
2. Kunywa maji mengi
Ni dhahiri kuwa miili yetu imejengwa kwa maji asilimia 70, hivyo kunywa vinywaji kama vile soda na sharubati (juice) Â za viwandani kunaongeza sumu mwilini.
Ni muhimu kufahamu kuwa ufanyaji kazi wa viungo kama vile figo hutegemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa maji ya kutosha mwilini. Hivyo maji yakikosekana ni dhahiri kuwa sumu nyingi sana hazitaondolea mwilini kwa njia ya msingi ya haja ndogo.
Soma pia: Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka.
3. Fanya mazoezi
Watu wengi hasa Waafrika hawana utaratibu wa kufanya mazoezi. Kufanya mazoezi kutakuwezesha viungo vyako vya mwili kufanya kazi ipasavyo. Ni dhahiri pia unapofanya mazoezi utatokwa na jasho; na hii ni njia nzuri ya kutoa taka mwilini ikiwemo sumu zilizoingia katika mwili wako. Unaweza kufanya mazoezi ndani au hata nje kutegemea vile unavyopendelea.
4. Punguza mafuta
Inawezekana unapenda kula vyakula vyenye mafuta mengi; hili si jambo zuri kwa ajili ya afya yako. Jizoeze kupunguza ama kuepuka mafuta katika vyakula vile unavyokula kwani si aina zote za mafuta zinafaa kwenye mwili wako.
Hivi leo yapo mafuta yasiyo halisi yanayozalishwa viwandani, hivyo kula mafuta haya ni kuongeza sumu mwilini mwako. Pia ulishaji mbaya wa wanyama umepelekea mafuta ya wanyama kuwa na viambata vyenye sumu ambavyo havifai mwilini mwako – Kwa mfano nguruwe wanapewa ARV na Urea ili wakue haraka.
Jitahidi kuepuka na kupunguza ulaji wa mafuta kadri uwezavyo ili uweze kuondoa sumu mwilini mwako.
5. Kula vyakula vya nyuzinyuzi
Unatakiwa kufahamu kuwa vyakula vyenye nyuzinyuzi ni vizuri pia katika kusafisha mwili na kuondoa sumu au takataka mbalimbali.
Vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ni pamoja na parachichi, ndizi, peazi, karoti, pilipili hoho, mchele wa brown (wanaoutumia watu wa kisukari), maharage meusi, njegere, tende, viazi vitamu, tofaa (apple), machungwa, ugali wa dona pia mkate wa unga wa ngano ambao haujakobolewa. Ulaji wa vyakula hivi utakuwezesha kuondoa kiasi kikubwa cha sumu mwilini.
6. Kaa kwenye hewa safi na yakutosha
Nyumba za kuishi au mazingira mengi ya kazi Afrika bado hayajali sana afya za wakaazi wake. Ikumbukwe kuwa sumu nyingi zipo kwenye hewa kutokana na uchafuzi wa mazingira; hivyo mtu anapokaa mahali ambapo hakuna hewa safi ya kutosha, anaongeza hatari zaidi ya kuongeza sumu mwilini.
Ni vyema ukajitahidi kukaa sehemu zenye hewa safi ya kutosha ili kuhakikisha kuwa huongezi bali unaondoa sumu ndani ya mwili wako.
7. Tambua bidhaa unazozitumia
Watu wengi hununua na kutumia bidhaa bila kuzifahamu vyema, inawezekana ni kutokana na ukosefu wa elimu au kuishi kwa mazoea. Elewa kila chakula au kinywaji unachotumia kina nini ndani yake.
Vinywaji vingine na vyakula vina viambata ambavyo ni sumu katika mwili wako. Kama siyo lazima kutumia kitu basi kiepuke ili kupunguza kama siyo kuondoa kiwango cha sumu kinachoingia mwilini mwako.
9. Epuka matumizi ya plastiki
Vyombo vilivyotengenezwa kwa plastiki vimetokana na kemikali mbalimbali ambazo nyingine ni hatari kwa afya yako. Matumizi ya vyombo vya chakula vilivyotengenezwa kwa plastiki vinaweza kusababisha kemikali kama vile Bisphenol A (BPA) pamoja na polymer kuingia mwilini mwako.
Hatari huzidi pale ambapo vyombo hivi hutumika kuwekea vyakula vya moto, kwani husababisha kemikali hizi kuyeyuka na kuingia kwa kiasi kikubwa mwilini. Unaweza kutumia vyombo vya kioo au udongo ili kukabiliana na tatizo hili.
Soma pia: Athari 5 za Kutumia Vyombo vya Chakula vya Plastiki.
10. Epuka matumizi ya pombe
Kama ilivyo kwa vyakula vya viwandani, pombe nyingi hutengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo nyingine ni hatari kwa afya yako. Ili kuondoa na kupunguza kiasi cha sumu zinazoingia mwilini mwako jitahidi kuepuka matumizi ya pombe na kutumia vinywaji vingine kama vile maji.
Soma pia: Njia 12 za Uhakika za Kuacha Pombe.
11. Tumia dawa kwa uangalifu
Dawa zisipotumika vyema zinaweza kuwa sumu hatari mwilini mwako. Epuka kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu. Dalili za ugonjwa mmoja zinaweza kuwa pia ni dalili za ugonjwa mwingine, hivyo ni vyema kufanya vipimo kabla ya kuanza kutumia dawa.
Unaweza kutumia njia za asili kutibu magonjwa mbalimbali badala ya kukimbilia kutumia dawa za viwandani ambazo zinaweza kusababisha sumu mwilini mwako.
12. Pata masaji
Masaji ina manufaa anuwai kwa jili ya mwili wako. Kufanya masaji hukuwezesha kuwa na mtiririko mzuri wa damu katika sehemu mbalimbali za mwili wako.
Damu inaposafiri vyema mwilini itachukua pia sumu zilizojikusanya kwenye mwili na kuzipeleka kwenye viungo kama ini na figo ili kuchujwa na kutolewa mwilini. Hivyo kama unaweza kupata fursa ya kufanya masaji, basi ifanye ili uweze kuondoa sumu mwilini mwako.
Hitimisho
Ni dhahiri kuwa sumu nyingi huingia katika miili yetu kutokana na mtindo wa maisha au mazingira yetu yasiyozingatia kanuni za msingi za afya bora. Mwili wa binadamu uliumbwa kutegemea na kutumia vitu halisi na si visivyo halisi (artificial).
Hivyo jitahidi kuwa mtu mwenye kupenda mboga na matunda zaidi kuliko vyakula vingine, ili uweze kupunguza kiasi cha sumu kinachoingia kweye mwili wako.
Je umenufaika kupitia makala hii au una swali au maoni? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine.
Eston ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zinazohusu tija, maendeleo binafsi pamoja na afya bora. Analenga kuwahamasisha wengine pamoja na kuubadili ulimwengu kwa kupitia maarifa stahiki.
Pamoja na maelezo mazuri ya uondoaji SUMU mwilini, vipo vyakula vingine tunavyopata mashambani vinalimwa kutumia MADAWA(SUMU) nyingi kuvikuza/kuvitunza; mfano,Karots,nyanya,mahindi nk.Mimi nitaepuka vipi vitu hivi maana uwezekano wa mimi kuvilima vyote siwezi.Naomba ushauri
Nashukuru sana kwa kutembelea blog yetu ya Fahamuhili; tunashukuru pia kwa maoni yako mazuri. Ni vyema kulinda vitu unavyokula; hakikisha tu unanunua vitu kutoka sehemu zinazoaminika kwani huwezi kulima kila kitu. Asante na karibu Fahamuhili.
Nahitaji namba yako 0714234300 au 0753541572
asante sana umetuelimisha vya kutosha
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
ASANTE SANA KWA USHAURI BORA
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Nimepata manufaa kwa kusoma sasa nakwenda kufanyia kazi God bless you
Asante sana kwa maoni yako ya thamani na yenye kutia moyo; karibu sana Fahamuhili.com
Kujua haya ni muhimu sana,maana watu wengi wanaingia hatarini bila kujua,naomba elimu itolewe katika jamii na pia mashuleni ili kuokoa familia na vizazi vyetu
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Kwa kwel nimefundishika vilivyo asanten sana !
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com
Madam nzuri
Yes I want to join in this discussion