Faida 20 za Kula Parachichi - Fahamu Hili
Tuesday, October 3Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Faida 20 za Kula Parachichi

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Parachichi

Parachichi ni aina ya kipekee ya tunda. Matunda mengi kwa asili ni wanga lakini parachichi limejaa mafuta yenye manufaa makubwa kiafya.

Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimebaini kuwa tunda la parachichi limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu.

Ikiwa unapenda kuwa na afya bora kwa kula tunda la parachichi, basi karibu nikushirikishe faida 20 za kula tunda la parachichi.

1. Parachichi limejaa virutubisho mbalimbali

Parachichi ni tunda la pekee ambalo limebeba virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa ajili ya miili yetu. Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi ni:

  • Kalori 240 (184 inatokana na mafuta)
  • Miligramu 11 za sodiamu
  • Gramu 13 za wanga
  • Gramu 10 za nyuzinyuzi za lishe
  • Gramu 1 tu ya sukari
  • Vitamini K: asilimia 26
  • Vitamini C: asilimia 17
  • Potasiamu asilimia 14
  • Vitamini B5: asilimia 14
  • Vitamini B6: asilimia 13
  • Asidi ya Folate: asilimia 20
  • Vitamini E: asilimia 10

Virutubisho vyote hivi ni muhimu kwa ajili ya mwili kujijenga na kujilinda dhidi ya magonjwa.

2. Lina virutubisho vitokanavyo na mimea

Pamoja na parachichi kuwa na virutubisho vingine mbalimbali, bado parachichi lina virutubisho muhimu tunavyovihitaji kutoka kwenye mimea. Virutubisho hivyo ni:

Carotenoids Inayopatikana kutoka kwenye parachichi ina manufaa makubwa kwa ajili ya miili yetu katika kulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali yakiwemo yale yatokanayo na umri.

Persenones A na B – Hii huzuia uvimbe na saratani mwilini.

D-Mannoheptulose Hii ni aina ya sukari inayopatikana kwenye parachichi, na inaaminika kusaidia kutawala kiwango cha sukari mwilini.

3. Husaidia kupunguza uzito

Swala la kupunguza uzito linaathiriwa sana na mfumo mzima wa lishe. Hivyo kula vyakula ambavyo vinawezesha mchakato wa metaboli kwenda vyema kutakuwezesha kupunguza uzito kwa muda mfupi.

Parachichi ni tunda zuri ambalo huwezesha mchakato wa metaboli kwenda vizuri mwilini.

4. Parachichi lina Fatty Acid

Fatty Acid ni asidi itokanayo na mafuta ya parachichi ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya shughuli mbalimbali katika miili yetu.

Fatty Acid inahitajika katika uzalishaji wa homoni, ukuaji wa seli pamoja na ufyonzwaji wa virutubisho.

5. Hupunguza lehemu mbaya (cholesterol)

Mafuta ya lehemu ni hatari ikiwa kiwango chake kitakuwa kingi mwilini; mafuta haya husababisha matatizo mbalimbali hasa maradhi ya moyo.

Matunda ya parachichi hayana lehemu mbaya inayoweza kuathiri afya yako. Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokula parachichi kiwango chao cha lehemu mwilini ni tofauti na wale wasiokula kabisa.

6. Kukabili maradhi ya kisukari

Parachichi ni tunda ambalo kiwango chake cha sukari hakina athari kwenye mwili. Hivyo utumiaji wa parachichi utakuwezesha kuweka kiwango cha sukari mwilini kuwa katika hali nzuri ya wastani.

7. Hulinda afya ya moyo

Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye tunda la parachichi kwa zaidi ya asilimia 14 ni muhimu sana katika utendaji kazi wa misuli ya moyo.

8. Huzuia uvimbe

Asidi ya Oleic inayopatikana kwenye parachichi, imebainishwa na wataalamu kuwa husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia uvimbe mwilini.

9. Hulinda afya ya macho

Kemikali ya lutein na zeaxanthin ni muhimu sana kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya ya macho.

Ikumbukwe kuwa parachichi ni tunda lenye kiasi kikubwa cha lutein ambayo pia hulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali yatokanayo na umri.

Soma pia: Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona.

10. Parachichi lina Potasiamu nyingi kuliko ndizi

Watu wengi wanapenda ndizi kwa kuwa ni chanzo kimoja wapo cha madini ya potasiamu, lakini hawafahamu kuwa ndizi ina potasiamu asilimia 10 na parachichi lina asilimia 14. Hivyo parachichi ni bora zaidi.

Potasiamu ni muhimu katika miili yetu kwani hutuwezesha kutawala kiwango cha sodiamu katika miili yetu na kutuepusha na madhara yatokanayo na madini haya ya sodiamu.

11. Huboresha afya ya nywele na ngozi

Naamini umewahi kusikia kuwa parachichi hutumika kutengenezea mafuta ya nywele na ya ngozi; hii ni kutokana na kusheheni vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele na ngozi zetu.

Hivyo badala kununua mafuta ya gharama kubwa ili kupata vitamini E kwa ajili ya ngozi na nywele zako, basi kula tunda la parachichi sasa.

12. Huzuia saratani

Tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa kula matunda ya parachichi kunasaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani ya tezi dume.

Hata hivyo, tafiti juu ya swala hili siyo nyingi sana lakini bado unaweza kula parachichi na kupata faida nyingine kemkem.

13. Huimarisha mifupa

Kutokana na parachichi kuwa na vitamini K pamoja na madini ya kopa na folate ambavyo ni muhimu kwa ajili ya mifupa, tunda hili linakuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha mifupa.

14. Huboresha mmeng’enyo wa chakula

Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu sana kwa ajili ya kuufanya mmeng’enyo wa chakula uende vizuri. Parachichi ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa karibu asilimia 13 ambazo ni sawa na kiwango cha asilimia 54 unachotakiwa kula. Je bado huoni umuhimu wa tunda hili? Anza kula ili uboreshe mmeng’enyo wako wa chakula sasa.

15. Ni muhimu kwa wajawazito

Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha folate, potasiamu, Vitamini C na B6 ambazo ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa mtoto; kunalifanya tunda la parachichi kuwa na umuhimu mkubwa kwa wajawazito.

Hivyo inashauriwa wanawake wajawazito wazingatie ulaji wa matunda hasa tunda la parachichi.

16. Huimarisha kinga ya mwili

Kinga ya mwili hutegemea vitamini B, C na E ili kujiimarisha na kujijenga. Hivyo ulaji wa parachichi utaimarisha kinga ya mwili yako kwani parachichi limesheheni vitamini B, C na E.

17. Huboresha afya ya ubongo

Madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi kwa zaidi ya asilimia 19 yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye kazi vyema.

Hivyo basi, ukitaka kuweka afya ya ubongo wako katika hali nzuri na kuweza kufikiri vyema, basi kula tunda la parachichi mara kwa mara.

18.Huboresha ufyonzwaji wa virutubisho

Baadhi ya virutubisho hufyonzwa kunapokuwa na mafuta (fat soluble); virutubisho hivyo ni kama vile vitamini A, E, D na K.

Kula parachichi kutawezesha virutubisho hivi kufyonzwa vyema mwilini.

19. Hukuweka katika hali nzuri (mood)

Baadhi ya tafiti zimeeleza kuwa watu wenye msongo wa mawazo wana upungufu mkubwa wa madini ya potasiamu.

Kwa kuwa parachichi ni chanzo kikubwa cha madini ya potasiamu, basi tunda hili linaweza kusaidia sana kukuweka katika hali nzuri.

20. Huongeza nguvu za mwili

Miili yetu inategemea sana wanga, protini na mafuta ili kupata nguvu. Ni wazi kuwa sasa unafahamu kuwa tunda la parachichi ni chanzo kikubwa cha virutubisho hivi vitatu.

Hivyo kuongeza parachichi katika mlo wako kutakuwezesha kuuongezea mwili wako nguzu zaidi.

Neno la mwisho:

Naamini sasa hutopuza tena tunda la parachichi kwani umefahamu faida tele za tunda hili. Parachichi ni tunda linalopatikana kwa urahisi bila gharama kubwa ikilinganishwa na matunda mengine kama vile tofaa (apple).

Fanya matunda kuwa sehemu ya mlo wako sasa hasa tunda la parachichi ili uwe na afya njema. Je wewe huwa unakula parachichi  kwa kiasi gani?

Ukiwa na maoni au maswali tafadhali tuandikie hapo chini. Usisahau kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3.4 36 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

37 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Judith Kashuku
Judith Kashuku
5 years ago

Nimependa sana hongera kwa kutujuza haya kwa afya

Zena ismail
Zena ismail
4 years ago

Hongera Sana kwa makala nzuri inayohusu atya zetu

Kornelio Maanga
Reply to  Zena ismail
4 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Wamanja
Wamanja
4 years ago

Tena huku kwetu hayana bei kabisa

Kornelio Maanga
Reply to  Wamanja
4 years ago

Ni kweli, inabidi sasa watu wajue thamani yake. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Mr.thicke
Mr.thicke
4 years ago

Nmejifunza kitu kuhusiana na mada hiyo, Hongera sana pia ahsante đź’Ş

Kornelio Maanga
Reply to  Mr.thicke
4 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Mohd
Mohd
4 years ago

Hongera Kwa ufafanuzi mzuri

Kornelio Maanga
Reply to  Mohd
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Mutashobya richar
Mutashobya richar
4 years ago

Ahsante sana kwa taarifa za faida za kula parachichi

Kornelio Maanga
Reply to  Mutashobya richar
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Emmanuel paul
Emmanuel paul
3 years ago

Ahsante san kwa maoni yako

Kornelio Maanga
Reply to  Emmanuel paul
3 years ago

Tunashukuru sana kwa kuwa msomaji wetu; pia tunashukuru kwa maoni yako ya thamani; tunakutakia kila la heri katika kutimiza malengo yako…karibu sana Fahamuhili.

Raiza yusuph
Raiza yusuph
3 years ago

.Kazi nzuri

Kornelio Maanga
Reply to  Raiza yusuph
3 years ago

Tunashukuru sana kwa kuwa msomaji wetu; pia tunashukuru kwa maoni yako ya thamani; tunakutakia kila la heri katika kutimiza malengo yako…karibu sana Fahamuhili.

Arnold Mwambungu
Arnold Mwambungu
3 years ago

Nimejifunza vingi sana ii page nzur

Kornelio Maanga
Reply to  Arnold Mwambungu
3 years ago

Tunashukuru sana kwa kuwa msomaji wetu; pia tunashukuru kwa maoni yako ya thamani; tunakutakia kila la heri katika kutimiza malengo yako…karibu sana Fahamuhili.

Heri mallya
Heri mallya
3 years ago

Asantee sana..ni Tunda ambalo ninaipenda kwa moyo wangu wwwote…inasemekana mama yangu alikula sana akinibeba..kwa week hukosa kulila labda mara moja na nusu.

Kornelio Maanga
Reply to  Heri mallya
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Rashid
Rashid
3 years ago

Hii habari ni nzuri sana Mungu akujaalie zaidi hakika umefundisha vyema sana nimeelewa sana zaid ya sana

Kornelio Maanga
Reply to  Rashid
3 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Saphnessedrian
Saphnessedrian
2 years ago

Kiukwel parachichi ni tunda lenye maajabu mengi sana

Kornelio Maanga
Reply to  Saphnessedrian
2 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Saphnessedrian
Saphnessedrian
2 years ago

Asante sana

Kornelio Maanga
Reply to  Saphnessedrian
2 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Kezia
Kezia
1 year ago

Thank byou

Kornelio Maanga
Reply to  Kezia
1 year ago

Asante sana kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

babuali
babuali
Reply to  Kornelio Maanga
10 months ago

Ni maelezo mazuri ingawa majani ,magome,mizizi na kokwa hazikushirikishw sana katika maelezo

Henry
Henry
11 months ago

Nashuru nimejua

Shomy classic
Shomy classic
8 months ago

Aisee me napenda ukila na chumvi ni matamu saana nisipokula kwa siku nahis kama nimemiss kitu

Kornelio Maanga
Reply to  Shomy classic
2 months ago

Hongera lakini Usisahau pia kutawala kiwango cha chumvi. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Frank saimoni mgimba
Frank saimoni mgimba
6 months ago

Tunashukulu kwa uduma zenu

Kornelio Maanga
Reply to  Frank saimoni mgimba
2 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Maguta
Maguta
5 months ago

Kiafya inashauriwa kula matunda mangapi ya parachichi kwa siku?

Emmanuel
Emmanuel
4 months ago

🤓wwaaoooww!!!! imekaa uzulii!.

Kornelio Maanga
Reply to  Emmanuel
2 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

37
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x