Njia 10 za Kukufanya Kuwa na Furaha - Fahamu Hili
Friday, September 29Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Njia 10 za Kukufanya Kuwa na Furaha

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Mwenye furaha

Kutokana na changamoto za kimazingira, kiuchumi na kijamii, watu wengi wamejikuta wakikosa furaha. Ni wazi kuwa kukosa furaha kuna madhara makubwa kwenye afya ya mwili, akili na hata katika utendaji wako wa kazi.

Watu wengi hutamani kuwa na furaha lakini bado hawapati furaha; wengi hudhani kuwa na vitu kama vile pesa ndiyo chanzo cha furaha, lakini mambo hayawi kama walivyotarajia pindi wapatapo vitu hivyo.

Je unahitaji kuwa na furaha ili uboreshe afya na ufanisi wa utendaji kazi wako? Karibu nikushirikishe njia 10 za kukufanya kuwa na furaha.

1. Samehe

Watu wengi hukosa furaha kutokana na kubeba uchungu na maumivu yaliyotokana na watu waliowakosea. Ikiwa unataka kuwa na furaha ni muhimu kumsamehe aliyekukosea hata kama hajaomba msamaha.

Kumsamehe aliyekukosea kuna manufaa kwako zaidi kuliko kwa yule aliyekukosea. Mara nyingi aliyekosea huendelea na maisha yake ya kawaida huku aliyekosewa akizidi kuumia.

Soma pia: Sababu 9 za Kwanini Umsamehe Aliyekukosea.

2. Fanya unachokipenda

“Mafanikio siyo ufunguo wa furaha. Furaha ni ufunguo wa mafanikio. Kama unapenda unachokifanya, utafanikiwa.”

Albert Schweitzer

Moja kati ya siri kubwa ya kufanikiwa na kuwa na furaha katika kile unachokifanya, ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapopenda kile unachokifanya, utakuwa na amani na furaha mara ukutanapo na changamoto au vikwazo.

Soma pia: Hatua 7 za Maumivu Zisizoepukika Kabla ya Kufanikiwa.

3. Kuwa na shukrani

Mara nyingi tunatazama mambo mengi kiasi cha kushindwa kuwa na shukurani kwa yale tuliyonayo. Ni rahisi kuona kuwa mambo kama vile afya, marafiki, usalama, malazi n.k. ni mambo madogo ambayo hatupaswi kushukuru kwa ajili yake.

Kwa hakika wapo watu wanaotafuta mambo hayo lakini hawayapati. Hivyo ili kupata furaha ni muhimu kutambua na kushukuru kwa yale machache tuliyonayo.

Soma pia: Mambo 20 Yakushukuru Kwa Ajili Yake Kwenye Maisha.

4. Saidia wengine

Kumsaidia mtu mwingine siyo kumpa pesa au vitu; hata kumpa mtu ushauri au kumtia moyo kunaweza kuwa na maana kubwa kwa mtu huyo.

Unapomsaidia mtu mwingine unajisikia kuwa na thamani na furaha kwani umeweza kufanya kitu chenye manufaa kwenye maisha ya mtu mwingine.

Nakumbuka niliwahi kumshauri mtu mmoja aliyekuwa amekata tamaa kutokana na kukosa pesa; baada ya muda kupita nikakutana naye, akashukuru sana kwa ushauri wangu. Alinieleza kuwa kama siyo yale maneno niliyomweleza angekuwa ameshajiua. Ni wazi kuwa nilijihisi mwenye furaha na amani kutokana na kuweza kumsaidia mtu mwingine.

5. Shirikisha wengine

Inawezekana jambo linalokukosesha furaha kuna mtu mwingine anafahamu utatuzi wake. Hivyo kwa njia ya kumshirikisha mwingine utapata ushauri au hata utatuzi wa tatizo lako. Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unamshirikisha mtu sahihi.

6. Ondoa mawazo hasi

“Akili ni kila kitu. Unavyofikiri ndivyo unavyokuwa.”

Buddha

Mawazo gani uliyonayo kwenye fikra zako? Je unawaza tu huwezi au kushindwa? Mawazo hasi au ya kushindwa ni chanzo kikuu cha kukukosesha furaha.

Amini unaweza hatakama unaona giza; leo ni giza, kesho ni mvua lakini keshokutwa jua litawaka.

Usikate tamaa, ondoa mawazo mabaya yanayokufanya ukose furaha na mani sasa.

Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

7. Usitafute ukamilifu

Mara nyingi watu hukosa furaha kwa sababu wanatafuta ukamilifu. Kwa hakika hakuna binadamu aliyekamilika; wote tuna madhaifu na mapungufu ya aina mbalimbali.

Badala ya kuyatafakari madhaifu yako na kuruhusu yakukoseshe furaha; yakubali na ukabiliane nayo kwa namna bora zaidi.

8. Kaa na watu sahihi

Je umekaa katikati ya watu wanaokulaumu, kukudharau au kukubeza kila wakati? Au pengine umekaa katikati ya watu walioshindwa wanaolaumu na kulalamikia kila kitu?

Watu wa aina hii wanakusababisha ukose furaha. Hakikisha unakaa katikati ya watu wanaokutia moyo na kukuthamini. Epuka watu walioshindwa ambao kazi yao kubwa ni kulalamika na kulaumu kila kitu.

Soma pia: Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako.

9. Ishi maisha yako

“Muda wako ni mdogo, usiupoteze kuishi maisha ya mtu mwingine.”

Steven Jobs

Watu wengi hukosa furaha kutokana na kuishi maisha ya watu wengine. Jikubali ulivyo, usitake kuwa kama mtu mwingine kwani hutoweza na utaishia kukosa furaha. Tambua wewe ni wa pekee na tembea katika upekee wako huo.

10. Jiburudishe

Je unajua kuimba? Je unapenda michezo au kusikiliza mziki? Kama jibu ni ndiyo, basi hii ni njia mojawapo amabayo inaweza kukupa furaha.

Ikiwa umekosa furaha, unaweza kuimba, kusikiliza mziki au hata kushiriki kwenye mchezo unaoupenda

Soma pia: Tabia 10 zitakazobadili maisha yako.

Hitimisho

Naamini sasa baada ya kusoma makala hii juu ya njia za kupata furaha, hutokosa tena furaha maishani mwako.

Usiruhusu vitu vya dunia hii vinavyopita vikunyime amani na furaha; maisha ni bora zaidi kuliko vitu. Je bado unatatizo katika kupata furaha? Je kuna njia nyingine unayoitumia kupata furaha?

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini. Usisahau kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

4.1 8 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

24 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Paul Elias
Paul Elias
4 years ago

makala iko poa ila jaribu ku-explain kwa undan zaid

Emmanuel Mayunga
Emmanuel Mayunga
4 years ago

nashukuru kaka nimependa sana mawazo yako naomba kupata mawasiliano yako kupitia namba 0753376327

Mungure Omben
Mungure Omben
3 years ago

Makala zuri imenielimisha

Agness mbunda
Agness mbunda
3 years ago

Nashukuru kwa makala nzur mana imenifunza nilishakata tamaa kila kukicha nilikua mtu wa kulia kutokana na mambo nnayopitia

Kileo musa
Kileo musa
3 years ago

Nimepemda naomba nijiunge

Neema salum
Neema salum
1 year ago

Asante nimejifunza mengi

Neema salum
Neema salum
1 year ago

🙏

Jessica
Jessica
1 year ago

Asante sana kwa makala hii, hakika umenijenga, imenitoa kwenye shimo, imenitoa kwenye giza sasa nimepata mwanga nimenza kujiona mimi na ninaiyona kesho yangu iliyojaa furaha, Asante na barikiwa.

Joh
Joh
1 year ago

Good

Gerald killongo
Gerald killongo
1 year ago

Shukran sana nimejifunza mazuri yaliyoniimarisha, naanza kujiona Mpya sasa!

Asnary
Asnary
1 year ago

Ahsante Sana

Caldina Mwinuka
Caldina Mwinuka
11 months ago

Nimewaelewa sana asanteni mmenitia moyo

Mariam Issa
Mariam Issa
10 months ago

Angetokea mtu akan kanseli jamani sina raha na haya maisha napenda watu nisaidia lkn mm sipat wa kunifariji kama wenzangu 😭😭😭😭

trackback
Sababu Kwanini Unakosa Furaha Mara Kwa Mara -
9 months ago

[…] Soma pia njia 10 za kufanya ili uwe na furaha […]

24
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x