Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako

Washirikishe Wengine Makala Hii:

sumu

Watu wasiofaa wapo kila mahali, kwa hakika wanakwaza na kurudisha maendeleo ya watu nyuma. Ukiwa kama mjasiriamali au mtu mwingine yeyote unatakiwa kufanya bidii kufikia malengo yako bila kuruhusu aina za watu wasiofaa kukuvuruga.

Inawezekana unawafahamu watu ambao ni sumu; yawezekana wanafanya kazi na wewe, ni marafiki zako au unaishi nao. Kadri unavyowaepuka katika maisha au kazi yako ndivyo mambo yatakavyozidi kuwa mazuri.

Fuatana nami katika makala hii nikushirikishe aina 8 za watu ambazo ni sumu unazotakiwa kuziepuka katika maisha yako.

1. Watu wanaohoji kila kitu

Watu wanaohoji kila kitu hutafuta njia ya kupinga na kukosoa kila unachokifanya. Utatumia muda mwingi kuwaelewesha lakini watasikia kwa sikio moja na swala hilo kutokea sikio la pili. Kujaribu kutafuta msaada na ushauri kutoka kwa watu wa aina hii ni kupoteza muda.

Watu hawa huwa na maswali kama vile kwanini unafanya hivi? Unapoteza muda; si jambo zuri; la fulani liliharibika; nani kakuambia ufanye; nitapata nini mimi? hauwezi kufanikiwa kwenye hili labda tafuta jingine; linahitaji fedha nyingi mno n.k.

2. Wenye wivu

Safari ya mafanikio ina milima na mabonde, hivyo ni vyema kuwa na watu ambao watakuinua na kukutia moyo unapopita katika changamoto. Watu wenye wivu huamini kuwa kila kitu kizuri kinatakiwa kitokee kwao tu.

Watu hawa watafurahia unapopata matatizo tu, wala hawatakusaidia wakati wa changamoto. Hivyo ni vyema ukajiepusha na aina hii ya watu ili uweze kufanikiwa katika maisha yako.

3. Wajuaji

Wajuaji hawako tayari kuambiwa au kuelekezwa kitu chochote, kulingana na wao wanajua kila kitu na wanajua njia bora ya kufanya kila kitu. Si kwamba watu hawa hawahitajiki katika maisha ya mtu binafsi pekee, bali hata katika mazingira ya kazi.

Katika maisha upo usemi unaosema kuwa “wapishi wengi huharibu mchuzi”. Hivyo basi, kwa kuwa wajuaji hujifanya wanajua kila kitu na  hawako tayari kupokea maelekezo, basi ni vyema ukawaepuka wasije wakakukwamisha.

4. Wenye kiburi

Watu wenye kiburi wamejaa katika jamii inayotuzunguka. Watu wenye kiburi hawaambiliki wala kushaurika, wao hufikiri ni bora kuliko kila mmoja anayewazunguka.

Unapofanya kazi na mtu mwenye kiburi ni vigumu kukaa naye pamoja mkapanga majukumu na yakatekelezwa; hivyo ni bora kuwaepuka.

5. Watu wenye visingizio na walalamikaji

Watu wa aina hii huwa hawaishiwi sababu, wao hulaumu kila kitu na kila mtu. Watu hawa hawakubali kupokea majukumu bali huwanyoshea wengine vidole; pia hawako tayari kuwajibika kutokana na makosa yao.

Mara nyingi watu hawa husingizia kitu au mtu mwingine kwa kila kosa wanalolifanya. Waondoe kwenye maisha, biashara au ofisi yako sasa ili uishi kwa amani na kuwa na mafanikio.

6. Wale wenye mawazo hasi au wapinzani

Mtu mwenye mawazo hasi atakausha nguvu zako za mawazo chanya. Watu hawa kila mara hujitahidi kukuvuta chini ili ufanane nao na kuamini kile wanachokiamini. Kamwe huwezi kupokea neno la hamasa kutoka kwao.

Watapuuza kila wazo jema ulilo nalo, watatafuta kila njia ya kukuonyesha jinsi utakavyoshindwa katika wazo lako kuliko utakavyofanikiwa. Hivyo ni vyema ukachukua hatua mapema ya kuwaepuka watu hawa.

7. Watu waongo

Ili kufanikiwa katika maisha unahitaji kuwa na watu ambao wanaaminika na kutegemewa. Unapokuwa na watu waongo ni vigumu kufanikiwa kwani utaamani mambo au taarifa fulani kumbe hazina ukweli wowote.

Hebu fikiri unafanya kazi na mhasibu mwongo; ataiba pesa au kupoteza taarifa kisha atakudanganya kuwa hajafanya hivyo; je unajua nini kitatokea? Utapata hasara; hivyo basi jitahidi kujiweka katikati ya watu wakweli.

8. Wambea

Aina hii ya watu ipo kila mahali, ofisini, nyumbani, shuleni n.k. Watu wambea hawawezi kutofautisha uzushi au uvumi na ukweli.

Watu wambea husambaza taarifa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine; kwa ufupi mtu anayekuambia taarifa za mwingine ndiye yeye huwaambia wengine taarifa zako. Wambea hutengeneza mazingira mabaya ya kazi yenye chuki na ugomvi. Hivyo ni vyema kuwaondoa watu hawa katika maisha, biashara au ofisini kwako.

Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

Neno la mwisho:

Nakukumbusha usemi usemao “ukikaa na waridi pia utanukia”; hivyo ukikaa na watu wabaya pia watakuwa na athari mbaya katika maisha yako. Jitahidi kujiweka katika mazingira yenye watu wanaopenda kufanikwa na wenye mawazo chanya.

Je una maoni gani kuhusu makala hii? Je ulishawahi kuathiriwa na aina hizi za watu? Tafadhali tuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine makala hii. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Fecebook ili kufahamu mengi zaidi.

3 10 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

7 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ayoub Leo
Ayoub Leo
3 years ago

Asante sana.Ujumbe mzuri wenye kutujenga.

Kornelio Maanga
Reply to  Ayoub Leo
2 years ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com

Yesse Munyali
Yesse Munyali
1 year ago

Maoni yangu ni kwamba ni kweli ni muhimu kuwaepuka watu wa aina ihii lakini ukiwa unamtenga mtu kutokana na tabia moja moja kama ulivyo elekeza utajikuta umepoteza au umetengana na kila mtu Kwene maisha coz hamna mtu aliye parfect in all coz unaweza kuta mtu ni muongo lakini hana wivu

Kornelio Maanga
Reply to  Yesse Munyali
6 months ago

Kuwaepuka hakumaanishi kutokuwasidia au kuwatenga, bali ni kujiepusha na tabia na ushawishi wao. Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Elinuru Ifande
Elinuru Ifande
1 year ago

Asante sana kwa makala nzuri yenye hekima na iliyojaa ukweli.

Kornelio Maanga
Reply to  Elinuru Ifande
6 months ago

Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com

Emanuel. Magembe
Emanuel. Magembe
7 months ago

Join and me

7
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x