Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema - Fahamu Hili
Friday, April 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Tovuti

Unaweza ukawa unajiuliza tovuti hizo ni zipi? Intaneti imejaa tovuti nyingi sana, za maana na zisizo za maana. Hata hivyo bado tovuti za maana na zenye manufaa zimeweza kujibainisha wazi kati ya zile zisizofaa.

Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe tovuti 20 ambazo kwa namna moja au nyingine zitakufaa katika maisha yako ya kila siku.

1. Have I Been Pwned?

Tovuti: https://haveibeenpwned.com/

Hii ni tovuti nzuri sana kwa ajili ya kukagua kama barua pepe yako imeshavuja kwenye taarifa za siri zilizoibiwa. Hivi leo kuna makampuni na tovuti nyingi zinazodukuliwa na kuibiwa taarifa za watumiaji wake. Hivyo unaweza kuwa ni moja kati ya watu ambao barua pepe zao ziliibiwa. Ikiwa utaambiwa kua barua pepe yako imeonekana kwenye taarifa zilizodukuliwa basi badili neno la siri haraka.

2. Radio Garden

Tovuti: http://radio.garden/

Kwa kupitia tovuti hii unaweza kusikiliza stesheni mbali mbali za redio duniani kote.

3. 10 Minute Mail

Tovuti: http://www.10minutemail.com/

Tovuti hii inafaa ikiwa unahitaji barua pepe ya muda mfupi tu. Inawezekana unataka kuingia kwenye tovuti fulani lakini inataka uweke barua pepe yako; ikiwa hautaki kuweka barua pepe yako halisi basi unaweza kupata barua pepe ya muda katika tovuti hii.

4. Math Way

Tovuti: http://www.mathway.com/

Ni tovuti maarufu kwa ajili ya wanafunzi, inafanya utatuzi wa maswali ya hesabu na Kemia na kuwawezesha wanafunzi kupata majibu.

5. Fake Spot

Tovuti: http://fakespot.com/

Ikiwa wewe ni mnunuzi wa bidhaa kutoka kwenye soko maarufu la Amazon; basi unaweza kutambua kama bidhaa ni feki kwa kutumia tovuti hii.

6. Noisli

Tovuti: https://www.noisli.com/

Kuna watu wanaopenda kufanyia kazi kwenye mazingira yenye sauti fulani ndipo wanfanye kazi vizuri. Ikiwa wewe ni mmoja wapo Noisli ina sauti kama vile kutiririka kwa maji na sauti za ndege, hivyo kukuwezesha kufanya kazi katika mazingira unayoyapenda.

7. Deadmansswitch

Tovuti: https://www.deadmansswitch.net/

Deadmansswitch ni tovuti ambayo hukuwezesha kutuma barua pepe baada ya kufariki. Kutuma barua pepe baada ya kufariki?

Ndiyo; tovuti hii itakutumia barua pepe kila baada ya kipindi fulani cha muda kuona kama bado upo hai, ikiwa itabaini kuwa haupo hai basi itatuma barua pepe kwa watu uliowachagua.

Hii inafaa sana pale ambapo kuna taarifa ambazo ungependa kuzitoa baada ya wewe kufa kama vile wosia, tarifa zako za kibenki, mali zako, wadaiwa wako n.k

8. Smallpdf

Tovuti: http://smallpdf.com/

Smallpdf ni tovuti ni tovuti intakayokusaidia kwa mahitaji yako yote yanayohusiana na pdf. Ikiwa unataka kutengeneza, kuhariri au kubadili mafaili ya pdf basi hii tovuti ni kwa ajili yako.

9. Zero Dollar movies

Tovuti: http://zerodollarmovies.com/

Zero Dollar movies ni tovuti kwa jili ya wapenzi wa filamu kutazama zaidi ya filamu zaidi ya 15,000 bure kabisa.

10. Picmokey

Tovuti: http://www.picmonkey.com/

Hii ni tovuti kwa ajili ya kuhariri picha kwa kupitia mtandao. Utaweza pia kutengeneza picha nzuri kwa ajili ya akaunti zako za mitandao ya kijamii.

11. Ninite

Tovuti: https://ninite.com/

Ninite ni tovuti inayokuwezesha kupakua na kusakinisha (install) programu unazozihitaji kwa pamoja kwenye kompyuta yako.

12. Duolingo

Tovuti: https://www.duolingo.com/

Je unapenda kufahamu lugha mbalimbali? Kwa kupitia tovuti hii ya Duolingo unaweza kujifunza lugha mbambali duniani bure kabisa.

13. Login2

Tovuti: http://login2.me/

Je kuna tovuti unayotaka kuingia lakini huna akaunti? Kwa kupitia Login2 utaweza kupata jina la mtumiaji (username) na nywila (password) za kuingia kwenye karibu kila tovuti.

14. Wetransfer

Tovuti: https://www.wetransfer.com/

Hii ni tovuti kwa ajili ya wale wanaopenda kutuma mafaili makubwa. Kwa kupitia tovuti hii utaweza kutuma mafaili yenye ukubwa wa hadi GB 2 bure.

15. Codecademy

Tovuti: http://www.codecademy.com/

Codecademy ni tovuti kwa ajili ya kujifunza lugha za kutengenezea programu za kopyuta. Kama unataka kujifunza kutengneza programu za kompyuta unaweza kutumia tovuti hii bure.

16. Stupeflix

Tovuti: https://studio.stupeflix.com/en/

Hii ni tovuti itakayokuwezesha kutengeneza video nzuri kwa kutumia violezo (templates) vilivyoandaliwa tayari bure bila malipo yoyote. Unaweza kupakia picha na video mbalimbali ili kukamilisha lengo lako.

17. Google Translate

Tovuti: https://translate.google.com

Hii ni huduma ya google ya kutafsiri maandishi kwenda kwenye lugha mbalimbali. Unaweza pia kuitumia tovuti hii kusoma maandishi yako kwa sauti. Kumbuka kutokana na kutumia akili bandia (artificially intelligent) kutafsiri, baadhi ya tafsiri zinaweza kuwa duni.

18. Homestyler

Tovuti: http://www.homestyler.com/

Hii ni programu itakayokuwezesha kutengeneza ramani ya nyumba katika mwonekano wa 3D.

19. Pixabay

Tovuti: http://pixabay.com/en/

Pixabay ni tovuti kwa ajili ya kupakua picha, video na michoro mbalimbali kwa ajili ya matumizi yako bure kabisa.

20. Kiddle

Tovuti: http://www.kiddle.co/

Kiddle ni injini pekuzi (search engine) nzuri sana kwa ajili ya watoto. Ikiwa unataka kumruhusu mtoto atumie intaneti bila kukutana na mambo machafu au mabaya basi unaweza kumfungulia injini pekuzi hii ya Kiddle.

Hitimisho

Naamini umefahamu tovuti nzuri ambazo kwa namna moja au nyingine zitakufaa sana kwenye maisha yako ya kila siku. Zipo tovuti nyingi sana duniani, lakini hapa nimekuchagulia baadhi tu ambazo naamini zitakuwa muhimu kwako.

Je umefurahia orodha hii? Je una swali au maoni? Tafadhali tuandikie hapo chini. Pia usisahau kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook pamoja na kuwashirikisha wengine makala hii.

3.3 4 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

1 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Steve
Steve
9 months ago

Oky

1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x