Vigezo na Masharti - Fahamu Hili
Tuesday, March 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Vigezo na Masharti

Karibu sana Fahamuhili!

Asante kwa kutumia huduma za tovuti yetu. Huduma zinazotolewa na Fahamuhili zinasimamiwa na Fahamuhili LLC. Kwa kutumia Huduma zetu, moja kwa moja unakubaliana na vigezo na masharti haya. Tafadhali yasome kwa makini na kuyaelewa. Kama kuna swali au unahitaji maelezo ya ziada, tafadhali tembelea ukurasa huu na kuwasilisha ombi lako. Ili kutumia huduma zetu, ni lazima ufuate sera zozote zinazotolewa kwako na unakubaliana na Sera yetu ya faragha. Vigezo na masharti ya kutumia huduma zetu ni kama ifuatavyo;

  • Usitumie Huduma zetu vibaya. Kwa mfano, usivuruge huduma zetu au kujaribu kuzifikia kwa kutumia mbinu nyingine isipokuwa kiolesura na maagizo tunayotoa.
  • Unaweza kutumia huduma zetu kama inavyoruhusiwa kisheria tu, zikiwemo sheria na kanuni husika za kudhibiti maudhui.
  • Tunaweza kusimamisha au kusitisha utoaji wa huduma zetu kwako kama hutafuata masharti au sera zetu au kama tunachunguza mwenendo mbaya tunaoshuku.
  • Kutumia huduma zetu hakukupi umiliki wa hakimiliki zozote katika huduma zetu au maudhui unayoyapata.
  • Huwezi kutumia maudhui kutoka kwenye Huduma zetu bila ruhusa ya maandishi ya Fahamuhili au umeruhusiwa vinginevyo kisheria kufanya hivyo.
  • Masharti haya hayakupi haki ya kutumia maudhui, rajamu au nembo zozote zinazotumiwa katika huduma zetu.
  • Usiondoe, usifute wala usibadilishe taarifa zozote za kisheria zinazoonyeshwa ndani ya au pamoja na huduma zetu.
  • Tunaruhusu kutoa maoni mbalimbali katika tovuti na huduma zetu. Hivyo, maoni yenye misingi ya chuki, matusi, matangazo ya kibiashara, ubaguzi n.k; tuna haki ya kuyaondoa. Hairuhusiwi kabisa kuweka maoni yanayokiuka sheria za nchi au za tovuti hii.
  • Huduma zetu huonyesha maudhui mengine ambayo si ya Fahamuhili. Maudhui hayo ni wajibu wa yule anayeyatoa peke yake (Matangazo n.k).
  • Tunaweza kutathimini maudhui ili kuamua kama ni kinyume cha sheria au yanakiuka sera zetu, na tunaweza kuondoa au kukataa kuyachapisha maudhui tunayoamini yanakiuka sera zetu au sheria. Kuhusiana na matumizi yako ya huduma, tunaweza kukutumia matangazo ya barua pepe, arafa za huduma, ujumbe wa usimamizi na maelezo mengine. Unaweza kuamua kujiondoa kwenye baadhi ya mawasiliano hayo.
  • Baadhi ya huduma zetu zinapatikana kwenye vifaa vya mkononi. Usitumie huduma kama hizo katika njia ambayo inakutatiza na kukuzuia kutii sheria za trafiki au za usalama.

Ulinzi wa Faragha na Hakimiliki

Sera za faragha za Fahamuhili huelezea tunavyokusanya na kutumia taarifa zako binafsi na kulinda faragha yako unapotumia huduma zetu. Kwa kutumia huduma zetu, unakubali kwamba Fahamuhili inaweza kutumia taarifa hiyo kulingana na sera zetu za faragha. Hairuhusiwi kwa namna yoyote kunakili au kusambaza maudhui yaliyo kwenye tovuti hii. Kufanya hivyo ni kinyume na sheria, Fahamuhili wana haki ya kukuchukulia hatua za kisheria. Huruhusiwi kunakili, kubadilisha, kusambaza, kuuza au kukodisha sehemu yoyote ya huduma zetu au programu zilizojumuishwa, isipokuwa umeruhusiwa kisheria au una ruhusa yetu kimaandishi.

Kubadilisha na Kukatisha Huduma zetu.

Tunabadilisha na kuboresha Huduma zetu kila wakati. Tunaweza kuongeza au kuondoa utendakazi au vipengele, na tunaweza kusimamisha au kusitisha Huduma kabisa. Unaweza kuacha kutumia Huduma zetu wakati wowote, ingawa tutasikitika kukupoteza. Fahamuhili inaweza kuacha kukupa huduma, inaweza pia kuongeza au kuweka mipaka mipya kwa huduma zetu wakati wowote.

Kuhusu Masharti haya

Tunaweza kubadilisha masharti haya au masharti ya ziada yanayotumika kwa huduma, kwa mfano, kuonyesha mabadiliko katika sheria au mabadiliko katika huduma zetu. Inafaa uangalie masharti haya mara kwa mara.Tutaweka taarifa za marekebisho ya masharti haya kwenye ukurasa huu. Tutaweka taarifa ya masharti ya ziada yaliyorekebishwa katika Huduma husika.