
Mambo 10 ya Kuzingatia ili Kutoa Huduma Nzuri kwa Wateja
Changamoto ya huduma duni kwa wateja imekuwa kubwa sana kwenye biashara nyingi za kiafrika. Watoa huduma wengi hawajui na hawataki kufahamu umuhimu wa kutoa huduma nzuri kwa wateja. Kwenye biashara na huduma nyingi mteja huchukuliwa kama kitu kisicho na nafasi wala umuhimu wowote. Lakini ukweli ni kuwa mteja ni msingi muhimu sana katika kufanikiwa kwa huduma au biashara yoyote ile. Kumbuka biashara yoyote isiyozingatia kutoa huduma nzuri kwa wateja wake itapoteza wateja na hatimaye itakufa. Kwa kutambua umuhimu wa kutoa huduma nzuri kwa wateja karibu nikushirikishe mambo 10 ambayo unapaswa kuyazingatia ili kutoa huduma nzuri. 1. Elewa hitaji la mteja Kamwe huwezi kumhudumia mteja vizuri bila kufahamu hitaji lake. Mara mteja anapofika katika biashara yako hakikisha unafa...