Mbinu 10 za Kuongeza au Kuvutia Wateja Kwenye Biashara - Fahamu Hili
Wednesday, October 23Maarifa Bila Kikomo

Mbinu 10 za Kuongeza au Kuvutia Wateja Kwenye Biashara

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Wateja

Haijalishi huduma au bidhaa yako ni kubwa kiasi gani, biashara yako haitazalisha pesa kama wateja hawatakuwa tayari kununua bidhaa au huduma yako. Hakuna wateja, hakuna biashara.

Tatizo la kukosa wateja hukabili sana biashara ndogo, na hata kusababisha biashara hizo kufa. Siyo kwamba wateja hawapendi kununua bidhaa za biashara hizi, bali tatizo kubwa ni mbinu duni za kujitangaza na masoko.

Katika makala hii nitakueleza mbinu 10 rahisi na za gharama nafuu ambazo unaweza kuzitekeleza na ukaongeza au kuvutia wateja zaidi kwenye biashara yako.

1. Lugha nzuri

Katika mambo yanayowapotezea wafanyabiashara wengi wateja ni lugha mbaya kwa wateja. Hakuna mteja anayependa kupokelewa au kujibiwa vibaya.

Hakikisha unazungumza na wateja wako kwa namna bora ambayo wataona unawajali, unawathamini na kuwaheshimu.

Mimi mwenyewe ninapenda kwenda kwenye biashara ambayo wahusika wana lugha nzuri; huwa nawashauri pia rafiki zangu kwenda kwenye biashara za aina hiyo. Hivyo hakikisha unatumia mbinu hii ili kuongeza wateja.

Soma pia: Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa.

2. Huduma au bidhaa za bure

Wateja wengi wanapenda vitu vya bure au zawadi. Siyo lazima ufanye jambo kubwa la bure ili kuwavutia wateja; hata jambo dogo tu linaweza kuwavutia sana.

Ili kuwavutia wateja unaweza kutoa huduma au vitu vya bure kama vile kalamu, mifuko, shajara (diary) au hata maji ya kunywa. Kwa njia hii utawavutia wateja wengi zaidi.

3. Punguzo

Punguzo ni njia bora sana ya kukabiliana na ushindani wa kibiashara na kupata wateja. Ikiwa mwenzako anauza sabuni kwa shilingi 2,100, wewe uza 2,050. Unaweza usipate faida kubwa kwenye bidhaa moja lakini utapata faida kubwa kwenye mauzo ya jumla.

Kwa mfano ikiwa faida kwenye sabuni hapo juu ni sh. 100, muuzaji wa kwanza akauza sabuni 5 kwa sh. 2,100 atapata faida ya sh. 500.

Lakini wewe ukauza sabuni 20 kwa sh. 2,050 utapata faida ya sh. 1,000. Je huoni kuwa umeuza na kupata faida zaidi kutokana na kuvutia wateja wengi kupitia punguzo? Weka punguzo sasa.

4. Shindano

Siyo lazima uwe na pesa nyingi ndipo uweze kuendesha shindano. Unaweza kuendesha shindano lenye zawadi ndogo kama vile vocha, kalamu, mikoba, shajara au hata vinywaji.

Kwa njia ya kuweka shindano watu wengi watavutiwa kununua bidhaa au huduma zako ili wawe washindi. Unaweza pia kuweka bidhaa au huduma zako kama kitu cha kushindaniwa badala ya zawadi nyingine.

5. Anzisha tovuti au blog

Watu wengi hawafahamu umuhimu wa tovuti au blog. Wengi hufikiri kuwa ni mahali pakuweka matangazo ya watu wengine ili wakulipe.

Ukweli ni kuwa blog au tovuti ni muhimu sana kwa ajili ya kuongeza wateja kwa njia ya kutangaza biashara yako.

Ukiwa una blog nzuri yenye watembeleaji wa kutosha, unaweza kuitumia kutangaza na kuuza bidhaa zako wewe mwenyewe na ukajipatia pesa nyingi.

Soma pia: Njia 14 Halali za Kupata Pesa Kupitia Blog.

6. Tumia mitandao ya kijamii

Kama ilivyo kwa blog na tovuti, vivyo hivyo mitandao ya kijamii inaweza kutumiwa kuzalisha pesa nyingi.

Ikiwa unataka kuongeza wateja, basi wafahamishe watu kupitia mitandao ya kijamii juu ya huduma au bidhaa zako. Hakikisha wanazielewa na kuweza kuzifikia kwa urahisi.

Soma pia: Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao.

7. Matangazo

“Biashara ni matangazo.”

Biashara nyingi hupuuza nafasi ya kujitangaza ili kuongeza wateja na hatimae kupata faida zaidi. Siyo lazima utumie njia za gharama kubwa kujitangaza kwani zipo njia nyingi sana.

Unaweza kutumia mitandao (rejea mbinu ya 5 na 6), vifungashio, saini ya barua pepe (email signature), card ya utambulisho wa biashara (busness card), vipeperushi n.k.

8. Toa misaada

Je umeshawahi kujiuliza kwanini biashara na kampuni nyingi hutoa misaada mbalimbali? Je ni kwa kuwa wana pesa za ziada au wanawapenda sana wale wanaowasaidia?

Ni wazi kuwa hii ni mbinu nzuri sana ya kujitangaza na wala si vinginevyo. Kwa njia ya kutoa misaada wateja huongezeka zaidi kwani watu huifaahamu biashara husika, pia huichukulia kama biashara inayowajali zaidi.

Kumbuka siyo lazima utoe misaada mikubwa au ya pesa nyingi. Unaweza kutoa hata bidhaa zako au huduma yako kama msaada kwa watu au taasisi fulani.

9. Lenga changamoto

Watu wananunua bidhaa au huduma fulani ili itatue changamoto zao. Hivyo kuendesha biashara isiyolenga changamoto za wateja haitapata soko.

Hebu fikiri mtu anaanzisha duka la kuuza dawa za Ebola Kenya au Tanzania, je atapata wateja kweli? Ni wazi kuwa hatapata wateja kwani tatizo la Ebola kwa Tanzania na Kenya ni dogo sana.

Hivyo ili kuongeza wateja hakikisha unakuwa mbunifu na kulenga changamoto na mahitaji ya wateja.

Soma pia: Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara.

10. Shirikiana na biashara au kampuni kubwa

Hebu fikiri kampuni kama Vodacom au Airtel wakikutaja kwenye matangazo yao kuwa wewe ni wakala wao; je unafahamu ni nini kitatokea? Moja kwa moja utafahamika zaidi pamoja na kile unachokifanya na utaongeza wateja zaidi.

Kumbuka kushirikiana na kampuni au biashara nyingine kubwa hukufanya pia uaminike zaidi kwa wateja.

Hitimisho

Naamini sasa umeona jinsi unavyopoteza wateja na faida bila sababu yoyote ya msingi. Fanyia kazi mbinu jadiliwa hapo juu nawe kwa hakika utaweza kuongeza wateja na hatimaye kupata faida zaidi. Je wewe unatumia mbinu gani kupata wateja?

Tafadhali tuandikie maoni na maswali yako hapo chini, kisha washirikishe wengine makala hii. Usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

Washirikishe Wengine Makala Hii:

6
Tafadhali tuandikie maoni yako:

avatar
3 Comment threads
3 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
3 Comment authors
HAMZA KAZIBUREKornel M.Chrispo Michael Recent comment authors
newest oldest most voted
Chrispo Michael
Guest
Chrispo Michael

Nimefurah sana kwakuwa nimejfunza mbnu mbalimbali za kibiashara hvyo nitaendelea kufuatilia zaid

HAMZA KAZIBURE
Guest
HAMZA KAZIBURE

Join the discussion…nimejifunza…naomba namba zako ..au nichek 0621961707 , 0659883213

HAMZA KAZIBURE
Guest
HAMZA KAZIBURE

Join the discussion…Join the discussion…nimejifunza…naomba namba zako ..au nichek 0621961707 , 0659883213