Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara - Fahamu Hili
Wednesday, October 23Maarifa Bila Kikomo

Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Wazo la biashara

Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii.

Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako.

Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara.

1. Chagua wazo unalolipenda

“Fanya kile unachopenda na pesa zitakufuata.”

Marsha Sinetar

Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya.

Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto.

Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa.

2. Chagua wazo unalolifahamu na kulimudu

Watu wengi hufanya kosa la kuchagua wazo la biashara ambalo hawalifahamu vyema au kulimudu. Hii ni kutokana na kuiga, kukosa ubunifu au hata tamaa ya pesa.

Kumbuka ili wazo lifanikiwe ni lazima litekelezwe na mtu anayelifahamu vyema na kulimudu. Kwa mfano unaanzisha biashara ya hoteli huku ukiwa huna maarifa wa ujuzi wowote kuhusu uendeshaji wa hoteli; ni wazi kuwa hutoweza kufanikiwa.

3. Zingatia swala la fedha

Kila biashara inahitaji fedha ili kujiendesha. Hivyo hakikisha wazo la biashara unalolichagua utaweza kupata fedha za kutosha ili kulitekeleza.

Lifahamu wazo vyema kabla ya kuamua kulifanyia kazi, fahamu gharama zote zinazohitajika katika kulitekeleza pamoja na faida itakayopatikana. Kwa njia hii utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kama wazo linafaa au la.

Soma pia: Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo.

4. Angalia uhitaji wa soko

Watu wengi hawafahamu umuhimu wa kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapoangalia uhitaji wa soko ni wazi kuwa utachagua wazo la biashara ambalo litauzika.

Usichague tu wazo kwa sababu ni wazo au wengine wanalifanya, bali hakikisha wazo lako linahitajika sokoni katika wakati husika.

5. Ushindani

Ushindani ni jambo muhimu ambalo kila mtu anayechagua wazo la biashara anatakiwa kulizingatia, kwani kufanikiwa kwenye biashara kunategemea kiwango cha ushindani na jinsi utakavyokabiliana nacho.

Hakikisha unafahamu vyema ushindani kwenye wazo husika na unaweza kuumudu vyema. Hakuna haja ya kuchagua wazo ambalo unashindana na makampuni yaliyoenea ulimwenguni kote wakati wewe ni mjasiriamali unayeanza.

Soma pia: Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa.

Neno la mwisho

Kama nilivyoeleza hapo awali, uchaguzi wa wazo la biashara unahitaji utulivu na umakini mkubwa. Ni muhimu ukahakikisha kuwa wazo unalolichagua unalimudu vyema na linaweza kukupa faida ya uhakika katika eneo unalolilenga.

Usichague wazo kwa kuwa wengine wamelichagua au wengine linawapa faida; bali chagua lile linalokufaa wewe na mazingira yako.

Je una swali lolote kuhusu kuchagua wazo la biashara? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

Washirikishe Wengine Makala Hii:

4
Tafadhali tuandikie maoni yako:

avatar
2 Comment threads
2 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
3 Comment authors
Amoxry luckmiryKornel M.GEORGE SEMAGANGA Recent comment authors
newest oldest most voted
GEORGE SEMAGANGA
Guest
GEORGE SEMAGANGA

MUMEELEZA VIZURI SANA ,JE HUWA MNA KUWA NA SEMINA

Amoxry luckmiry
Guest
Amoxry luckmiry

Makala nzuri ila kuna haja ya kuongeza content zaidi, coz umezungumzia minner issues ambazo wengi wanazifaham.