Njia 9 za Kutangaza Biashara Yako Bila Pesa - Fahamu Hili
Thursday, February 22Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Njia 9 za Kutangaza Biashara Yako Bila Pesa

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Tangaza

Matangazo ni swala muhimu kwa kila biashara. Tatizo linatokea pale ambapo biashara inashindwa kumudu gharama za matangazo, hasa matangazo ya gharama kubwa.

Naamini wewe kama mjasiriamali unafahamu kuwa kuna wakati bajeti ya biashara inakuwa imebana. Hivyo swala la kujitangaza linakuwa na changamoto.

Fuatilia makala hii kwa karibu ili nikufahamishe njia 9 unazoweza kuzitumia kutangaza biashara yako bure au kwa gharama nafuu sana.

1. Tumia tovuti

Tovuti au blog ni njia rahisi na ya gharama nafuu ya kujitangaza. Ikiwa una blog au tovuti ambayo inaidadi nzuri ya watembeleaji, unaweza kuweka tangazo la biashara yako hapo na likaonekana kwa watu wengi zaidi.

2. Tumia mitandao ya kijamii

Kama ilivyo wenye njia ya blog, vivyo hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram n.k. ili kujitangaza.

Kumbuka hivi leo karibu kila mtu anatumia mitandao ya kijamii. Hivyo kutangaza biashara yako kupitia kurasa au akaunti zako za mitandao hii ni rahisi na utawafikia watu wengi zaidi.

3. Tengeneza vifungashio au zawadi ndogo

Siyo lazima uwe na pesa nyingi ndipo utoe zawadi au huduma ya vifungashio vyenye chapa yako. Unaweza kubuni na kuchapisha vifungashio vyenye jina na maelezo mafupi kuhusu biashara yako ili kujitangaza.

Unaweza kutoa zawadi ndogo kama vile kalamu au shajara (diary) vyenye maelezo ya biashara yako.

4. Tengeneza kadi za kibiashara na vipeperushi

Unapopewa kadi ya kibiashara (business card) au kipeperushi lengo lake hasa ni kujitangaza. Unaweza kutengeneza kadi za kibiashara pamoja na vipeperushi vyenye maelezo mafupi kuhusu biashara yako.

Naamini njia hii ni nafuu sana kuliko kuweka tangazo kwenye televisheni wakati wa habari.

5. Kuwa wakala wa biashara kubwa

Kuwa wakala wa biashara kubwa ni njia moja nzuri ya kujitangaza na kuongeza wateja. Mara nyingi biashara kubwa huwatangaza mawakala wao katika matangazo yao ya gharama kubwa.

Hivyo, kwa kuwa wakala wa biashara au kampuni kubwa kama vile makampuni ya simu, bima, dawa, pembejeo, au fedha; utakuwa umepata nafasi ya kutangazwa bure kabisa.

6. Hudhuria semina na makongamano

Njia nyingine nzuri na rahisi ya kujitangaza ni kwa kuhudhuria semina, makongamano au sehemu zenye mikusanyiko.

Uwapo katika maeneo haya, hakikisha unatafuta angalau nafasi ya kutoa salamu katika maeneo haya, ukipewa nafasi ya kuzungumza taja tu hata jina la biashara yako kwani ina maana kubwa sana. Unaweza kuvaa pia mavazi yenye maelezo au matangazo ya biashara yako.

7. Jitolee au toa misaada

Naamini mara kadhaa umewahi kuona wafanyakazi wa kampuni au biashara fulani wakitoa misaada au hata kujitolea kufanya kazi kama vile usafi wa mazingira.

“Hakuna chakula cha bure kwenye uchumi.”

Je ni nini hasa msingi wa swala hili? Kama wanauchumi wa kale walivyotangulia kusema kuwa hakuna chakula cha bure kwenye uchumi, vivyo hivyo matendo ya kujitolea au msaada yana lengo fulani.

Mara nyingi makampuni au biashara fulani zinapotoa misaada waandishi wa habari hurekodi na kutangaza habari hiyo. Hii ni njia nzuri sana ya kujitangaza.

8. Endesha shindano

Nani asiyependa kushinda? Naamini hata wewe unapenda kushinda zawadi fulani.

Ili ushinde unatakiwa kununua bidhaa au kusambaza habari kuhusu biashara fulani, je kwa njia hii hujaitangaza biashara hiyo? Naamini utakuwa umefanya hivyo tayari.

Unaweza kuendesha shindano dogo lenye zawadi za kawaida kama vile mikoba, vocha za simu, vinywaji, kalamu au hata bidhaa unazouza. Kwa njia hii utajitagaza kwa gharama nafuu kabisa.

9. Toa elimu au ushauri bure

Kama kuna elimu au ushauri fulani unaoweza kuutoa ambao unaendana na biashara yako; fanya hivyo sasa.

Kwa njia hii utafahamika na kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo kuitangaza biashara au huduma yako kwa urahisi na  kwa gharama nafuu kabisa.

Hitimisho

Kufanikiwa katika kitu chochote kunahitaji mikakati sahihi na ubunifu. Naamini umeona jinsi ambavyo unaweza kutumia njia mbalimbali kujitangaza kwa bei nafuu au bure kabisa.

Naamini hutoumiza tena kichwa kufikiri njia za kupata pesa nyingi kwa ajili ya matangazo ya gharama kubwa.

Soma pia: Mbinu 10 za Kuongeza au Kuvutia Wateja Kwenye Biashara

Ukiwa na swali au maoni tafadhali tuandikie hapo chini. Usisahau kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

3 3 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

4 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Agnes ngatuni
Agnes ngatuni
5 years ago

Hallow how are you.sijui hata nilikuwa nafanya nn had I nikakuta ninachokiita shule mtandaoni.najiona nimechelewa kupata hii shule.hope nimeanza ukurasa Mpya wa maisha kiuchumi.nilikuwa nawaza sana how to run a business in a very low capital nitafarijika sana kama utaendelea kuwa Mwl.au mentor walao nijikwamue kimaisha.hongera sana .you seem to be resource person

BABA EPIPHANIA
BABA EPIPHANIA
3 years ago

Nimependa Sana Nakala yako nzur Sana nimewahi Nunua vitabu vinavy husu Biashara lkn sijawahi Soma vitu vizur Kama hivy nilivyosoma na kujifunza kwako,hakika Biashara yang itakuw ya mwonekano wa Tofaut,Lugha Zur kwa Mteja na jinsia ya kucheza na sakolojia y Kila Mteja, Ubarikiw Sana Fahamuhili ubarikiw MAANGA

4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x