
Vitu 10 Ambavyo Kila Mzazi au Mlezi Anatakiwa Kumfundisha Mtoto Wake
Mzazi au mlezi ndiye mwalimu namba moja wa mtoto wake. Kwa kiasi kikubwa sana mtoto hujifunza na kuiga vitu au mambo mbalimbali kutoka kwa wazazi au walezi wake. Hivyo ni muhimu sana mzazi kuhakikisha anamfundisha mtoto wake mambo muhimu anayopaswa kujifunza ili akue katika malezi bora na awe na baadaye (future) njema. Kwa kutambua umuhimu wa mzazi au mlezi kumfundisha mtoto wake mambo kadhaa muhimu; karibu ufahamu vitu au mambo 10 ambayo kila mzazi au mlezi anatakiwa kumfundisha mtoto wake.
1. Matumizi mazuri ya muda
Matumizi ya muda ni swala muhimu kwa kila mtu, tena ni msingi wa mafanikio kwa kila mtu. Hivyo mzazi au mlezi anapaswa kumfundisha mtoto wake matumizi ya muda tangu akiwa mtoto ili akue akiwa na tabia hiyo. Mzazi au mlezi anapaswa kumfundisha mtoto wake maswala...