
Yafahamu Majengo 10 Marefu Zaidi Duniani
Dunia imeendelea kushuhudia uhaba mkubwa wa rasilimali mbalimbali kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu. Moja ya rasilimali ambazo zimekua adimu sana duniani kwa wakati huu ni ardhi, uhaba wa ardhi umefanya wahandisi kote duniani kuumiza vichwa vyao kufikiri namna ambavyo ardhi iliyopo itatumika vyema na kwa manufaa zaidi kwa wengi. Pamoja na sababu nyingine lukuki, ufinyu wa ardhi umechangia kwa kiasi kikubwa kujengwa kwa majengo marefu na ya kushangaza katika maeneo mbalimbali duniani. Yafuatayo ni majengo kumi marefu zaidi duniani maarufu kama sky scrapers kwa lugha ya kimombo.
10. International Commerce Centre
Jengo hili linashika nafasi ya kumi kwa majengo marefu zaidi duniani. Lina urefu wa mita 484 pamoja na ghorofa 108; lilijengwa mwaka 2010.
09. Shanghai worl...