Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo - Fahamu Hili
Thursday, March 30Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Mfanya biashara

Watu wengi wamekuwa wakitamani kuanza biashara lakini wanafikiri namna ya kuanza kwani mtaji wao ni mdogo sana.

Usiogope; kuwa na mtaji mdogo au kutokuwa nao kabisa sio mwisho wako wa kutimiza malengo yako.

“Usilie juu ya kile ambacho huna; tumia vizuri kile ulichonacho.”

Reginald Mengi

Zipo mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukuwezesha kufanya biashara hata kama utakuwa na mtaji mdogo. Tafadhali fuatilia hoja jadiliwa hapo chini kwa ufafanuzi zaidi.

1. Kuwa mbunifu

Moja kati ya mambo ambayo yatakusaidia sana kwenye kuanza biashara kwa mtaji mdogo ni ubunifu. Kwa njia ya ubunifu utaweza kushinda biashara na bidhaa zilizoko sokoni kwa urahisi zaidi. Unaweza kufanya haya yafuatayo:

  • Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema. Hili litakusaidia kukabili changamoto vyema.
  • Angalia tatizo au uhitaji uliopo sasa na uutatue kwa bidhaa au huduma yako.
  • Panga bei vizuri; unaweza kuweka bei ambayo ni tofauti kidogo na bidhaa au huduma ambazo tayari ziko sokoni ili uwavutie wateja.

Kwa kufanya mambo yaliyoelezwa hapa juu utaweza kukuza biashara na mtaji wako kwa muda mfupi zaidi.

2. Anza na unachokijua

Unapokuwa na mtaji mdogo huhitaji kuhusisha mambo mengi mageni au yanayotegemea sana watu wengine kwa kuwa huna pesa za kuyagaramia.

Kwa mfano kama unaanzisha biashara ya ushonaji basi anza kutengeneza mavazi yale unayoyaweza kwa kutumia vifaa ulivyonavyo; kwa njia hii utajenga mtaji wako kisha baadaye utaweza kuajiri wengine watakao kuwezesha kutengeneza aina nyingine zaidi.

Unapofanya kile unachokijua gharama huwa haziwi kubwa sana kwani ni kitu unachokimudu mwenyewe.

Soma pia: Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara.

3. Waambie watu unachokifanya

Waambie watu unachokifanya kwani hili litakuwezesha kupata wateja na kufahamika. Watu wakijua unachokifanya watatamani kukifahamu zaidi; hili litakuwezesha kupata wateja na kuongeza mtaji wako.

Usiogope kueleza kuwa unafanya biashara ya mboga, chakula, duka dogo la bidhaa n.k. Kwani hujui unaemweleza atakuwa nani kwenye biashara yako.

Ukiwa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii waeleze pia juu ya kile unachokifanya.

4. Epuka gharama zisizokuwa za lazima

Kwakuwa bado una mtaji mdogo jitahidi kuepuka garama zisizo za lazima kama vile ofisi ya kifahari, matangazo ya gharama kubwa n.k.

Kuwa na matumizi mazuri ya fedha hasa kwa mambo ya msingi tu. Watu wengi wameshindwa kwenye biashara kwa sababu wameanza biashara kwa mbwembwe za matumizi badala ya huduma bora zenye ubunifu.

5. Fanya kazi kwa bidii

Kamwe huwezi kuona mafanikio kama hutofanya bidii. Kumbuka wewe ni mjasiriamali anayeanza hivyo ni lazima ufanye bidii ili soko litambue kuwa upo pia unaweza.

Tumia muda vizuri, pia hakikisha unatoa huduma yenye ubora wa hali ya juu kwa bei ambayo wateja wataweza kuimudu. Jitese kwa muda mfupi kwa kipindi cha kuweka msingi wa biashara yako kwani hata kipindi cha kupanda katika kilimo huwa ni cha taabu.

Soma pia: Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa.

6. Tumia rasilimali na fursa zilizopo

Njia nyingine itakayokuwezesha kuanza biashara ukiwa na mtaji mdogo ni kutumia fursa zilizopo. Kumbuka kuwa huwezi kutengeneza fursa kama huwezi kutumia fursa zilizopo.

Tumia fursa kama vile mitandao ya kijamii ili kujitangaza. Pia unaweza kutumia udhaifu uliopo katika biashara nyingine za watangulizi wako kama fursa kwani unaweza ukarekebisha udhaifu huo kupitia biashara yako.

Zipo pia fursa za mikopo yenye masharti nafuu ambayo itakuwezesha kuongeza mtaji wako. Kumbuka unahitaji kutumia mkopo kwa makini kwani utahitajika kuurudisha pamoja na riba tena kwa wakati.

7. Jali wateja

Kujali wateja katika biashara  ni jambo muhimu sana kama unataka kuona matokeo chanya. Siku zote ninapenda kusema “wateja hufugwa”. Wateja hufugwaje? Hufugwa kwa huduma nzuri.

Waheshimu wateja wako pia hakikisha unatimiza na kumaliza haja zao katika ubora wa hali ya juu. Kumbuka siku zote mteja huja kwanza kabla ya pesa; hivyo usitangulize pesa kabla ya huduma nzuri kwa mteja.

Ukilifanyia kazi hili utaweza kukuza biashara na mtaji wako kwa muda mfupi.

Soma pia: Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka.

Hitimisho

Zilizojadiliwa hapa ni mbinu saba zitakazokuwezesha kuanza biashara na mtaji mdogo. Usiogope unaweza hata kama una kiasi kidogo sana cha fedha.

Thubutu, nza, fanya bidii, weka nidhamu, mtangulize Mungu na hakika utaona mafanikio chanya katika biashara yako.

“Anzia ulipo.Tumia ulicho nacho. Fanya unachoweza.”

Arthur Ashe

Bado umekwama katika eneo la kuwa na mtaji mdogo? Tafadhali tupe maoni yako; pia karibu uwashirikishe wengine makala hii. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

 

4.1 11 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
guest

62 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Michael mstafa
Michael mstafa
5 years ago

Nashukuru kwa elimu nzuri, ila kuna mambo ningependa kuuliza kutoka kwako kama hutojali
Namba yangu 0759428***

Machi Jacob
Machi Jacob
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Nataka kuwa wakala

Paul
Paul
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Hey kaka

Frank laurent
Frank laurent
Reply to  Michael mstafa
3 years ago

Uliza

Michael katuri
Michael katuri
5 years ago

Kwanza niwashukuru watoa mawazo mazuri hapo hujuu kwan wamenifungua akili vzr.mm nina tatizo la kukata tamaa mapema je nifanyaje? naombeni msaada wenu

Nelly chriss
Nelly chriss
4 years ago

Asanteni kwa ushauli wenu

Rajabu Seph Rajabu
Rajabu Seph Rajabu
4 years ago

Chamuhimu ni kujua nini unapenda kufanya napia sio pesa ndio ufanye biashara ila mawazo kwanza.

amos. festo
amos. festo
4 years ago

Its okay and fantastic

ramadhani makwisa
ramadhani makwisa
3 years ago

hakika nimejifunza vitu vizuri hapa

Frank laurent
Frank laurent
3 years ago

Mada nimeielewa nilikua nashindwa jinsi ya kuanza sasa nimepata mwanga ninamtaji wa kiasi cha laki najifikilia cha kufanya bado xijapata jibu naomben mawazo nifanye mini?

Nickson francis
Nickson francis
3 years ago

ndg nashukukru kwa somo lako zuri najua nitayafanyia kazi

Amos Wambahu
Amos Wambahu
3 years ago

Elimu yako iko vizuri.Je,ukiwa na 50000 Unaweza kuanza mtaji?

Matthew Zechariah
Matthew Zechariah
3 years ago

Asante sana kwa ushauri mzuri kuhusu ujasiriamali.

Kulwa mrisho
Kulwa mrisho
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Asante KWA ushauli mm namtaji wa30000 nitafanyaje

Dede sheke
Dede sheke
3 years ago

Nashukur Sana kwa elimu hii nataka kuwa mfanya biashara was nguo nitaifanya sehemu gani?

Dede sheke
Dede sheke
3 years ago

Nashukur Sana kwa elimu hii nataka kuwa mfanya biashara was nguo nitaifanya sehemu gani hiyo maana naona sehemu zote Kuna ushindani Sana na mm Sina mtaji was kutosha kumudu huo ushindani

Lizyberth
Lizyberth
3 years ago

Nashukuru kwa somo zurii sana nimefurah saana kupata elimu hii pia Nina maswali machache nahitaji kuuliza

Lugano Mwakalo Israel
Lugano Mwakalo Israel
2 years ago

Naweza kuwa wakala wa M-pesa kwa mtaji wa 100,000?

Aisha endrew
Aisha endrew
2 years ago

Nataka kufanya biashara ya uwakala mpesa,tigo pesa unanishauri Nini?

lucas chambika
lucas chambika
2 years ago

Nimefarijika sana na elimu unayotoa MUNGU azidi kukupa nguvu ili uzidi kutuelimisha..
Napendekeza ungeazisha na group la whatsap ili tuwe karib nawe zaid😊

Catherine
Catherine
2 years ago

Mmh asante Ila nahitaji kujua zaidi kabisa natumaini nitazidi kukufuatilia kwani

Susan
Susan
2 years ago

Nimeshukuru

Irene
Irene
2 years ago

Asanteni kwa ushauri wenu mim Ni mfanya bihashara ila hii bihashara tuna share watu wa will sasa mwenzangu mda mwingi anakuwa anahusika na mimi mda mwingine nakuwa kazini niliko ajiliwa ila inapotokea kama kuhusika kifedha uwa nahusika bila tatizo kama kuna pesa inaitajika ili kupiga hatua kibihashara kinacho nipa hofu Sasa Ni wakati wa kuibland bidhaa yetu yeye ndio anae jitambulisha zaidi ata kutoa mawasioiano anatoa contakti moja tu ambayo Ni yake mfano kwenye nembo ya bihashara , vipeperushi, ata business card yaan kiujumla hakuna kitu chochote kinachoonyesha kuwa na mim Ni muhusika je happy nini nifanye nahisi italeta shida… Read more »

Idanes
Idanes
2 years ago

Thnks

Daniel laurent
Daniel laurent
2 years ago

Mm nimuajiliwa ninauwezo wa kupata mtaji mdogo lakn sjui nifanye biashala gan yaan hapo tu ndpo mm nakwama

Elinipendo M Godwin
Elinipendo M Godwin
2 years ago

What are business which does not involve any capital?

Kimaro Elimringi
Kimaro Elimringi
2 years ago

Je, ni gani yakuweza kupata mikopo kuongezea mitaji midogo tuliyonayo?

Joshua
Joshua
2 years ago

Njemaa

Joshua
Joshua
2 years ago

Ahsante saana kwa ushauri mzur

Alfayo Mpagike
Alfayo Mpagike
1 year ago

Mungu akubariki Mimi tayari ni mjasiriamali wa genge dogo la mahitaji madogomadogo ya nyumbani nashukuru Kwa Elimu nzuri

Hero de Ngwikwi.
Hero de Ngwikwi.
8 months ago

Kiukweli, nimejifunza vingi na kupata ujasiri wa kile nachokwenda kukifanya..MUNGU ATUTANGULIE SOTE..BILA KURUDI NYUMA.

62
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x