
Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa
Hakuna mtu anayeanzisha biashara akitegemea ife, lakini wakati mwingine hili hutokea. Utafiti umebaini kuwa biashara na kampuni nyingi hufa ndani ya kipindi cha miaka miwili hadi mitano tangu kuanzishwa kwake. Kufa kwa biashara siyo jambo zuri, ni wazi kuwa kila mtu nayefanya biashara atatamani kufanya juu chini ili ainusuru biashara yake isife. Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha biashara mbalimbali kufa. Fahamu sababu 13 zinazosababisha biashara nyingi kufa pamoja na jinsi ya kuziepuka.
1. Mipango duni
Ili ufanikiwe katika biashara unahitaji mpango mzuri wa biashara. Biashara nyingi zinazoanzishwa Afrika hazina mipango madhubuti ya kibiashara inayoonyesha maswala kama vile muundo wa utawala, mtaji, mikakati au mipango ya mauzo, n.k Biashara nyingi pia hukosa lengo; jambo a...